Ushauri KWA Tundu Lisu;-Samehe yote,Rudi nyumbani,ujumuishwe kwenye kikosi kazi cha mkandala mchango wako ni muhimu,Muda wa kukaa ughaibuni umeisha!

Ushauri KWA Tundu Lisu;-Samehe yote,Rudi nyumbani,ujumuishwe kwenye kikosi kazi cha mkandala mchango wako ni muhimu,Muda wa kukaa ughaibuni umeisha!

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,280
Reaction score
2,522
Wazalendo wote popote mlipo!nitumieni ujumbe huu kwa ndugu yetu Tundu lisu,Taifa lako linahitaji uchapakazi wako na taaluma YAKO ya sheria, sahau yote na urudi NYUMBANI ufanye kazi ya kulijenga Taifa lako Tanzania.

Team yenye Warioba ndani yake,Tundu Lisu,Mkandala na wadau wengine ni team nzuri Sana ambayo inaweza kushughulika na changamoto mbali mbali za kisheria na kikatiba na hatimaye kupata katiba Mpya!Muda umefika Sasa ni wakati wa kuwa pamoja kama Taifa na kujadili mstakabali wetu KWA pamoja!mchango wako unahitajika Rudi nyumbani haraka na umuombe Rais akujumuishe kwenye kikosi kazi cha katiba mpya cha mkandala.

Muda wa katiba mpya ni Sasa Ili tupate Tanzania Mpya tulioiota KWA miaka Mingi.

Mungu ibariki TANZANIA!
 
Waliotaka kumuua bado wapo na polisi ambao wanapaswa kufanya uchunguzi wamedhihirisha jinsi na wenyewe walivyo sehemu ya washukiwa kwa kukataa kufanya uchunguzi kwa kuleta visingizio vya kipumbavu kwamba wahanga waje wasaidie uchunguzi.

Sasa kama wahanga wote wangefariki kwenye tukio sijui hao polisi wangeacha kufanya uchunguzi kisa wahanga wote wamefariki dunia na hii inatuonyesha aina ya polisi tuliyo nayo.

Huu mkwamo wa kulichunguza hili tukio unaonyesha wazi jinsi serikali ya Magufuli ilivyohusika katika njama za kumuua Bwana Lissu.
 
Kikosi kazi chenyewe ni batili, kilisema Katiba Mpya isubiri, ili kumfurahisha Rais aliyekitengeneza, baadae Rais huyo huyo alipokutana na Kamati Kuu ya chama chake, wakakubaliana Katiba Mpya ije.

Mpaka hapo naona hicho kikosi kazi hakina kazi tena.
 
..kwanini waliomshambulia hawakamatwi?

..kuna ugumu gani kuanza na aliyeondoa walinzi wa area D siku ambayo Lissu alishambuliwa?

..kwanini rekodi za CCTV camera za eneo la tukio haziwekwi wazi ili wananchi tuwasaidie Polisi kuwatambua waliohusika?
 
Waliotaka kumuua bado wapo na polisi ambao wanapaswa kufanya uchunguzi wamedhihirisha jinsi na wenyewe walivyo sehemu ya washukiwa kwa kukataa kufanya uchunguzi kwa kuleta visingizio vya kipumbavu kwamba wahanga waje wasaidie uchunguzi.

Sasa kama wahanga wote wangefariki kwenye tukio sijui hao polisi wangeacha kufanya uchunguzi kisa wahanga wote wamefariki dunia na hii inatuonyesha aina ya polisi tuliyo nayo.

Huu mkwamo wa kulichunguza hili tukio unaonyesha wazi jinsi serikali ya Magufuli ilivyohusika katika njama za kumuua Bwana Lissu.
Hakika umenena. Huwa najiuliza swali je wangefariki ,polisi wasingefanya uchunguzi? Hili ni swali linloniumiza kichwa sana
 
Kikosi kazi ni laana hakina malengo na taifa la Tanzania kina malengo na chama dola CCM ,yaani kikwete alipoteza milioni 300 bado UVCCM wanampongeza
 
Ukimsikiliza vizuri Lissu sidhani kama atarejea hivi karibuni.maana wale waliopewa madaraka wengi ni mahasimu wake waleeee wasiojulikana waliomfunga mbowe. Wazeee wa Pijiooooo.
 
Hakuna haja ya kurudi. kumbuka alikuwa anatetea masikini wajinga na wapumbavu. Na siku zote ukitetea makundi haya na wewe utangamia. Na hata ikitokea amerud tumshauri. awa tetee matajiri kwenye biashara zao na uwekezaji. Kwa7babu raia wa 🇹🇿 %97 wanaishi kwenye makundi hayo matatu
 
Nchi ina watu wenye mawazo ya kipumbavu sana eti mtu ana comment Lissu anamuachia huyo mbelgiji vp .Hizo tuhuma za kipuuzi mnazomtuhumu Lissu ndo mambo mnayofanya nyie wenyewe.Idiot
 
Nchi ina watu wenye mawazo ya kipumbavu sana eti mtu ana comment Lissu anamuachia huyo mbelgiji vp .Hizo tuhuma za kipuuzi mnazomtuhumu Lissu ndo mambo mnayofanya nyie wenyewe.Idiot
Mwache ajipalie makaa ya moto.
Zaburi 140 itampa muhusika majibu kwani hakuna hupitacho bila majibu husika na mtu atavuna kuendana na kutenda kwake.
 
Back
Top Bottom