Ushauri kwa timu zinazowakilisha nchi kimataifa

Ushauri kwa timu zinazowakilisha nchi kimataifa

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Kutokana na kutokuwepo kwa mashindano yoyote ambayo ingetumika kujiweka sawa na kuchagua mfumo na mbinu mbali mbali kutokana na wachezaji wapya waliosajiliwa ni vyema kwa timu za Biashara, Simba, Azam na Yanga kutafuta timu walau zisizo pungua nne hivi za kucheza nazo ili kujiweka sawa kimashindano.

Msimu uliopita timu nyingi zilishindwa kuonesha viwango vyao kutokana na kutocheza mashindano kwa muda mrefu kutokana na tatizo la ugonjwa wa covid 19 hivyo kuwafanya wachezaji kukosa fitness.

Tusipoangalia hali hiyo inaweza ikatukuta katika timu zetu hivyo kwenye pre season zinazofanywa na klabu zetu zisiishie tu kwenye kufanya mazoezi, bali tafuteni timu za kucheza nazo kabla hamjaingia kwenye mchezo ya klabu bingwa na shirikisho CAF.

Aidha kwa upande wa mshindani wa Yanga timu ya Rivers Utd wametoka kumaliza mashindano ya ligi yao juzi tu tarehe 5 mwezi huu na pia Al Hilal ambayo anaweza kukutana nayo endapo atawatoa Rivers, tarehe 12 ya juzi wametoka kucheza mechi na bado wanamechi zingine mbele.

Azam pia game inayofuata kama ikiwatoa Horseed atakutana na pyramids ambayo mpaka sasa wanaendelea na ligi hivyo hivyo kwa Biashara endapo itapita hii hatua ya awali, hatua inayofuata itakutana na timu ambazo bado hazijamaliza ligi zao.

Ni Simba pekee ndio atakayekutana na timu zilizotamatisha ligi zao zaidi ya miezi mitatu. Hivyo timu zote zijitahidi kutafuta timu kadhaa za kucheza nazo mechi za kirafiki ili kujiweka sawa.

Kila la kheri
 
Point muhimu sana hii ya mleta mada.

kuna timu nawasiwasi nayo kutolewa cafcl kabla ligi ya ndani haijaanza na wakitolewa ngumi zitasimama klabuni kwao.
 
Ndo tushaanza mechi za kirafiki tumepigwa 9-0
 
Huu ushauri hauihusu Simba, maana itaanza kucheza mechi ya CAF raundi ya kwanza October.

Itakuwa ishaanza kucheza mechi za Pre season, Simba day, Ngao ya jamii na zile mechi za awali za ligi kuu.
 
Huu ushauri hauihusu Simba, maana itaanza kucheza mechi ya CAF raundi ya kwanza October.

Itakuwa ishaanza kucheza mechi ya Simba day, Ngao ya jamii na zile mechi za awali za ligi kuu.
Mechi za .. day (Bonanza) kila mchezaji anakuwa katika mood flani hivi yaani hakuna mchezaji anaye floop na ndio maana hata Sarpong alionekana bonge la straika anafunga hata kama kafungwa kitambaa machoni.

Lakini baada ya bonanza kila mchezaji anarudi kwenye uhalisia. Hivyo usihesabie hilo bonanza katika kuchambua mapungufu ya mfumo, mbinu au wachezaji waliopo.

Hivyo hapo Simba atakuwa kacheza mechi mbili tu inayoweza kufanyika analysisi, mechi ya kwanza ni ya ngao ya jamii na ya pili mechi ni ya mzunguko wa kwanza ligi kuu bara. Je hizo mechi mbili zitatosha kufanya analysis ya timu?
 
Mechi za .. day (Bonanza) kila mchezaji anakuwa katika mood flani hivi yaani hakuna mchezaji anaye floop na ndio maana hata Sarpong alionekana bonge la straika anafunga hata kama kafungwa kitambaa machoni. Lakini baada ya bonanza kila mchezaji anarudi kwenye uhalisia. Hivyo usihesabie hilo bonanza katika kuchambua mapungufu ya mfumo, mbinu au wachezaji waliopo. Hivyo hapo Simba atakuwa kacheza mechi mbili tu inayoweza kufanyika analysisi, mechi ya kwanza ni ya ngao ya jamii na ya pili mechi ni ya mzunguko wa kwanza ligi kuu bara. Je hizo mechi mbili zitatosha kufanya analysis ya timu?
Wakiwa Pre season, Simba itacheza mechi 4 na timu za pale Moroco. Hivyo huo ushauri wako waambie Uto.
 
Wakiwa Pre season, Simba itacheza mechi 4 na timu za pale Moroco. Hivyo huo ushauri wako waambie Uto.
Mkuu unaonesha ni namna gani ulivyo na mahaba bila hoja. Mara ya kwanza ulisema kuwa Simba hawahitaji mechi za pre season kwavile mechi yao ya klabu bingwa ni October ambapo watakuwa wamecheza ligi kuu, simba day na ngao ya jamii hivyo mechi za pre season Simba haiwahusu. Sasa hivi umekuja kujipinga tena kuwa Simba itacheza mechi nne za pre season hivyo ushauri apewe utopolo. Mimi nimetoa ushauri wangu kwavile sijui program za timu yeyote ile kati ya timu nne zinazowakilisha nchi kama wamepanga kucheza mechi kadhaa za pre season. Wewe unakazania tu waambie uto waambie uto utafikiri unajua taarifa za hao uto na za Simba .

Kwavile wewe unajua program za Simba kuwa itacheza pre season mechi nne naomba unifahamishe anacheza tarehe zipi na zipi na dhidi ya timu zipi.
 
Akikujibu unitag hao ndo mashabiki holela.
 
Huu ushauri hauihusu Simba, maana itaanza kucheza mechi ya CAF raundi ya kwanza October.

Itakuwa ishaanza kucheza mechi ya Simba day, Ngao ya jamii na zile mechi za awali za ligi kuu.
Wakiwa Pre season, Simba itacheza mechi 4 na timu za pale Moroco. Hivyo huo ushauri wako waambie Uto.
Asa mbona haueleweki unasimamia upande upi? Mara unakataa mechi za preseason kuwa haziwahusu Simba halafu tena unakubali kuwa simba itacheza preseason mechi nne. Una wenge bila shaka
 
Mpaka sasa ni Yanga pekee ndio wameonesha hawana muda wa kuwekeza kwenye maandalizi ya kikosi (kucheza mechi ya majaribio) Biashara, Azam na Simba wote wapo bize kwenye maandalizi na wameshacheza mechi za kirafiki ili kujiweka sawa na bado wanaendelea na ratiba za kutafuta mechi za kujiweka sawa.
 
Azam kacheza mechi tatu mpaka sasa za kimataifa za kirafiki. Jana kacheza na Zesco ya Zambia na Azam kuondoka na ushindi wa goal moja. Azam mechi tatu za kimataifa kushinda 2 kafungwa mechi 1. Simba mechi 2 za kimataifa. Yanga mechi moja ya kimataifa. Biashara ajacheza mechi ya kimataifa hata moja.
 
Point muhimu sana hii ya mleta mada.

kuna timu nawasiwasi nayo kutolewa cafcl kabla ligi ya ndani haijaanza na wakitolewa ngumi zitasimama klabuni kwao.
Kumbukumbu ya maoni ya mwana JF. Haya ndio madhara ya kuthamini wiki ya mwananchi kuliko klabu bingwa Africa. Hongereni sana Biashara United, kila la kheri Azam leo hii na Simba hapo kesho
 
Back
Top Bottom