Kwanza tunamshukuru Mungu kwa uzalishaji mkubwa wa zao la mpunga kwa msimu huu. Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wananchi wamepata mavuno makubwa ya mpunga. Kwa sasa bei ya mchele inazidi kuteremka na ninaambiwa kuwa maeneo ya Katavi kilo moja ya mchele umefika Tshs. 600.
Pia wafanyabiashara wageni kutoka Uganda, Kenya wameanza kuingia maeneo ya Mkoa wa Mara, Simiyu, Shinyanga na Mwanza wakiwarubuni wakulima kuuza mpunga wao kwa bei ya kutupa. Ushauri wangu kwa Serikali, ni vema Serikali ikachukua uamuzi wa busara kununua mpunga wote toka kwa wananchi kwa bei rafiki kama Tshs. 80,000 kwa gunia la kilo 100 kuliko kurubuniwa na walanguzi wanaowarubuni kuuza gunia moja kwa Tshs.30,000.
Ninajua kuna dhana ya supply and demand lakini kwa Serikali inayojali wananchi wake ni vema ikaingilia kati. Tumeona Serikali ikinunua mazao kama mahindi vivyo hivyo wafanye kwa mpunga. Mpunga watakaonunua unaweza kuuzwa kwa dola ya Marekani kwa faida kubwa. Mhe. Bashe wasaidie wakulima wa mpunga.