isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,143
- 6,560
Habari 👋
Siku ya leo nimeona vyema nizikumbushe mamlaka za soka nchini Tanzania katika masuala kadhaa, nitumaini langu baada ya ushauri huu utekelezaji utaanza na msimu mpya 2021/2022 tutashuhudia makubwa na yaliyokuwa bora. Nimekuwa mfuatiliaji wa masuala mbalimbali lakini mpira wa miguu umekuwa kama sehemu ya maisha yangu. Nikiri wazi nazitambua jitihada na maboresho yanayofanywa na TFF, Bodi ya Ligi na Ligi Kuu japo naona kuna nguvu ya ziada inahitajika kuboresha mchezo wa soka na ligi zake.
1. Kutengeneza na kusimimia chapa ya Ligi Kuu
TFF, Bodi ya Ligi na ushirika wa Wizara ya Michezo zihakikishe zinatengeneza chapa ya Ligi Kuu, kuiendesha na kuisimimia kuleta tija katika kuinua mchezo husika ndani ya taifa, kuingiza mapato, kutangaza taifa na kutoa burudani. Ligi Kuu ni vyema isimame yenyewe huku ikiwa na wadhamini katika mlengo wake. Ligi Kuu kama chapa itambulishwe, itambulike na ifahamike kwa wepesi kwa kila rika, jamii na hali tofauti.
Kupitia chapa ya Ligi Kuu kama taasisi zitengenezwe taasisi ndogo chini yake ambazo zitakuwa katika mlengo wa soka kama ifuatavyo:-
Ligi Kuu na Bodi ya Ligi zitatakiwa kuandaa mfumo utakaosimamia vilabu viwapo uwanjani na nje ya uwanja kimuenekano na katika chapa husika. Chapa za vilabu, wadhamini na ligi kuu kama ifuatavyo:-
Hii ni font ya GONTSERRAT ambayo inaweza kusomeka na kuonekana katika jezi kwa uzuri.
Muonekano wa majina katika jezi.
3. Ligi Kuu na vilabu kidijitali na mawasiliano yake
5. Ligu Kuu na taratibu za afya na usalama wa wachezaji na mashabiki
6. Chombo huru ndani ya Ligi Kuu kitakacho husika na urushaji wa matangazo kwa washirika
Sergio
Siku ya leo nimeona vyema nizikumbushe mamlaka za soka nchini Tanzania katika masuala kadhaa, nitumaini langu baada ya ushauri huu utekelezaji utaanza na msimu mpya 2021/2022 tutashuhudia makubwa na yaliyokuwa bora. Nimekuwa mfuatiliaji wa masuala mbalimbali lakini mpira wa miguu umekuwa kama sehemu ya maisha yangu. Nikiri wazi nazitambua jitihada na maboresho yanayofanywa na TFF, Bodi ya Ligi na Ligi Kuu japo naona kuna nguvu ya ziada inahitajika kuboresha mchezo wa soka na ligi zake.
1. Kutengeneza na kusimimia chapa ya Ligi Kuu
TFF, Bodi ya Ligi na ushirika wa Wizara ya Michezo zihakikishe zinatengeneza chapa ya Ligi Kuu, kuiendesha na kuisimimia kuleta tija katika kuinua mchezo husika ndani ya taifa, kuingiza mapato, kutangaza taifa na kutoa burudani. Ligi Kuu ni vyema isimame yenyewe huku ikiwa na wadhamini katika mlengo wake. Ligi Kuu kama chapa itambulishwe, itambulike na ifahamike kwa wepesi kwa kila rika, jamii na hali tofauti.
Kupitia chapa ya Ligi Kuu kama taasisi zitengenezwe taasisi ndogo chini yake ambazo zitakuwa katika mlengo wa soka kama ifuatavyo:-
i/. Uwepo wa ligi kuu itakayosimama kawaida katika mpira wa miguu unaohusisha timu za wanaume (Ligi Kuu).
ii/. Uwepo wa ligi kuu ya wanawake ambayo itapewa nguvu, kusimamiwa na kuendeshwa katika mfumo sawa na unaondesha ligi ya wanaume hii itambulike (Ligi Kuu ya Wanawake au Ligi Kuu Women).
iii/. Uwepo wa ligi kuu ya vijana chini ya miaka 23 itakayofahamika kama (Ligi Kuu ya Vijana au Ligi Kuu U23).
iii/. Kuanzisha ligi kuu ya vijana chini miaka 18 itakayofahamika kama (Ligi Kuu ya Vijana au Ligi Kuu U18).
iv/. Uanzishwaji wa ligi kuu ya watoto chini ya miaka 13 itakayofahamika kama (Ligi Kuu ya Watoto au Ligi Kuu U13).
v/. Uanzishwaji wa ligi kuu ya mpira wa ndani au Fútsal ambayo itapewa nguvu kuwezesha kuinua, kuonesha na kutengeneza ajira na mapato kwa vijana, taaisi na taifa.
vi/. Kuanzisha ligi kuu ya mpira wa fukwe maarufu kama Beach Soccer, ligi hii ipewe nguvu na isimamiwe vilivyo kuwezesha kuleta tija kwa vijana na taifa.
vii/. Uanzishwaji wa ligi kuu ya michezo kimtandao eSport au eGames, ligi kuu hii itahusisha mfumo wa ligi tajwa hapa juu utofauti wake yenyewe ni michezo ya kimtandao au games ambayo itahusisha zaidi wapenzi na wafuatiliaji mchezo wa soka.
Mfano wa haya ni kama picha ambatanishwa zinazoonesha ligi kuu ya soka nchini Chile.
Ligi Kuu
Ligi Kuu ya Wnawake
Ligi Daraja la Kwanza
Ligi Daraja la Pili
Ligi ya Vijana
Kombe la Ligi
Kombe la Shirikisho
Ligu Kuu ya Mpira wa ndani | Futsal
Ligi Kuu ya Michezo | eFootbal/ eGames
2. Kupitia na kuweka taratibu mpya za muenekano wa vilabu ndani na nje ya uwanjaLigi Kuu na Bodi ya Ligi zitatakiwa kuandaa mfumo utakaosimamia vilabu viwapo uwanjani na nje ya uwanja kimuenekano na katika chapa husika. Chapa za vilabu, wadhamini na ligi kuu kama ifuatavyo:-
i/. Timu zote shiriki zitatakiwa kutumia mwandiko 'font' rasmi katika jezi zao utakaotumika kuwatambulisha wachezaji na namba zao mgongoni, benchi la ufundi na wahusika wa timu ziwapo uwanjani au katika sare za timu. Katika hatua ya awali naambatanisha mfano na mwandiko pendekezwa.
Hii ni font ya GONTSERRAT ambayo inaweza kusomeka na kuonekana katika jezi kwa uzuri.
Muonekano wa majina katika jezi.
ii/. Jezi za vilabu zitatakiwa kuambatanisha nembo au matangazo ya wadhamini kama ifuatavyo:- Mdhamini mkuu atatakiwa kuchukua nafasi eneo la kifuani, mdhamini mkuu wa pili atatakiwa kuchukua nafasi mkono wa kushoto, nembo ya Ligi Kuu itatakiwa kuwa mkono wa kulia na nafasi ya chini ya mgongo itumike tuu kuweka tangazo linalohusisha jamii au kuigusa jamii (Inaweza kuwa taasisi, shirika au kauli mbiu) mfano, JamiiForums Foundation au Vijana na Ajira, Zuia Rushwa, Tokomeza Uviko na Ajali Basi. Sehemu ya ziwa la kulia ni nembo ya mtayarishaji jezi na sehemu ya kushoto ni nembo ya timu husika basi.
iii/. Vilabu vyote shiriki vyatakiwa kuwa na bao za matangazo na mahojiano kwa kila timu na iv/. Kila timu ni lazima ifanye mahojiano kabla na baada ya mchezo (Pre Match Conference na After Match Conference) na mahojiano na waandishi wa habari kabla na baada ya mchezo. Bao hizo ni mfano wa picha ambatanishwa hapa
3. Ligi Kuu na vilabu kidijitali na mawasiliano yake
i/. Ligi Kuu ihakikishe inaanda mawasiliano yake kama Ligi Kuu katika mitandao ya Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Spotify na LinkedIn mitandao hii isimamiwe ipasavyo siku hadi siku kuwezesha kufikisha taarifa na maendeleo ya mchezo wa soka na ligi yenyewe.
ii/. Iwe ni lazima kwa vilabu kuwa na majukwa katika mitandao hasa Facebook, Twitter na Instagram kupita mitandao hiyo itatakiwa vilabu vyote viwe hai 'active' na kuendesha akaunti hizo katika misingi ya soka, nidhamu na uungwana.
iii/. Ligi Kuu inatakiwa kuwa na tovuti rasmi ambayo itakuwa sehemu rasmi ya taarifa, ratiba, sheria, muongozo na masuala yote yanayohusisha ligi kuu. mfano Campeonatos Chilenos 2021 au Premier League Football News, Fixtures, Scores & Results
iv/. Vilabu vyote ni lazima kuwa na tovuti rasmi katika shughuli zake za utendaji wa kila siku.
4. Ligi Kuu, washirika na wadhaminiTFF, Bodi ya Ligi na Ligi Kuu ihakikishe kuna wadhamini wafuatao ndani yao:- i/. Mshirika mkuu wa ligi kuu (Lead Partner/s) ii/. Mshirika mkuu katika utoaji vifaa kwa ajili ya ligi kuu mpira na jezi maalumu za waamuzi (Official Ball Partener) iii/. Mshirika mkuu katika masuala ya kifedha (Official Bank) iv/. Mshirika mkuu katika masuala ya vinywaji (Official Drink Partner) v/. mshirika muu katika masuala ya muda amabaye atatoa bao za muda na vifaa vya muda kwa waamuzi (Official Timekeeper) vi/. Mshirika mkuu katika masuala ya usafirishaji (Official Travel Partener).
5. Ligu Kuu na taratibu za afya na usalama wa wachezaji na mashabiki
Ligi Kuu ihakikishe inasamimia na kupigania afya za washiriki katika mchezo na mashabiki ikiwa kwa kufuata taratibu za kujikinga na kupambana na UVIKO, maradhi ya moyo, magonjwa ya upumuaji, maradhi ya ngozi na usalama wa jumla kwa kufuata yafuatayo:-
i/. Ligi Kuu itatakiwa kuwa na madaktari rasmi kama taasisi katika kila mchezo ambao watasaidia katika dharura na msaada wa nyongeza, hii iambatane na ulazima wa vilabu kuwa na madaktari idhinishwa na vyama na taasisi zinazosimamia madaktari na kila timu na gari la kubebea wagonjwa.
ii/. Timu zote zitatakiwa kuchukua tahadhari kabla, wakati na baada ya mchezo dhidi ya magonjwa tajwa hapo juu.
iii/. Vilabu vyote vitatakiwa kuwa na hati za afya ya jumla kutoka kwa Hospitali za kitaifa/mikoa na kuidhinishwa jopo la madaktari wa ligi kuu.
iv/. Mashabiki watatakiwa kuchukua tahadhari wawapo viwanjani kwa kuacha nafasi ya kiti au mtu mmoja baina yao kujikinga na kupambana na UVIKO.
v/. Ligi Kuu inatakiwa kuajiri walinzi binafsi maarufu 'stewards' ambao watakuwa chini yao katika kulinda usalama wa wachezaji, timu, viongozi na mashabiki, ligi kuu chini ya TFF itatakiwa kuomba msaada wa askari polisi wachache sana kuwepo uwanjani kwa hali za dharura. Hii ni kuondoa mkanganyiko wa mpira na siasa na hali zisizo za kiungwana kama zilivyoshuhudiwa katika vipindi tofauti waandishi na mashabiki wakipigwa na askari.
6. Chombo huru ndani ya Ligi Kuu kitakacho husika na urushaji wa matangazo kwa washirika
Ligi Kuu inatakiwa kuanzisha chombo chini yake kitachokuwa na majukumu ya:-
i/. Uandaaji, uchakataji na urushaji matangazo ya mchezo wa soka.
II/. Ujenzi wa makao makuu hayo.
iii/. Ununuaji wa vifaa husika.
iv/. kuajiri watendaji husika.
v/. Kuzalisha na kusimamia shughuli za kila siku.
7. Ligi Kuu, waamuzi na usaidizi wa video (Video Assistant RefereeLigi Kuu ihakikishe inapitisha sheria na kuanza kutumika kwa usaidizi wa video (Video Assistant Referee) ikiwa ni pamoja na:-
i/. Kuagiza au kushirikisha chombo cha Ligi Kuu Productions kufanikisha hilo.
ii/. Kutoa mafunzo kwa waamuzi au wataalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano kufanikisha hilo.
iii/. Kutafiti mbinu wezeshi zitakazo wezesha uwepo wa mfumo wa maamuzi ya video.
Haya ni machache natumai kupitia hapa wadau mbalimbali watatoa maoni mengi zaidi kuhakikisha tunakuza soka na ligi ya Tanzania.Sergio