MwajabuOmary
JF-Expert Member
- Jul 11, 2013
- 384
- 418
Awali ya yote napenda kusema mimi sio mwanachama wa CHADEMA lakini kama Mtaanzania na mwanadamu ninachoamini mimi ni kwamba Siasa ni sehemu ya maisha yangu.
Nimekua mfuatiliaji wa mambo mengi ya Kisiasa hapa nchini kwa muda mrefu kwa sababu naamini ni wajibu wangu.
Tangu tarehe 12/12/2024 Mh. Lisu alipo tangaza nia ya kugombe uenyekiti Taifa, kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na magazeti, kumekua na sintofahamu ya hapa na pale. Viongozi na wanachama jifunzeni kunyamaza kwani nafasi mnayo ya kupiga kura full stop.
Sina ubaya wa aina yoyote na Mbowe na wala sina uzuri wowote na Lissu. Lakini kwa muda ambao Mbowe amekitumikia chama kiungwana kabisa angetangaza tu kwamba hatagombea. Katika hili la Mbowe kung"atuka hofu yangu ni moja tu CHADEMA isije kuwa kama ACT wazalendo; nimetoa mfano wa ACT kwa tukio la Nondo kutekwa, chama hicho kilionekana kwamba Zitto ni kama ndio bado Kiongozi wa Chama, mimi mpaka leo ukiniuliza Kiongozi wa ACT ni nani kiukweli simjui. Mbowe mpe nafasi Lissu baki kuwa mshauri wa Chama vinginevyo neno Demokrasia litakua halina maana yoyote zaidi ya kubakia kiini macho kumbe ndani yake kumejaa ubinafsi mtupu.
SALAMU ZANGU KWA JACOB BONIFACE NA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA MBEYA.
Jifunzeni kunyamaza, nimeona maandiko yenu na matamko yenu. Naomba niwakumbushe kidogo, mwaka 2005 wakati JK anatangaza nia ya kugombea Urais wapo watu viongozi walijitokeza hadharani na kumpinga JK asigigombee Urais na waliokuwa wengi walikua team Monduli. Mmmoja wa Wakuu wa Mikoa aliyekuja hadharani na kutokubaliana na JK kupewa hiyo nafasi alikua mzee wangu Mashishanga wakati huo kama nakumbuka vizuri alikua Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Wote mnajua nini kilitoke baada ya JK kuchukua urais wa nchi. Jifunzeni kutokana na hili.
Liachieni sanduku la kura litoe maamuzi lakini sio kupayuka hadharani kwa sababu Lissu nae ni binadamu,
JIFUNZENI KUNYAMAZA ITAWASIDIA SANA KUBAKI KWENYE MIKONO SALAMA.