Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,518
- 10,839
Huu ni ushauri kwa mliomaliza kidato cha 4 (O-Level) mwaka huu na mnafikiria kujiunga na chuo japokuwa mna ufaulu mzuri wa kujiunga A-Level. Kama ni mzazi una mtoto aliyemaliza masomo hayo na ana wazo hili unaweza kumpatia ushauri huu. Natoa ushauri huu from experience na niliyoyaona baada ya mimi kupita njia hiyohiyo.
Kumekuwa na wimbi kubwa la wahitimu wengi wa kidato cha 4 kukwepa masomo ya A-Level wakiona kama ni kupoteza muda kwasababu tu ukipita chuo unapata ujuzi kwa fani unayoitaka, unaokoa muda (which isn't true), kupata ajira za diploma, kukimbia masomo ya A-Level yanayoaminika kuwa ni magumu.
Ila ni lazima wanafunzi wajue umuhimu wa masomo ya A-Level. Kwenye ngazi za kielimu A-Level inakupa hadhi ya "High School Graduate" ambayo kuipata kwenye nchi nyingi ni 12 years in school, sasa ukiishia form 4 unahesabika kama mtu ambaye hajahitimu High School. Pia, A-Level hutoa ujuzi muhimu na maarifa ambayo huunda msingi wa elimu zaidi na stadi za maisha. Wanafunzi hupata msingi mzuri kwa masomo kama: hesabu, sayansi na sanaa ya lugha.
Kimataifa elimu zinazotolewa Tanzania na kutambulika ni High School (A-Level), Bachelor's Degree, Master's Degree. Kutokana na Utandawazi na mapinduzi ya Teknolojia ni vyema kuendana na kasi ya Dunia kwa kuwa na International Credentials, hii itakupa wigo mpana kwenye soko la ajira na hata elimu pia.
Sasa tukirudi kwenye my experience, mwaka jana nilitaka kwenda kujiendeleza kielimu nje ya nchi, Central Europe. Shida ikaja kwenye vyeti nilivyonavyo kwakuwa sikuhitimu High School (12 years) nikawa sikidhi vigezo vya kujiunga na masomo hayo, japokuwa tayari nilikuwa nimefanya post-secondary studies. Ikatakiwa nifanye Foundation Program, ambayo inaongeza gharama za kifedha na muda wa mwaka mmoja.
So ushauri wangu ni vyema upite A-Level then, Bachelor's Degree. Ukihitimu unakuwa na ngazi mbili za kielimu zinazotambulika kimataifa. Hapahapa nchini kuna waajiri wanataka watu waliohitimu High School.
Ushauri wangu kwa serikali, katika maboresho ya sera za elimu 2027 baada ya kufuta darasa la 7 na kufanya uhitimu wa elimu yetu kuwa miaka 12 badala ya 13. Waangalie namna ya kufanya O-Level na A-Level kuwa mandatory na kidato cha 4 kuwe na mtihani wa taifa kama ilivyo sasa ila kusiwe na cheti na baada ya kuhitimu A-Level ndiyo mwanafunzi apate High School Certificate.