Ushauri kwa wahitimu wa kidato cha 4 (O-Level)

Toa maelezo kuhusu hii
Foundation Program ni mwaka wa maandalizi kwa masomo ya Bachelor's Degree kwa International Students ambao hawakidhi vigezo. Vyuo vyao vinataka uwe umehitimu High School ambayo ni miaka 12, ukiwa na cheti cha O-Level ni miaka 11 hivyo unakuwa hujakidhi vigezo.
 
Mfumo wa nchi nyingi za Ulaya hazina A-level bali mwanafunzi akihitimu form four anaenda university moja kwa moja.

Anzia na mfumo wa elimu wa Netherlands nakadhalika uone kama wana ujinga wa A-level halafu linganisha na mfumo wetu wa elimu wa kukaririshwa madesa kuanzia Primary, O'level hadi A'level.

Yaani hakuna mwanafunzi anachojua nje ya alichokaririshwa darasani.

Mwanangu akimaliza form four hata awe na division one ya pointi 7 ataenda chuo na sio kupoteza muda A'level kama wengi tulivyopoteza.

Tunakutana na mabumunda yaliyohitimu A'level mtaani unamuuliza swali la mtego kidogo tu ya kile ambacho walifundishwa shuleni haelewi chochote.

Nimesoma chuo na watu waliopitia certificate kisha diploma halafu wale wa fresh from school (A'level) wanakimbizwa vibaya sana kazi za group za wanasaidiwa na watu wa diploma.

Hata matokeo ya mwisho watu wa diploma wanaongoza kwa mbali kwasababu wana uzoefu na msingi wa profession tangu certificate.
 
OUT itamuhusu au sio?
 
Wazazi wanataka shortcut kwenye maisha. Na wengi hawana exposure kabisa. Mimi naona ni ukatili kwa mtoto kumwekea limits kwenye maisha yake. Mtoto mwenye elimu ya A - Level ana nafasi kubwa ya kupata fursa nyingi kimataifa.
 
Aah sawa je mitaala inayotumika Advance hapa kwetu ni sawa na mitaala inayotumika kwao?
Mfumo wetu wa elimu utakaoanza kutumika 2027 unaweza kufanana na England. Unapozungumzia mtaala (curriculum) kwa shule zetu za Serikali ni tofauti kabisa na International Schools zilizopo hapahapa nchini. Kinachofaya A-Level itambulike kimataifa ni miaka inayohitajika mwanafunzi kuhitimu, hapa kwetu mwanafunzi anakaa shule miaka 13 kuhitimu High School ambayo ni zaidi ya ile inayotambulika kimataifa (12).
 
Una akili za kimaskini sana.
 
Wamepunguza sasa kuna la 6 ndio mwisho ila bado inasoma 13 mwanzo ilikua 14
 
Ni lazima mfumo wa elimu ubadilishwe. Tuwaige hata majirani zetu Kenya, baada ya kufutwa darasa la 6 tutakuwa tunaenda sawa na sera za elimu za kimataifa ila tunapaswa kuwa na ngazi moja tu ya elimu ya upili inayotambulika ili kuachana na hizi O-Level & A-Level.
 
Wazazi wanataka shortcut kwenye maisha. Na wengi hawana exposure kabisa. Mimi naona ni ukatili kwa mtoto kumwekea limits kwenye maisha yake. Mtoto mwenye elimu ya A - Level ana nafasi kubwa ya kupata fursa nyingi kimataifa.
Kweli kabisa, serikali inapaswa kuangalia namna nzuri ya kufanya elimu ya upili iwe ile inayotambulika kimataifa ikiwa na maana elimu ya juu kabisa kwa secondary iwe inakamilisha miaka 12. Kenya mfumo wao ni 8-4-4 maana yake ukitoka shule ya msingi, unaenda shule ya upili na ukihitimu moja kwa moja umekamilisha miaka 12 ya High School ambayo inatambulika Kimataifa na unaweza kujinga vyuo vya kati au chuo kikuu.

Huu mfumo wa 7-4-2 unampa mwanafunzi option ya kuishia njani na kuruka ngazi muhimu ya A-Level kwenda chuo.
 
Narudia tena na tena hapa kuandika, vijana nendeni A-level ikiwa mna ndoto za kusoma zaidi, kutokupoteza muda na kuwa na wigo mpana wa kusomea mambo tofauti tofauti au kuwa na uwanja wa kimataifa.

Diploma wakasomee watu wenye hizi sifa tu;
1. Wanaosaka ujuzi wa kwenda kuajiriwa moja kwa moja baada ya kuhitimu hiyo diploma.
2. Waliokosa sifa stahiki za kuendelea mbele zaidi kimasomo kwa njia ya moja kwa moja.
 
Hiki kitu huwa kinanishangaza sana unakuta mtoto ana sifa zote za kuingia kidato cha Tano ila mzazi sijui anatoa wapi ushauri anaacha kumpeleka mtoto.

Halafu badae anaanza kulia.
Advance Level ni nzuri sana.
Na mimi najiuliza. Mtoto kachaguliwa form five, kwa nini asiende kusoma hiyo miaka miwili ili akimaliza asone Diploma mana wengine wanaona Diploma ni rahisi kuajiriwa kuliko Degree
 
Huo ndio ukweli. Mwanangu alitakiwa kujiunga na A level mm nikagoma nikampeleka diploma ya CO Iringa sasa hivi anaajira ya serikali na anajisomea mengine taratibu wakati anauhakika yupo kazini
 
Huo ndio ukweli
 
Kama hajasoma physics basi aende tu high school.
Vyuo vya Kati ni vizuri kwa upande wa afya na engineering tu zile kozi zingne ni Bora akatokea advance tu ili aje kupata mkopo.
Kitu kingine kinachopelekea watu kukimbia advance ni competition ya kupata vyuo Bora vyaa gvt kwa ajiri ya kozi nzri Kama medical doctor, n.k.
Nimeshuhudia watu wamesoma pcb na wakafaulu vzr kwa dv 1 of 8 pnt lkn walikosa hata nafasi ya nursing kwa vyuo vya gvt kwa sababu kule wanataka angalau pnt 6 kwenye masomo husika,
wamejikuta wanasoma food science, natural science na course zingne za afya ambazo hata mtu Alie soma CBG anaweza kuzisoma.
 
Shida yako unatoa maoni kwa kaungalia njia wewe,ambayo sio njia ya kila mtu wengine hawana haja ya kwenda nje na wengine kamwe hawataajiriwa
 
Mkuu kama sina haja ya kwenda huko ughaibuni kuna haja gani ya kwenda A-Level?Maana umejieleza sana lakini mwisho ukasema wewe umekwama kwenda eirope kwa sababu hukusoma A-level. Ushauri wako ni mzuri sana
 
Mkuu kama sina haja ya kwenda huko ughaibuni kuna haja gani ya kwenda A-Level?Maana umejieleza sana lakini mwisho ukasema wewe umekwama kwenda eirope kwa sababu hukusoma A-level. Ushauri wako ni mzuri sana
Ni ushauri tu, hata mimi nilipomaliza O-Level sikuona umuhimu wa A-Level nikaachana nayo.

Huu ni ushauri kwa wale waliomaliza kidato cha 4 na wapo njia panda kufanya maamuzi wachukue ngazi ipi kielimu.
 
Unakitu utafika mbali mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…