Ushauri kwa Serikali: Kuliko kutozana pesa ya Bima ya Afya in lump sum, tozo zirudishwe kwa ajili ya Bima ya Afya kwa wote

Ushauri kwa Serikali: Kuliko kutozana pesa ya Bima ya Afya in lump sum, tozo zirudishwe kwa ajili ya Bima ya Afya kwa wote

Serikali ina uwezo wa kuwapa wananchi wake wote Bima ya afya bila Tozo kwasababu ina Rasilimali za kutosha ni vile tu basi.
Nyie ndio tukenge,wewe uliye na shamba hapo linakusaidia nini kama huna uwezo wa kuliendeleza?

Kwa hiyo serikali isubirie wawekezaji waje kuendeleza ndio tupate Bima wakati tunaweza kuanza na Bima kwa kutumia tozo.
 
Tozo ni muhimu sana kwa ajili ya Bima maana hata ukibisha na kupiga ngumi ukuta lazima utalipa Bima utake au usitake.

Sasa elewa hivi , hizo tozo zimefutwa kuanzia tarehe 1/10/2022.
Kwani zimepingwa tena kwa facts hadi waliozianzisha wakaamua kuzifuta.
Hizo tozo kuanzia kesho hazipo hivyo embu andika topic za maana
 
We bang

Waumie wafanya miamala ya mara kwa mara we ukafaidike na maumivu ya wengine kupata bima? Kuna watu mwaka mzima kafanya muamala wa pesa hauzidi mara 10 tu, mwingine kwa mwezi tu hata mara 5+. Hebu wawe na strategies za kila mnufaika kuona anawajibika na ulipaji wake.
Ndio ni kawaida hiyo kwani unadhani Bima ya Afya wanayokatwa watumishi wote wanaenda hospital? Ni asilimia chache wanaenda hospital ila inafaidisha wengine pia..

So ndio inavyotakiwa hivyo kwani hata Kodi iko hivyo unapo trade zaidi unakatwa zaidi.
 
Sasa elewa hivi , hizo tozo zimefutwa kuanzia tarehe 1/10/2022.
Kwani zimepingwa tena kwa facts hadi waliozianzisha wakaamua kuzifuta.
Hizo tozo kuanzia kesho hazipo hivyo embu andika topic za maana
Tozo zipi zilizofutwa? Nenda Banks Katoe pesa zaidi ya 30,000 hiyo kesho afu uje na hadithi zako hapa.
 
Tozo zipi zilizofutwa? Nenda Banks Katoe pesa zaidi ya 30,000 hiyo kesho afu uje na hadithi zako hapa.

Hujielewi wewe jamaa,kabla ya hapo ilikuwaje?
Kwani lazima kila mtu atoe zaidi ya elfu 30?
Unaweza pia kumwamishia mtu fedha kwenye akaunti ya benki
 
Kuna mtu asiyefanya miamala kwenye simu? Watalipiwa na wengine kama ilivyo kwa watumishi na wategemezi au mtu mwaka mzima hajaenda hospital lakini anakatwa.

Cha msingi kila mtu awe na Bima

Kwa hiyo unataka kusrma kabisa kila mtu anafanya miamala?
 
Hujielewi wewe jamaa,kabla ya hapo ilikuwaje?
Kwani lazima kila mtu atoe zaidi ya elfu 30?
Unaweza pia kumwamishia mtu fedha kwenye akaunti ya benki

Kwa hiyo unasema zimefutwa au zimepunguzwa?
 
Aisee mimi nashauri Serikali iachane na mambo ya elimu bure, kila mtu asomeshe mtoto wake aliyezaa labda kwa zile familia masikini sana zilizopo kwenye tasaf

Hiyo hela itakayookolewa itumike kutoa bima ya afya kwa wote
Sahih kbsa Ni Bora kuboresha ktk afya kwa kufuta elmu bure kila mtu apambnane na mwanae ndio tutafanya kazi Kweli kweli

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Sasa kwa wale ambao hawatumii bank na hawafanyi miamala watakuwa wanalipa vipi? Na ikumbukwe kwenye matumizi ya miamala ya simu na bank kila mtu ana matumizi yake!

Kiufupi hoja yako ni kwamba serikali higharamie swala la bima ya afya kwa wote ...
mbona mtoto wako anatibiwa kwa makato yako ya bima hapo na maana halisi mkuu ya kuwepo watu tegemezi iyo ipo hata ulaya na kwengine cost sharing ni nafuu itapunguza mzigo mkubwa mana hata mfanyabiashara pia atakuwa ameusika kwenye makato ya bima ya afya wazo zuri mno fikilia kwa undani zaidi mkuu
 
Mleta mada ni mtu wa hovyo sana!! Bandiko lako linathibitisha jinsi nchii hii ilivo ngumu!! Unashauri bima ilipwe kwa lumpsum lakini pia chanzo cha bima hiyo iwe ni tozo kutoka kwa banks na miamala!! Na bila aibu unaona mambo hayo yanahusiana!!

Jiulize maswali haya:
a) Kama itakuwa ni lazima kila mtanzania kuwa na bima ya afya na chanzo cha funding ikawa ni hizo tozo, je unasema kila mtanzania ana bank account na pia anafanya miamala ya simu?? Mtoto wako mdogo anayehitaji huduma za afya ana simu na account ili awe mchangiaji?
b) Dhana yako ya kuchangia kupitia tozo haitofautiani na ya uongo ya kijamaa kuwa huduma za afya zinatokewa bure! Bima ni uthibitisho kuwa huduma za afya si bure tena. Na kuwa zitachangiwa na kila atakayezipokea. Swali - je tozo za miamala na banks (ambazo zinalipwa na wachache) zinatosha kugharimia “kwa haki” mahitaji ya taifa zima? Zingatia - chini ya asilimia 20 ya watanzania wana bank accounts.

Iwe lumpsum au one payment, bima ya afya lazima ichangiwe na kila mgonjwa mtarajiwa - hata kama si yeye anailipia (mfano watoto vis-a-vis wazazi au waangalizi wao).

Sidhani unajua concept nzima ya bima ya afya. Ninaona unaangalia jambo dogo la lumpsum!! Ungetumia muda/nafasi yako kuwafundisha watu kuwa mchango mdogo kabisa wa bima maana yake ni gharama ndogo kabisa italipwa na bima na mgongwa akihitaji gharama kubwa katika matibabu - itapaswa kulipia kutoka mfukoni mwake!!!
 
Serikali imekusudia kuanzisha Bima ya Afya kwa wote Kwa kuitungia Sheria kuwa lazima.

Na kwa Mujibu wa Waziri wa Afya, Bima itaambatanishwa na huduma zingine kama leseni nk.

Aidha kutakuwa na vifurushi vya Bima na mtu atalazimika kuchangia pesa kwa lumpsum kiwango atakachochagua.

Sasa binafsi naona hiyo italeta usumbufu Sana na kufanya bima isiwe effective.

Naishauri Serikali iunde Bodi ya Kusimamia Bima ya Afya na iwe na chanzo chake cha mapato ambacho kiwe ni tozo zote za banks na za miamala ya simu Ili kupata pesa badala ya kuchangia kwa lump sum.

Chukulia bima ya 30,000 au 50,400 imeshindikana kuoatikana sembuse hiyo ya kuchangia?

Tozo zirejeshwe kwa ajili ya Bima ya Afya.
Nakubaliana na mchangiaji,unaweza ukawekwa utaratibu wa mfumo utatambua kila mchangiaji atachingia kutokana na matumizi yake ya simu,anapafanya miamala anajua anachangia bima ya afya, mfumo ukiwepo michango itatambulika kupitia namba ya mtimiaji, pia itampandishi kiwango Cha matibabu kutokana na matumizi yake ya miamala ya simu.
 
Mleta mada ni mtu wa hovyo sana!! Bandiko lako linathibitisha jinsi nchii hii ilivo ngumu!! Unashauri bima ilipwe kwa lumpsum lakini pia chanzo cha bima hiyo iwe ni tozo kutoka kwa banks na miamala!! Na bila aibu unaona mambo hayo yanahusiana!!

Jiulize maswali haya:
a) Kama itakuwa ni lazima kila mtanzania kuwa na bima ya afya na chanzo cha funding ikawa ni hizo tozo, je unasema kila mtanzania ana bank account na pia anafanya miamala ya simu?? Mtoto wako mdogo anayehitaji huduma za afya ana simu na account ili awe mchangiaji?
b) Dhana yako ya kuchangia kupitia tozo haitofautiani na ya uongo ya kijamaa kuwa huduma za afya zinatokewa bure! Bima ni uthibitisho kuwa huduma za afya si bure tena. Na kuwa zitachangiwa na kila atakayezipokea. Swali - je tozo za miamala na banks (ambazo zinalipwa na wachache) zinatosha kugharimia “kwa haki” mahitaji ya taifa zima? Zingatia - chini ya asilimia 20 ya watanzania wana bank accounts.

Iwe lumpsum au one payment, bima ya afya lazima ichangiwe na kila mgonjwa mtarajiwa - hata kama si yeye anailipia (mfano watoto vis-a-vis wazazi au waangalizi wao).

Sidhani unajua concept nzima ya bima ya afya. Ninaona unaangalia jambo dogo la lumpsum!! Ungetumia muda/nafasi yako kuwafundisha watu kuwa mchango mdogo kabisa wa bima maana yake ni gharama ndogo kabisa italipwa na bima na mgongwa akihitaji gharama kubwa katika matibabu - itapaswa kulipia kutoka mfukoni mwake!!!
Unaongea pumba tuu,kwani Tozo zinaingiza Bei gani? Wengine wameenda bali zaidi kutaka vileo ndio vichangie na sio lumpsum ya mtu binafsi.

Kipi Bora kutumia tozo au hii 84,000 iliyowekwa kwa kichwa?👇
 
Attachments

  • 20221008_152432.jpg
    20221008_152432.jpg
    193.8 KB · Views: 2
We usituchanganye, watafute vyanzo vingine sio tozo....
 
We usituchanganye, watafute vyanzo vingine sio tozo....
Vyanzo vingine utalipa wewe na wamepanga kila kichwa 84,000 sasa linganisha Kati ya tozo na hiyo kwa kichwa..

Kama una familia ya watu 5**84,000 ndio utajua hujui..

Kama toto Afya Card ya 50,400 mlishindwa lipeni hiyo Sasa na ni lazima.👇
 
Attachments

  • Screenshot_20221008-151811.png
    Screenshot_20221008-151811.png
    104.6 KB · Views: 2
Huwezi weka bima ya afya au kuanzisha Bima ya afya kwa wananchi na nchi maskin mambo mengne serikali iache kutafta pesa kwa lazma na kwa matumizi yake binafsi kwa kusingizia kuanzisha bima ya wananchi

Serikal iboreshe kwanza huduma na maisha ya wanachi wake kwanza ndo ianzishe bima
Iboreshe
Huduma za afya
Maji na umeme
Kipato cha wananchi
Mishahara ya wafanyakazi
Uzazi wa mpango na huduma za mama na mtoto, nk

Wafanyakazi wa serikal na wale wa sekta binafsi ni group ndogo sana kulinganisha na idadi ya watanzania wote sasa km izo bima za afya zilizo azishwa kwaajiri ya wafanyakazi wa serikal na wale wa sekta binafsi zimeshindwa kutoa matokea chanya na zimeshindwa kutoa suluisho sasa hii ya wanachi wote ndo itafanikiwa

Wacha tusiwe wachawi na wapinga maendeleo wacha Mchakato uje wananchi km kawaida yetu tutachangia iyo Bima ya afya sabu itakua ni sheria

Ushauri wa bure tutafte pesa uduma nzuri utaipata ukiwa na pesa ila sio izo kadi za Bima ya afya
 
Back
Top Bottom