Ushauri kwa serikali kuhusu tembo waharibifu

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
Jana nimefungua facebook nikaona mkurugenzi mmoja wa wanyama pori ametoa wazo kuwa serikali itoe kibali tembo wanaoharibu mazao kwa sasa wauwawe.

Mimi kama mzalendo sikubaliani na wazo hili kwa sababu tutakuwa tunatatua tatizo moja tunaunda lingine.Tutajenga mawazo mabaya kwa majangili kuwa sasa ruksa.

Naomba aliyetoa wazo hili asisulubiwe naye japo ni mkurugenzi ana mawazo yake

Nashauri zitumike mbinu za kisayansi kudhibiti hali hii kama ifuatavyo
1.Askari wa germ watumie mbinu kuwarudisha watokako
2.Waweke mizinga ya nyuki

Tembo na ukubwa wake lakini anaogopa sana nyuki.Tembo ana uwezo wa kusikia sauti ya nyuki popote alipo na akiisikia anakimbia.

Pia tujaribu kutafuta vitu ambavyo tembo havipendi tu m discourage kwa wadudu tungetumia wataalamu wa Sokoine chuo kikuu ila kwa wanyama nadhani wataalam wa wildlife wanafahamu.

elephant.JPG
 
Tatizo ni kuongezeka kuzidi uwezo wa maeneo yao ya asili au kutokana na changamoto za tabia nchi yale maeneo ambayo wangeweza kupata maji na malisho hayawezi kuwatosheleza.

Ni rahisi nyumbu kupungua kwa kufa mto Mara au kuwindwa, je, tembo wanapungua kwa mechanism ipi? Je, waachwe tu waendelee kuongezeka na kuleta uharibifu wa mazao na kuua wananchi?
 
uko sawa ila sasa tukiwaua idadi ya tembo itapungua hivi unajua wakati tunapata uhuru tulikuwa na tembo wangapi na kwa sasa wamebaki wangapi? kuna mbinu nyingi mno hata electric fence
 
Eti kupunguza tembo kwa kuwaua

Dunia itatushangaa

Ova
 
Bora angeshauri tuwauze kwa mabeberu tu
 
Wanadamu ndio wanavamia maeneo ya tembo. Tembo huishi maeneo yake ya asili tu. Leo utamuona mvamizi lakini actually vizazi vyake vilipita maeneo hayo.
 
Eti kupunguza tembo kwa kuwaua

Dunia itatushangaa

Ova
Tukumbuke kwamba kwenye sayansi ya wanyamapori kuna kitu kinaitwa kupunguza wanyama pale inapoonekana wamezidi levels fulani ili kuondoa human - wildlife conflicts. Hivyo kupunguza wanyama kwa kuwauwa na kutumika kama kitoweo kama analiwa siyo jambo geni. Uvamizi wa tembo kwenye mashamba ya wakulima umekuwa mkubwa sana jambo ambalo linafanya jamii iwe na negative attitude towards conservation.
 
Tatizo ni kuongezeka kuzidi uwezo wa maeneo yao ya asili au kutokana na changamoto za tabia nchi yale maeneo ambayo wangeweza kupata maji na malisho hayawezi kuwatosheleza.

Ni rahisi nyumbu kupungua kwa kufa mto Mara au kuwindwa, je, tembo wanapungua kwa mechanism ipi? Je, waachwe tu waendelee kuongezeka na kuleta uharibifu wa mazao na kuua wananchi?
Ndio maana Magu alikuwa anawasambaza kwenye mapori ya akiba. Unakuta burigi hakuna tembo hata wa dawa lakini tarangire wametapakaa kila mahali.
 
Eti kupunguza tembo kwa kuwaua

Dunia itatushangaa

Ova
unaona aiseee
kwanza Tembo ni endangered species halafu mtu anasema tuwapunguze.
Wale tembo waliokuwa na manyoya miaka 5000 wako wapi?
Mnataka na hawa tulio nao wapotee?
Sayansi itumike binadamu amejaliwa akili kuliko wanyama
 
Attachments

  • mamoth.JPG
    mamoth.JPG
    10.6 KB · Views: 5
Tatizo ni kuongezeka kuzidi uwezo wa maeneo yao ya asili au kutokana na changamoto za tabia nchi yale maeneo ambayo wangeweza kupata maji na malisho hayawezi kuwatosheleza.

Ni rahisi nyumbu kupungua kwa kufa mto Mara au kuwindwa, je, tembo wanapungua kwa mechanism ipi? Je, waachwe tu waendelee kuongezeka na kuleta uharibifu wa mazao na kuua wananchi?
Nawewe una uhakika kuwa wameongezeka? Takwimu ziko wapi? Kuingia katika makazi ya watu kuna maana nyingi. Moja, watu waweza kuwa wamesogelea corridors za wanyama hao. Mbili, shughuli za binadamu kama uchomaji wa malisho, uwindaji na uharibifu wa vyanzo vyao vya maji vyaweza kuwafanya tembo kutoka katika makazi yao ya asili
Sasa wewe unaposema wameongezeka bila kutoa takwimu tukueleweje?
 
Jana nimefungua facebook nikaona mkurugenzi mmoja wa wanyama pori ametoa wazo kuwa serikali itoe kibali tembo wanaoharibu mazao kwa sasa wauwawe.

Mimi kama mzalendo sikubaliani na wazo hili kwa sababu tutakuwa tunatatua tatizo moja tunaunda lingine.Tutajenga mawazo mabaya kwa majangili kuwa sasa ruksa.

Naomba aliyetoa wazo hili asisulubiwe naye japo ni mkurugenzi ana mawazo yake

Nashauri zitumike mbinu za kisayansi kudhibiti hali hii kama ifuatavyo
1.Askari wa germ watumie mbinu kuwarudisha watokako
2.Waweke mizinga ya nyuki

Tembo na ukubwa wake lakini anaogopa sana nyuki.Tembo ana uwezo wa kusikia sauti ya nyuki popote alipo na akiisikia anakimbia.

Pia tujaribu kutafuta vitu ambavyo tembo havipendi tu m discourage kwa wadudu tungetumia wataalamu wa Sokoine chuo kikuu ila kwa wanyama nadhani wataalam wa wildlife wanafahamu.

View attachment 2355219
unapinga kwa kuwa wewe si mkulima, na hivyo una upeo finyu wa madhara ya tembo kwa mkulima anayetegemea mazao kama mshahara wake.

unapaswa kujua kuwa kama ambavyo wewe mwenye ajira unavyoumia unapoachishwa kazi ghafla, mkulima analia na kufa nafsi mazao yake yanaposhambuliwa na wanyama kama tembo.
 
Back
Top Bottom