Ushauri kwa Simba SC: Kamwe msiingize kikosi cha kwanza katika mechi yenu na Yanga SC

bizplan

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
592
Reaction score
574

Timu ya Simba pokeeni ushauri huu.

Kwa kuwa mna kikosi kipana na kizuri, tumieni kikosi cha pili kucheza na Yanga.

Kwa nini?

1. Katika kipindi hichi ambacho mmepata mafanikio timu ya Yanga itakamia mechi ili kuonyesha kuwa na wao ni bora.
2. Ikiwa mechi hii ikamiwa hivyo inaweza kuwaacha na majeruhi wa kutosha au kuwakosa wachezaji wenu muhimu.
3. Mkiwakosa wachezaji muhimu mjue Kaizer Chiefs anawatoa kiulaini.
4. Pia hamuwezi jua ikiwa Kaizer Chiefs watatumia mbinu kupitia kwa mchezaji mmoja mmoja kuwatengenezea majeruhi.

Ushahidi: Mliona vile Prison iliwakamia katika ule mchezo wa kwanza.

Suluhisho:
Kwa kuwa tayari mnaongoza ligi, na kwa kuwa bado mnaweza kuwa mabingwa wa ligi, na kwa kuwa mnataka haswa kuingia nusu fainali na hata fainali,

MSIINGIZE KIKOSI CHA KWANZA.

Kama hamtaki, BASI.
 
Hii ni mechi nyepesi sana sijaona mchezaji wa utopolo wa kuisumbua Simba pale.

Kikosi cha kwanza lazima kiingie maana tunataka ushindi mnono hatutaki ushindi wa goli 2-0 tunataka ule ushindi wa kuanzia 4.
 
Lakini ni mechi nzuri ya mwalimu kuiweka gameplan yake kwenywe majaribio. Kumbuka kila mpinzan ana mpira tofaut saaa ili mwalimu ajiridhishe kuwa plan yake wachezaj wameielewa basi ni lazima aijaribu kwenye mechi tofaut. Ukiangalia toka mwanzo simba plan zote za mechi za caf walikuwa wanajaribu kwenye mechi za vpl.

Ila mi naona mambo ya kuogopa sijui wapinzan watasoma mbinu wachezaj wa kikos A wakae bench ni ya kizaman. angalia ulaya huko kina man city wanataka ubingwa na wako uefa na wachezaji ni wale wale.. kuumia kwa wachezaj kama ni makusud itaonekana na wanaweza wakaumizwa na bado simba ikashinda kwa Kaizer.

Kikubwa jitihada na Dua
 
Nilichojifunza kwa huyu Kocha wa Simba(Gomes) wala hanaga tabia ya kuzarau Mechi, yeye game zote anapanga full mziki.
Anachokifanya ni kusoma uwezo wa timu anayocheza nayo na kubadili game plan tu.

Kwa mechi hii ya Yanga atawaambia watafute kwanza goli kisha warelax kwa kuuchezea mpira. Hivyo hii game wala haitakuwa na magoli mengi ila itakuwa ni game ya pasi nyingi za kuburudisha watu wa majukwaani.

Ni mechi inayomfaa sana Benard Morson.
 
Muingize kikosi cha pili ili mkifungwa mpate kisingizio..au siyo!???...

Nimejua janja yako...
 
Wana simba mna uhakika sana..

Lakini kuzimia uwanjani hatutaki..
 
Sioni nafasi kwa simba kushinda kwa Yanga hasa kwenye Ligi kuu. Msimu wa tatu huu Yanga anaupiga mwingi kwenye hizi game za watani.
 
UNATAKA WAMTIMUE KOCHA WAO BAADA YA KUWAFUNGA? MECHI YA HESHIMA HIIπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ€£
 
Sioni nafasi kwa simba kushinda kwa Yanga hasa kwenye Ligi kuu. Msimu wa tatu huu Yanga anaupiga mwingi kwenye hizi game za watani.

Wangeupiga mwingi wangepeleka m40 kwa wale mgambo, ili japo wajitafutie nafasi ya shirikisho, japo hawataipata kwa kunyanya kombe labda kama best loser!
 
Umeandika upuuzi , kwanini hamjiamini nyie Mbumbumbu?

Mara oooh wachezaji wataumia... wabadilishieni majukumu sasa waende kufanya kazi viwanda vya MO
 
Haya mkujrni huku mtoe mrejesho. Simba alikula ngapi nabbadae kaizer aliwapiga ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…