Ushauri kwa TANESCO Arusha; Hii siyo hujuma?

Ushauri kwa TANESCO Arusha; Hii siyo hujuma?

broken ages

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2012
Posts
235
Reaction score
84
Nimeona kitu kinachofanyika ama sijui ni tanesco ama ni jiji ila kwa namna nilivyoona ni uharibifu
ni kweli inawezekana kwamba miti hii inazuia ama inaleta madhara kwenye nyaya na njia za umeme na hivyo inapaswa kukatwa ili kupisha nyaya za umeme Hili siwezi kupingana nalo ila ambacho mimi hakijaniridhisha ni namna kazi hii inavyofanyika ndani yake kukiwepo uharibifu mkuwa mno wa mazingira na hata miundombinu ya barabara na taa za barabarani kama utakavyoona kwenye baadhi ya picha ambazo zimepigwa kwenye barabara inayotoka Impala hotel kwenda Philips ndani ya jiji la arusha

Wakataji wanakata miti hovyo na kuliacha eneo husika likiwa kama jangwa eneo ambalo lilikuwa na mandhari nzuri na ya kuvutia mno kabla ya ukataji huu usiozingatia ubora wa mazingira na hata namna ya ukataji wao ni kizamani mno miti inaanguka na kuzivunja taa zote za barabarani na wao wanaendelea na ukataji tu bila kujali (heri ingekuwa imevunjika taa moja ama mbili)

USHAURI WANGU ni bora wangeyaparua matawi yanayoelekea kwenye nyaya ama wakaipunguza urefu miti hiyo ikabaki kuwa mifupi kiasi kwamba haitofikia nyaya ili ikichanua ingependezesha bado eneo husika ama mazingira kuwa mazuri na umeme usipate madhara pia
na wakati wa kukata watumie wataalam na mashine kama misumeno ya kukatia miti(chainsaw) badala ya kutumia mashoka ambayo ni mtindo wa zamani mno na uliopitwa na wakati ili pia waweze kuimudu wapi ianguke na hivyo kuepuka uharibifu wa miundo mbinu nyingine

naomba kama mpango huo ni endelevu wazingatie ubora wa miti na mazingira ili yote yawe na nafasi yake.

25272AC8-AF17-49DE-81DA-45181D4D3602.jpeg


68EEB482-56D4-47AF-97CC-7D601349E5AD.jpeg




705B7612-86AB-4730-B693-FD714064DB8E.jpeg
 
Du Hawana Kujari Kama Wapo busy ukiwaona Huwezi amani kama ndio hao wenye Umeme wa kata kata
 
Tanesco Arusha wamekuwa wajinga kwenye Hilo swala kukata miti ovyo wanashindwa kutoa elimu kwa watu ambao wapo karibu na hyo kwa kuipunguza au hata wenyewe wanashindwa kuipunguza.

Nashangaa watu wa mazingira wanakaa kimya kuhusu Hilo alafu baada ya miaka 5 tuanze kulazimishana kila Kaya ioteshe miti 3.

Uongozi wa wilaya na mkoa kote jiji&wilaya mpaka tanesco wajitathmini kuhusu hili la ukataji miti kijinga
 
Vibarua hao, hapo utakuwa foreman aliyekabidhiwa yuko kwake anakunywa bia, kisha jioni anapiga tu simu kwa mmoja wa hao vibarua kuuliza kazi imekwendaje.
 
Back
Top Bottom