WembeMkali
JF-Expert Member
- Jun 16, 2007
- 282
- 3
Mzee S.H.Kasori,
Asante sana kwa ujumbe wako mzito.
Sisi kama vijana wa Taifa hili tunapenda sana kuendelea kupata mawazo ya busara kama haya kutoka kwa wazee wetu.
Naomba niungane na wewe hasa kwenye masuala ya maadili kwa viongozi wetu,kukemea ufisadi na elimu nchini mwetu.
Ni kweli kabisa kuwa hali ya shule,vyuo vyetu vikuu,na sekondari zetu ni mbaya mno.Busara inahitajika ili kuweza kubadilisha hali hii na kuwakomboa watanzania ambao wengi wanategemea sana vyuo hivyo na shule hizo ili kuweza kupata ujuzi na maarifa ya kupambana na kukabiliana na maisha yao ya kila siku.
Serikali yetu imetutupa sana kwa hili,tunasikia tu nyimbo za ujenzi wa shule kwa nguvu za wananchi wakati serikali yenyewe inatenga fungu dogo kwenye sekta ya elimu kwa kweli huu ni usaliti.
Tunachoona ni mashangingi ya kila aina yakinunuliwa na wakuu wetu wa kiserikali huku hali yetu ya kimaisha hailingani kabisa na gharama hizo. Kuna wakati huwa najiuliza kuwa hawa viongozi wana vichwa vyenye akili au vina maji ndani yake? Mbona busara zao ni ndogo namna hiyo?
Basi mzee wetu tunatumaini kuwa viongozi wetu watayaona haya machache uliyoyasema na pengine huruma itawaingia mioyoni mwao ili waweze kuwasaidia watanzania .
-Wembe