6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Habari yako mhe. Tundu Lisu?
Nina imani huko ulipo umzima wa afya wewe na familia yako, hivyo wengi ndio furaha yetu sisi tunaopenda kuona kila binadam yuko salama, mzima na mwenye afya njema.
Leo nimeamua kukuandikia wewe mwenyewe direct humu kwa lengo la kukufungua macho na akili yako itafakari kwa kina kuhusu yale yanayokutokea katika maisha yako hasa katika kipindi ambacho uchaguzi wa chama chako unapokaribia na kuweka mvutano mkubwa kati yako na boss wako.
Kikawaida hali kama hiyo haukuwahi kukutokea huko nyuma kabla ya 2017, kwa sababu haukuwa na mawazo yoyote ya kuja kukiongoza chama chako. Ila kuna watu ambao wao walikuwa na shauku ya kukiongoza chama hicho na matokeo yake mwenyewe unayajua. Chacha Wangwe aliekuwa mstari wa mbele kutaka mabadiliko ya uongozi ndani ya chama, yalimkuta ya kumkuta na matokeo yake akapoteza maisha katika mazingira ambayo hata wewe mwenyewe unayajua.
Baadae kidogo akajitokeza Zito Kabwe akiwa ametanguliza tunguli zake mbele kwa lengo la kumlinda na chochote kitachomtokea endapo atashtukiwa mapema kuwa anataka kuleta mageuzi ndani ya chama. Kweli aisee, baada ya Zito kushtukiwa kuwa anataka kuleta mageuzi ya uongozi ndani ya chama akakumbana na hali ambayo wewe mwenyewe unaifahamu, ulikwepo na uliiona. Zito akawa kaponea chupuchupu (hapa sijui kama ni Mungu au tunguli) zilimsaidia kukwepa kuingia kwenye 18 ya boss wenu.
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2015, kuisha na chama chako kuangukia pua. Kila mtu akaweka macho na masikio kwa boss wenu ili kuona kama atajiuzulu kwa kitendo chake cha kumleta Lowasa ndani ya chama agombee uraisi, na wakati kulikuwa na hazina kubwa ya viongozi wenye maono na ushawishi mkubwa ndani ya chama na nchi kwa ujumla kama vile wewe, Dr Slaa nk. Baada ya boss kugoma kujiuzulu ukuu wa chama, wengi wakawekeza akili na mawazo yao kwako ili uchaguzi mkuu wa chama utapofika waweze kumuadhibu boss huyo kupitia sanduku la kura na kukuweka wewe kama kiongozi mpya wa chama.
Baada ya miluzi mingi na kelele za watu kuonesha kuwa unaweza kugombea na kushinda ukuu wa chama, mambo yakabadilika ghafla ukaanza kuona watu wanakufuatilia fuatilia kimya kimya, kila unapokwenda. Nakumbuka uliwahi kutoa taarifa mapema kuwa kuna watu wanakufuatilia, lakini hakuna aliejali wasi wasi wako. Na matokea yake siku 1 ukaingia kwenye 18 kabla ya uchaguzi kufika. Ukashambuliwa kwa lengo la kuondoshwa duniani ila Mungu akakujaalia, haukufa. Ila dereva alipohitajika ili ahojiwe mazingira yaliosababisha wewe ushambuliwe bila yeye kupata jeraha hata la kuchubuka, boss alimchukua dereva yule na kumkimbiza pasipojulikana. Hadi leo kijana anaishi na siri kubwa moyoni mwake na hataki mtu mungine ajue zaidi ya yeye na wale waliopewa kazi hiyo.
Mwaka huu ukiwa na lengo la kum challenge tena boss wako, baada ya kugoma kuachia kiti kama alivyoahidi miaka ile, umeanza tena kuona mauza uza ambayo yanafanana na yale ya kipindi kile ulichotwangwa risasi. Ukiachana na zile shutuma za kutembeza pesa ndani ya chama ili wewe ushindwe uchaguzi, lakini pia inafanyika mbinu nyingine ya nje ya chama ambayo ndio hiyo inayofanya leo uone kuna watu wanakufatilia fuatilia kila unapokwenda. Na usipokuwa makini hao jamaa wataondoka na roho yako kweli. Maana watu wamedhamiria kuendelea kuongoza chama alaf wewe unakuja kuwanyang'anya mkate wao walioutengeneza miaka mingi iliyopita.
So ushauri wangu kwako ni aidha..
1. Uachane na mawazo ya kugombea kiti cha uongozi wa chama.
2. Uanzishe chama chako mwenyewe.
3. Uombe ulinzi binafsi hata wa watu wako wa karibu (kama hauamini wa serikali)
Because it seems like kuna kiongozi fulani wa chama chako anatumika na watu wa mfumo, kuhakikisha hakuna kiongozi wa kweli wa upinzani anachukua uongozi wa chama kwa lengo la kuing'oa CCM na serikali yake madarakani.
Huu ni mfumo uliotengenezwa toka wakati wa uanzishwaji wa vyama vingi ili kuendelea kupokea misaada na hela mbali mbali kutoka huko ukubwani. Aliyoyafanya hayati Mrema kwa kina Marando, ndio aliyoyafanya Lipumba kwa Maalim Seif na pia ndio hayo hayo anayoyafanya boss wako kwako.
Uwezekano wa wewe kuchukua kiti kwa mazingira yaliopo na mgumu sana kwa sababu mwenzako ana nguvu ya mfumo na pesa nyuma yake. Wakati wewe unabebwa na hoja, misimamo na kujitolea kwako kwa ajili ya chama.
So muda ndio huu wa kuamua moja kati ya hayo matatu hapo juu. Usije sema haukushauriwa mapema.
Pia soma:
Kuelekea 2025 - Singida: Tundu Lissu adai kufuatiliwa na Watu wasiojulikana
DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali