Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Mkipata kazi kwanza mjue mlichojifunza Chuoni ni kama 60% hivyo mnahitaji kujifunza kwa haraka majukumu mtakayo pangiwa bila dharau kwa mtakao wakuta. Degree inakusaidia kupata kazi ila haikusaidii kuendelea kubakia kazini.
Kitakachokufanya usalie kazini na kuendelea kula mema ya nchi ni kama utafanya yafuatayo;
1. Kufanya kazi kwa bidii na kukamilisha majukumu yako kwa USAHIHI na kwa wakati.
2. Kuwasiliana/Communication kama kuna kitu umeshindwa/huelewi uliza ili uelekezwe ili usiharibu au kushindwa kumaliza kwa wakati (hii ni muhimu sana).
3. Epuka kupiga Soga wakati wa kazi na utani sijui wa Yanga na simba, mitindo ya nguo/nywele nk hii hupelekea uzembe wa kuchelewesha huduma.
Kumbuka mteja/huduma unayotoa ndio imekuweka kazini. Simu/Meseji/ndugu/marafiki wanaweza kusubiri.
4. Wewe ni msomi hivyo angalia taratibu gani zipo vizuri kwenye Idara uliyopangiwa uzifuate na zile mbaya epuka; mbaya ni kama kuchelewa kazini, wizi, kutoroka, kupiga soga wakati wa kazi, majungu nk.
5. Epuka visingizio vya mara kwa mara (watu wengi wanachangamoto zao ila hawazileti makazini); hii inaweza kukupa reputation mbaya kwa muda mfupi na kupelekea kuachishwa pale kunapokuwa na haja...
Narudia tena, Degree itakusaidia kupata kazi ila haikusaidii kusalia kazini na kumbuka wapo wasomi wengi pengine kuliko wewe wapo nje wanasubiria hiyo nafasi!
Mkifeli na kufukuzwa msije anza kulia lia kuwa mmeonewa huku nimeshawapa marking scheme ya mtihani; Kazi kwenu!