Uchaguzi 2020 Ushauri kwa Tume ya Uchaguzi

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Kufuatana na Ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 25 Agosti, 2020 ni siku ya UTEUZI. Ushauri wangu ni wa bure kwenu.

Hakikisheni Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Majimbo Tarehe 25 Agosti, 2020 wanakaa kwenye vituo vyao bila kukosa na isije ikajirudia mapungufu yaliyotokea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 2020. ambapo ofisi nyingi za watendaji zilifungwa.

Pili, HAKI itendeke na kusiwe na upendeleo wa Vyama. Tatu, siku ya UTEUZI Watendaji wa Tume muwe ofisini, ufuatiliaji uwepo pale penye matatizo ya hapa na pale na matatizo kama yapo maelekezo yatolewe na Tume haraka iwezekanavyo na jibu lipatikane.

Mwisho, sisi kama Wananchi tunataka Uchaguzi ulio HURU na HAKI bila kumuonea mgombea yeyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…