Ushauri kwa wafanyabiashara mitandaoni (online)

Carnivora

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,650
Reaction score
6,015
Habari za usiku mabibi na mabwana.

Ni matumaini yangu kuwa mnaendelea vema na shuguli zenu za kila siku. Wenye matatizo poleni na endeleeni kupambana kumaliza hayo matatizo.

Naam, niende kwenye mada.

Kumekuwa na fursa kubwa sana ya kupata wateja wa bidhaa mbali mbali katika mitandao ya kijamii. Hapa nazungumzia Instagram, Facebook, Twitter n.k . Maendeleo ya teknolojia yameleta mapinduzi makubwa ya kibiashara hata namna tunavyofanya shughuli nyingi za kila siku. Watu wengi wanamiliki simu janja (smart phones), hivyo kumekuwa na uwanja mpana wa kupata wanunuzi ambao ni watumiaji wa mitandao hiyo. Unaweza kuwa unauza vitu mtandaoni na wala huna duka wala store maalum.

Nimeamua nitoe ushauri kwa watu wanaofanya biashara kwa kujitangaza humo mitandaoni kwa sababu nina uzoefu nilioupata nikiwa kama muuzaji na pia mnunuzi. Ni changamoto ndogo ndogo lakini zina athari (impact) kubwa kibishara ya mitandaoni. Wengi wanakosea sana. Hivyo ushauri wangu ni kama ifuatavyo:

1. WEKA BEI
Hili ni tatizo kubwa mno, unakuta mtu anapost bidhaa yenye picha kali inamvutia mtazamaji lakini maskini hakuna bei. Labda tuulizane, sote tunaijua THE POWER OF PRICE TAG? Kuweka bei kuna faida kuu mbili.

Moja inamfanya mnunuzi tarajai (potential customer) afanye maamuzi hapo hapo, kwamba kitu kakipenda je ana pesa ya kununua? Ikiwa jibu ni ndio anapiga simu/ana wasiliana nawe moja kwa moja akitaka kujua namna ya mzigo kumfikia na namna ya kulipa sio tena kuanza kuuliza bei kisha muanze bargaining.

Faida ya pili ni context ya wateja wetu wengi. Inafahamika watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii ni vijana miaka 18-40, ndio maana bidhaa nyingi zinazouzwa mitandaoni zinawagusa watu hawa. Kwa context yetu ya Kibongo bongo vijana 22 mpaka 35 umri wengi wanasoma na walio na kazi basi hawajakaa vizuri sana kiuchumi. Hawa ni watu wa kuwawekea bei kabisa waamue hapo hapo.

Sio matajiri hao ambao pesa yao hawaifikirii sana. Sambamba na hilo usipoweka bei inaashiria unafanya ulanguzi, yaani kila anayekuja unampa bei yake. Ndo unakuta post nzuri kisha chini kwenye comments wanauliza bei au kaandika price DM. Nije DM uniatapeli? Sio kitu kizuri.

2. INTERACT NA WATEJA WAKO
Namaanisha ukishapost tangazo lako liwe la kulipia au post ya kawaida basi jitahidi uwe unajibizana na commentators wako. Kuna wanaouliza je rangi fulani ipo? Au wanataka maelezo ya ziada uwe active kuwapa, wataona ni mtu serious na utapata wateja.

3. JIBU MESSAGE/CALL BACK NA/AU POKEA SIMU KWA WAKATI
Hili nalo ni jipu kubwa sana. Unakuta muuzaji kaweka namba pale kwenye post yake. Ukipiga haipokelewi na/au ukipiga anajibu mtu atakayesema hayupo dukani kabisaa kwa wakati huo. Atakwambia mpigie wa dukani. Sasa unajiuliza mliweka namba ya kazi gani kama wewe haupo dukani.

Pia kuna wale anakwambia DM for purchase. Ukienda huko DM hujibiwi au baada ya siku nzima ndo unajibiwa. Yaani hapo dakika chache sana unapoteza wateja. By experience nilimpigia mtu ninunue saa ya mkononi Makumbusho pale, aliyepokea akaniambia yeye hakai dukani mara kwa mara.

4. ELEKEZA MTEJA VIZURI ULIPO
Hili linawahusu wale ambao wanapokea simu kisha mteja anauliza duka lilipo na mhudumu anashindwa au anafanya makusudi kutomuelekeza mteja. Hii iliwahi nikuta wife aliniagiza sabuni fulani hivi nimchukulie akanipa na namba., nimepiga aliyepokea ananimbia njoo Magomeni mtaa wa Fundikira.

Nikamwambia sipajui hebu nielekeze natokea Kinondoni! Akarudia hivyo hivyo na kuongeza njoo tu Magomen shuka kituo gani sijui vile (nimesahau jina). Dada siji na daladala nielekeze vizuri, simu ikakatwa as if kila mtu anaijua Magomeni yote mwanzo mwisho. Kwa msaada wa Google map nikafika. Na ni kwasababu tu ni wife anahitaji, otherwise nisingekwenda. Kufika kwa mteja kunaweza mfanya anunue bidhaa nyingine pia ziada ya kile kilichomleta.

5. KUWA MWAMINIFU
Usiache au usikubali mteja wako alalamike kwa hali yoyote ile. Ulichopost na mteja alichochagua muuzie kama kilivyo. Kama kuna defection yoyote mwambie kabla hajatoa pesa yake. Usijedanganya jeans hii haivutiki kumbe ya mpira au suruali hii haipauki wakati tunajua cadet nyingi hupauka vibaya mno. Eleza ukweli ubora wa bidhaa yako kwenye maelezo. Pia usitapeli watu, ukitumiwa pesa tuma mzigo. Uaminifu ni MTAJI mkubwa sana.

6. Lastly, tunza kumbukumbu za mawasiliano ya wateja wako. Product mpya ikija watumie huenda wakawa interested ukauza. Kwa kutumia whatsapp unaweza andaa broadcast list ukawatumia wote kwa pamoja na amini nakuambia, ukiwatumia watu 100 basi kuna angalau asilia 5 yaani watu 5 utauza kwao. Kuna fashion and trend lovers hawapitwi na kitu, catch them up. Usitegemee tu wateja wapya.

Naomba niishie hapa. Mengine kwenye comments. Unaruhusiwa kuongezea yanayofaa.

Asanteni.
Tattoo
 
Njema sana.

Suala la kuweka mpangilio mzuri wa tangazo hujaligusia naona. Mana utakuta kuna mtu kaweka tangazo utadhani ni mtoto wa darasa la 3B, tangazo halivutii hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili sijaligusia sana sababu nimeexperience wengi wanaweka picha na maelezo mazuri tu. Wanapiga picha na kwa kutumia app mbali mbali wananonegesha. By the way asante pia kwa kuligusia suala hilo, ni muhimu pia.
 
App gani za simu unatuma kuedit picha in total? Naomba ziorodheshe zote tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Canva mkuu ni Moto wa kuotea mbali.ingia play store ipakue
20200722_181926_0000.jpg
20200722_184140_0000.jpg
 
Habari za usiku mabibi na mabwana.

Ni matumaini yangu kuwa mnaendelea vema na shuguli zenu za kila siku. Wenye matatizo poleni na endeleeni kupambana kumaliza hayo matatizo.

Naam, niende kwenye mada.

Kumekuwa na fursa kubwa sana ya kupata wateja wa bidhaa mbali mbali katika mitandao ya kijamii. Hapa nazungumzia Instagram, Facebook, Twitter n.k . Maendeleo ya teknolojia yameleta mapinduzi makubwa ya kibiashara hata namna tunavyofanya shughuli nyingi za kila siku. Watu wengi wanamiliki simu janja (smart phones), hivyo kumekuwa na uwanja mpana wa kupata wanunuzi ambao ni watumiaji wa mitandao hiyo. Unaweza kuwa unauza vitu mtandaoni na wala huna duka wala store maalum.

Nimeamua nitoe ushauri kwa watu wanaofanya biashara kwa kujitangaza humo mitandaoni kwa sababu nina uzoefu nilioupata nikiwa kama muuzaji na pia mnunuzi. Ni changamoto ndogo ndogo lakini zina athari (impact) kubwa kibishara ya mitandaoni. Wengi wanakosea sana. Hivyo ushauri wangu ni kama ifuatavyo:

1. WEKA BEI
Hili ni tatizo kubwa mno, unakuta mtu anapost bidhaa yenye picha kali inamvutia mtazamaji lakini maskini hakuna bei. Labda tuulizane, sote tunaijua THE POWER OF PRICE TAG? Kuweka bei kuna faida kuu mbili.

Moja inamfanya mnunuzi tarajai (potential customer) afanye maamuzi hapo hapo, kwamba kitu kakipenda je ana pesa ya kununua? Ikiwa jibu ni ndio anapiga simu/ana wasiliana nawe moja kwa moja akitaka kujua namna ya mzigo kumfikia na namna ya kulipa sio tena kuanza kuuliza bei kisha muanze bargaining.

Faida ya pili ni context ya wateja wetu wengi. Inafahamika watumiaji wakubwa wa mitandao ya kijamii ni vijana miaka 18-40, ndio maana bidhaa nyingi zinazouzwa mitandaoni zinawagusa watu hawa. Kwa context yetu ya Kibongo bongo vijana 22 mpaka 35 umri wengi wanasoma na walio na kazi basi hawajakaa vizuri sana kiuchumi. Hawa ni watu wa kuwawekea bei kabisa waamue hapo hapo.

Sio matajiri hao ambao pesa yao hawaifikirii sana. Sambamba na hilo usipoweka bei inaashiria unafanya ulanguzi, yaani kila anayekuja unampa bei yake. Ndo unakuta post nzuri kisha chini kwenye comments wanauliza bei au kaandika price DM. Nije DM uniatapeli? Sio kitu kizuri.

2. INTERACT NA WATEJA WAKO
Namaanisha ukishapost tangazo lako liwe la kulipia au post ya kawaida basi jitahidi uwe unajibizana na commentators wako. Kuna wanaouliza je rangi fulani ipo? Au wanataka maelezo ya ziada uwe active kuwapa, wataona ni mtu serious na utapata wateja.

3. JIBU MESSAGE/CALL BACK NA/AU POKEA SIMU KWA WAKATI
Hili nalo ni jipu kubwa sana. Unakuta muuzaji kaweka namba pale kwenye post yake. Ukipiga haipokelewi na/au ukipiga anajibu mtu atakayesema hayupo dukani kabisaa kwa wakati huo. Atakwambia mpigie wa dukani. Sasa unajiuliza mliweka namba ya kazi gani kama wewe haupo dukani.

Pia kuna wale anakwambia DM for purchase. Ukienda huko DM hujibiwi au baada ya siku nzima ndo unajibiwa. Yaani hapo dakika chache sana unapoteza wateja. By experience nilimpigia mtu ninunue saa ya mkononi Makumbusho pale, aliyepokea akaniambia yeye hakai dukani mara kwa mara.

4. ELEKEZA MTEJA VIZURI ULIPO
Hili linawahusu wale ambao wanapokea simu kisha mteja anauliza duka lilipo na mhudumu anashindwa au anafanya makusudi kutomuelekeza mteja. Hii iliwahi nikuta wife aliniagiza sabuni fulani hivi nimchukulie akanipa na namba., nimepiga aliyepokea ananimbia njoo Magomeni mtaa wa Fundikira.

Nikamwambia sipajui hebu nielekeze natokea Kinondoni! Akarudia hivyo hivyo na kuongeza njoo tu Magomen shuka kituo gani sijui vile (nimesahau jina). Dada siji na daladala nielekeze vizuri, simu ikakatwa as if kila mtu anaijua Magomeni yote mwanzo mwisho. Kwa msaada wa Google map nikafika. Na ni kwasababu tu ni wife anahitaji, otherwise nisingekwenda. Kufika kwa mteja kunaweza mfanya anunue bidhaa nyingine pia ziada ya kile kilichomleta.

5. KUWA MWAMINIFU
Usiache au usikubali mteja wako alalamike kwa hali yoyote ile. Ulichopost na mteja alichochagua muuzie kama kilivyo. Kama kuna defection yoyote mwambie kabla hajatoa pesa yake. Usijedanganya jeans hii haivutiki kumbe ya mpira au suruali hii haipauki wakati tunajua cadet nyingi hupauka vibaya mno. Eleza ukweli ubora wa bidhaa yako kwenye maelezo. Pia usitapeli watu, ukitumiwa pesa tuma mzigo. Uaminifu ni MTAJI mkubwa sana.

6. Lastly, tunza kumbukumbu za mawasiliano ya wateja wako. Product mpya ikija watumie huenda wakawa interested ukauza. Kwa kutumia whatsapp unaweza andaa broadcast list ukawatumia wote kwa pamoja na amini nakuambia, ukiwatumia watu 100 basi kuna angalau asilia 5 yaani watu 5 utauza kwao. Kuna fashion and trend lovers hawapitwi na kitu, catch them up. Usitegemee tu wateja wapya.

Naomba niishie hapa. Mengine kwenye comments. Unaruhusiwa kuongezea yanayofaa.

Asanteni.
Tattoo
Hongera Sana mkuu kwa Uzi huu was Moto. Umegusa mule mule
 
Uzi mzuri nami nichangie. Pia Facebook wameinunua Instagram, na hivi karibuni wamenunua pia whatsapp. Ukiona bidhaa yako inahitaji kuwapa elimu kwanza watumiaji mfano kupunguza uzito,nguvu za kiume, lishe n.k unaweza link Facebook na whatsapp, kisha whatsapp ikawa ndiyo platform ya walengwa wako,

Kutatua changamoto zao,hivyo watakuamini na inakuwa rahisi kufanya biashara. Nicheki kwa 0713039875 kwa wanaohitaji msaada bure wa kulink hizi app 3.

wifi new.png
 
Back
Top Bottom