Ushauri kwa TFF, bodi ya ligi na ligi kuu Tanzania


"...TFF wanafaa waiache ligi kuu iwe ni project inayojitegemea waipe nafasi ya kuwa Kama kampuni ama taasisi binafsi ..yenye kujitosheleza..ikiwezekana iwe na wataalamu na wajuzi wa mambo ya marketing katika football Ili lengo litimie."

Hakika!
 
Shukrani Castr kwa hint! Kubwa, naona mfungo na structure zibadilike sasa kuwezesha mageuzi.

Ni kweli Ligi ya Wanawake ipo lakini haieleweki ni Ligi au bonanza. Katika hili ni lazima kwa vilabu kuwa na timu za wanawake, vijana na watoto.
Ligi kuu ya wanawake ni copy and paste ya ligi kuu wanaume..kwa sababu timu mbili zenye nguvu ndizo zinatawala pia huko..angalau timu za jeshi zinajitutumia..lakn nazo sioni zikiwa na muda mrefu wa kutamba..maana kwa nzia msimu huu ushindani uko kwa Simba Queens na Yanga Princes ..msimu ujao na mingine Hali itabaki hivi hivi..kwa sababu hizo timu zingine hazina uwezo wa kuhudumia wachezaji kwa msimu mzima..jiulize timu haina hata mdhamini..wachezaji hawalipwi mshahara..wengi wanacheza walitarajia kusajiliwa na Simba Queens ama Yanga Princes ndio angalau walipwe..kwa namna hio ushindani huku nako utakuwa ni zero plus zero...mdhamini aliyepo anatoa milioni 5-19 kwa msimu kwa kila hii pesa uitumie kutunza wachezaji (camp cost) safari za timu kucheza mechi, ulipe mishahara kwa wachezaji na makocha plus gharama zingine kwa timu ..BADO mwenye timu hajajigawi na yeye gawio lake hapo..so unajikuta pesa yote hii hazitoshi hata ..
 
Pesa za kufunga hizo screen waziokote wapi!!? Ligi yetu inavalue ya hivyo..wafunge LCD screen za matangazo hayo kwenye miundombinu ipi!? Je gharama za kurun hizo screen zitakuwa kwa TFF ama timu za ligi kuu ama wamailiki wa viwanjan!?

Kuna mahali nimeeleza TFF, Bodi ya Ligi, Ligi Kuu na wizara ya michezo zitafute udhamini na ushirika. Sio lazima pesa yote itolewe na TFF hapana! Ikiwa kupitia ushirika kuna namna ya kupata udhamini katika haya.

Mfano, taasisi tajwa hapo zinaweza kuomba ushirika kutoka kampuni na taasisi kadhaa kufanikisha haya. Tunaweza kupeleka proposal Sony, Xiaomi, Huawei au Samsung kuwekeza katika skrini hizo na LCD kwa makubaliano kadhaa ikiwamo kuonekana kama moja ya wadhamini.
 
Bro..kipaji bila matunzo ni sawa na kupalilia Shamba lisilopandwa mbegu..kutaota magugu tu...watoto wengi Wanavipaji..matunzo hakuna...Kuna academy chungu laki huko mitaani..zipo kwa kuwa zipo..na haizja namna lakini hazifuati misingi ya kukuza mchezaji..leo hii halaand mchezaji wa Borusian Dortmund ana miaka 20 analimwili Jumba Kama vile..sisi huku mchezaji wa age hio anakamwili kalikodumaa kwa utapiamlo kea kukosa mlo sahihi...matokeo yAke..anavuka miaka ya kuwa kwenye academy lakini bado yupo hapo hapo anatafuta nafasi..akija kuipata nafasi anabadiliaha cheti za kuzaliwa kutoka miaka yake halsii anaipunguza ..Kama alikuwa na 24 ana ipinguza mpaka 17 ..matokeo yAke tunakuwa na wachezaji vikongwe kwenye timu zetu..ambao wanashindwa kutupa matokeo chanya hata pale inapoonekana kuwa tunastahili kuyapata.
 
Uko sahihi, but kwa mvuto Gani ulipo kwenye ligi yetu mpaka hizo kampuni zikaja kuwekeza kwenye hayo Mambo!?..ukiacha mechi ya Simba na yanga, Simba vs Azam a, Yanga vs Azam ni mechi Gani zingine zinamvuto kwa watu na tentions kwa media!? Tena hapo itoe Azam ..ibaki Simba vs Yanga ama Yanga vs Simba..we have the only one match yenye mvuto..sasa kweli mtu she kupoteza karibu milioni 500-bilioni 10 kwa mechi Moja tu..tena ambayo imejaa ukiritimbana kuanzia dk 1-90!? Ngumu
 

Ikiwa kufanikisha haya ni hadi tufikie kiwango fulani sioni tukipiga hatua. Ni kheri kuanza sasa.
 
Ikiwa kufanikisha haya ni hadi tufikie kiwango fulani sioni tukipiga hatua. Ni kheri kuanza sasa.
Sure..unahisi tuanze ..japo itachukua muda mrefu lkn sio mbaya...Ila shida watu tulionao kwneye mifumo ya Uongozi wa soka ..wanajiwaza wao na kesho yao tu..hawawezi kesho ya wajukuu zao...na hiki lipo lila mahali kwenye nchi hii..mtu anafanya Kazi kwa kujiangalie yeye na familia yake ..hawezi kuhusu wajukuu zake...ifike mahali..tufanye Kazi kwa kujiangalia , na kuwaangalia wajao ndio mafanikio yatapatikana ..
 
Hili suala la ustawi kwa pamoja ni muhimu sana kwa kila hali na mahali katika taifa.
 
TFF na Ligi Kuu ihakikishe mgawanyo sawa wa mechi zitakazo oneshwa kwa vilabu vyote shiriki. Watakaochukua haki za matangazo wahakikishe wanajizatiti kwa kuongeza channeli zao kuwezesha kutoa fursa za uchaguzi wa mechi ya kuangalia mubashara.
 
Mkuu isajorsergio mwanzo sikuuona huu uzi. Nadhani ni moja ya nyuzi bora kabisa za football hapa JF. Mawazo yako ni mazuri sana na mengi kama sio yote yanatekelezeka ni kuwa na uthubutu tu.

Ningeendelea kuandika ila kwasasa nipo busy kidogo nitarudi tuendelee kujadili.
 
Nasikia Azam FC chini ya Azam - Bakhresa inafunga LED Lights, LCD Screens (Ads Boards) na kuongeza majukwaa katika kiwanja cha Azam Complex.
 
Hapo kwenye namba 5 ndipo ulipochemka! Ukiendekeza hilo mashabiki hawataruhusiwa viwanjani kwa kisingizio cha corona. Kumbe kilichoko nyuma ya pazia ni makampuni ya TV na mitandao wakitaka kupiga pesa ndefu!!
 
Mimi sipingani na hili la uwekezaji kwa watoto, kwani ushiriki wa watoto kwenye michezo mbalimbali huenda sambamba na ukuaji kwa maana ya rika na elimu iwe ya awali, msingi na kadhalika. Nilichokuwa nakilenga ni kudhani kuwa ukosefu wa miundombinu ya kisasa , ukosefu wa rasilimali fedha za kumaliza changamoto zote zinazotukabili na hivyo kutoa mianya kwa wajanja wenye fedha kidogo wenye malengo yao ya siri kuingiza fedha zao kwa mashindano ya muda mfupi ili kupata platform ya kupanda ngazi kisiasa , rejea Mashindano ya Diwani cups huwa yanafanyika kila uchaguzi mkuu ukikaribia then yanatoweka, vipindi vya michezo mashuleni ni kama havina tija tena, vimekuwa ni sehemu ya Waalimu na Wanafunzi kupata muda wa kufanya mambo yasiyokuwa na uhusiano na michezo ama wanafunzi kuvumbua aina mpya ya michezo isiyo rasmi kama vile kukimbizana juu ya madawati. Viwanja vya michezo Mashuleni vimekufa kwa kujengwa madarasa mapya. Mtoto nae amekuwa brainwashed kuwa bila ya kuvaa vifaa maalum vya mchezo husika, ufanisi hauwezi kupatikana hivyo kufifisha hata ile juhudi kidogo ya kujiendeleza. Fedha kidogo inayopatikana kwa ajili ya michezo, tayari wajanja wanakuwa tayari wameishaipigia mahesabu ya kuipiga.
 
Timu za majeshi au mashirika kutofanya vzr ni changamoto kubwa ya kukosa uongozi sahihi kusimamia timu husika

Huwa inanifikirisha kiasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…