Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Kutokana na kutokuwepo kwa mashindano yoyote ambayo ingetumika kujiweka sawa na kuchagua mfumo na mbinu mbali mbali kutokana na wachezaji wapya waliosajiliwa ni vyema kwa timu za Biashara, Simba, Azam na Yanga kutafuta timu walau zisizo pungua nne hivi za kucheza nazo ili kujiweka sawa kimashindano.
Msimu uliopita timu nyingi zilishindwa kuonesha viwango vyao kutokana na kutocheza mashindano kwa muda mrefu kutokana na tatizo la ugonjwa wa covid 19 hivyo kuwafanya wachezaji kukosa fitness.
Tusipoangalia hali hiyo inaweza ikatukuta katika timu zetu hivyo kwenye pre season zinazofanywa na klabu zetu zisiishie tu kwenye kufanya mazoezi, bali tafuteni timu za kucheza nazo kabla hamjaingia kwenye mchezo ya klabu bingwa na shirikisho CAF.
Aidha kwa upande wa mshindani wa Yanga timu ya Rivers Utd wametoka kumaliza mashindano ya ligi yao juzi tu tarehe 5 mwezi huu na pia Al Hilal ambayo anaweza kukutana nayo endapo atawatoa Rivers, tarehe 12 ya juzi wametoka kucheza mechi na bado wanamechi zingine mbele.
Azam pia game inayofuata kama ikiwatoa Horseed atakutana na pyramids ambayo mpaka sasa wanaendelea na ligi hivyo hivyo kwa Biashara endapo itapita hii hatua ya awali, hatua inayofuata itakutana na timu ambazo bado hazijamaliza ligi zao.
Ni Simba pekee ndio atakayekutana na timu zilizotamatisha ligi zao zaidi ya miezi mitatu. Hivyo timu zote zijitahidi kutafuta timu kadhaa za kucheza nazo mechi za kirafiki ili kujiweka sawa.
Kila la kheri