Ushauri kwa TFF: Mnapopanga ratiba za saa nane mchana, hakikisheni Kila timu inaguswa na hiyo ratiba

Ushauri kwa TFF: Mnapopanga ratiba za saa nane mchana, hakikisheni Kila timu inaguswa na hiyo ratiba

Ushauri huu ufike moja kwa moja katika shirikisho la mpira Tanzania (TFF), nilikua naangalia ratiba za wenzetu waliotuzidi kimaendeleo ya mpira wa miguu, nikili tu kiukweli ratiba zao hazina upendeleo haswa kwenye suala muda.

Iwe man u, iwe na Manchester city ratiba ya muda Kama ni mchana basi ratiba itakugusa haijalishi wewe ni mkubwa kiasi gani na hiyo ndiyo mantiki ya shirikisho la mpira kutoingiliwa katika upangaji wake wa ratiba labda itokee dharura.

Sikumbuki ni lini timu zetu kongwe(Simba na Yanga) zilicheza saa nane mchana sikumbuki kabisa na Kama walicheza basi ni muda mrefu sana.

Ukizitoa Simba na Yanga kutocheza saa nane mchana jua Kali likiwaka timu zilizobaki zote huwa zinaguswa na hiyo ratiba ya saa nane mchana, sijui ni kipi huwa kinatazamwa.??

Nikisema ni upendeleo nitakua nimekosea?? Je hao wanaochezeshwa mchana wakati wengine ratiba hiyo haiwagusi, je wanajisikiaje???

Najua Simba na yanga siku wakichezeshwa saa nane jua Kali Kuna wachambuzi, wanasayansi mpaka wataalamu wa jua wataibuka kuzitetea timu zao pendwa Ila kwa Sasa wapo kimya tu.

My take, TFF guseni ratiba ya mchana kwenye timu zote siyo ihefu, ruvu nk


Imeandikwa na NALIA NGWENA
Niliandika humu kuhusu jambo hili nikaishia kutukanwa
 
Mechi ya Simba na Yanga ina mengi nyuma, Moja ni Biashara. Hizi mechi huwa zinapangwa kuhakikisha Mapato yanakusanywa kwa wingi sana,mfano kutanua wigo wa wahudhuriaji.
Anajifanya hajui..

Yeye anatoa ushauri tu, nikajua anatoa na fungu la kudhamini pengo la mapato
 
Back
Top Bottom