Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,968
- 8,139
Wakulungwa habari za siku nyingi.
Leo nimeonelea nitumie muda wangu kidogo kuandika kwa ajili ya kuwapa ushauri vijana wetu ambao ndio wamemaliza kidato cha sita, hasa wale ambao ndoto zao ni kuendelea na masomo ya chuo. Zifuatazo ni dondoo chache kutoka kwangu kaka yenu ambae nimebahatika kuwatangulia.
1.Usichague kozi kwa sababu tu ya kupata mkopo asilimia 100
Naelewa kwamba wengi wanaweza wasinielewe kwa huu ushauri, kwa sababu mbalimbali ikiwemo hali mbaya ya kiuchumi kwa familia wanazotokea. Lakini, nisikilize mimi, moja ya kosa kubwa ambalo vijana wengi huwa wanafanya katika hatua hii ni kuchagua kozi kwa kigezo cha kwamba kozi hiyo itamuwezesha kupata mkopo kwa asilimia 100, huwa mara nyingi hawafikirii mbele kuwa baada ya hapo nini kinafuata. Hivyo, unakuta kijana anakwenda kusoma kozi ambayo ya kitu ambacho hata hakipendi kutoka moyoni, hana passion nacho ni vile tu bora liende apate mkopo asilimia 100, basi. Hii mara nyingi huja kusababisha kijana kushindwa kupambana na hali halisi baada ya kumaliza masomo yake, kwani anakua hana mapenzi na alichosomea, hivyo ugumu anaokutana nao badala ya kupambana anakata tamaa mapema kwa sababu hana mapenzi na fani yake.
2.Anza ku-connect na "gurus" wa field yako , na jifunze vitu kuhusu fani yako tangu mwaka wa 1
Kitu cha kwanza kabisa ambacho inabidi ufanye mara tu baada ya kuanza masomo ya chuo kikuu ni kujisajili na mtandao wa LinkedIn. Ukishafanya hivyo, lets say wewe unasome Bachelor of Accountancy & Finance (BAF) pale Chuo Kikuu cha Mzumbe, ukishajiunga tu na kuweka details zako kwenye profile yako, anza sasa ku-connect na wataalamu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ambao wako kwenye hiyio field yako ya Accountancy & Finance. Ukisha connect nao, tafuta wawili/watatu ambao kutokana na profiles zao utaona ni maguru kabisa katika hiyo field yako (eg Finance Managers, Finance directors, Financial Analysts, Accounts Managers, Finance Specialists, etc) kwenye makampuni mbalimbali makubwa nchini kama Mabenki, NGOs, serikalini, then anza kuwatumia meseji na kuwaomba wawe mentors wako.
Waambie wewe ni mwanafunzi wa BAF Mzumbe ambae utafurahi kama akiwa mentor wako. Kati ya watatu, wanne, watano ambao utawatumia mesejim, hautakosa wawili watatu ambao wata-respond positively na kukubali ombi lako; Wakishakubali tu sasa na wewe unakua active (usiwasumbue sana lakini,maana hawa ni watu ambao wako busy sana), unawaomba ushauri wa hapa na pale kuhusu fani yako na kuwauliza maswali mawili matatu ili wazidi kukujenga na kukupa mwanga wa namna ya kusogea mbele katika taaluma na fani yako. Hawa hawa pia ndo utawatumia hadi kwenye kuomba nafasi za "field" huko mbele ya safari.
Pamoja na hayo, watakusaidia kukupa mwanga wa fani yako, hutakua kama wale anasoma hadi anamaliza miaka mitatu halafu anaanza kuuliza hivi watu waliosomea Project Management wanaweza kufanya kazi wapi?
Tumia simu yako ku-google na kutafuta taarifa mbalimbali kuhusu fani yako; mambo gani mapya yanatokea kwenye fani yako, fani yako ina soko maeneo wapi, changamoto za kwenye fani yako ni ipi, specializations tofauti tofauti za fani yako, na kadhalika na kadhalika.
3.Anza kujiongeza kwa kusoma kozi za muda mfupi zinazohusiana na field yako tangu mwaka wa 1, pamoja na kuongeza ujuzi (skills) zinazohusiana na fani yako
Hapa sasa lazima uwe mjanja mjanja kuanza kujijenga mapema na kujitofautisha na wengine ambao uta-graduate nao. Anza kusoma vikozi vya muda mfupi mfupi vya hapa na pale vinavyohusiana na kozi yako (Kwa sababu utakua umechagua kozi unayoipenda kwa kufuata ushauri namba 1-na sio kwa ajili ya kupata mkopo,ina maana hii itakua rahisi zaidi kwako);Tukiendelea na mfano wetu wa BAF, kuna vile vikoze vyenu vya watu wa finance vile, sijui certificate ya nini na nini, blah balh blah.
Unaweza ukaenda mbali zaidi hata kusoma zile certifications za kulipia kwa kadri ya muda na uwezo utakavyokuruhusu (Hapa ikibidi hata utumie boom kidogo kulipia vikozi vya aina hiyo kama itahitajika, au hata pia kuomba sapoti kwa wazazi kama wana uwezo wakulipie gharama ya hivyo vi-certificates, vitakuja kukusaidia sana).
Hili liendane sambamba na ku-gain ujuzi (skills) mbalimbali zinazoendana na hizo certificates, sio unajza vyeti tu ujuzi huna, huo nao utakua ni upimbi plus plus. Hapa pia usisahau kuendelea ku-update profile yako ya LinkedIn kuongezea hivyo vi-certificates na skills kadri unavyozi-gain.
Kwa leo ni hayo tu wadogo zangu, kwa wenye nyongeza wanakaribishwa kuongezea mawili matatu kwa ajili ya kuwapa mwanga zaidi wadogo zetu.