Ushauri kwa wanaotunza pesa za wafanyakazi wa serikali/Binafsi-pesa za kustaafu (NSSF/PSSF)

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
7,005
Reaction score
9,264
Huu ni Ushauri tu ila najua kwasababu mtu mweusi ni mnyimina mbinafsi hamtaupokea kwasababu unagusa maslahi ya fedha

Ni hivi, Wafanyakazi wa serikali/binafsi wanakatwa pesa yao kila siku kwa ajili ya mafao baada ya kustaafu ila ukweli ni kwamba pesa ile haizalishi chochote kile zaidi ya kutumiwa isivyo halali na taasisi hizo-tuliona jinsi pesa hivyo zilivyopigwa hadi mafao yanakosekana

SASA basi, sasa hivi tuna UTT na takataka kibao za UWEKEZAJI, kwanini watumishi wasiruhusiwe ku "roll over" mafao yao kwenye hizi taasisi za uwekezaji ili wapate faid(kwasababu pesa inakua na kujizalisha) ila wasiruhusiwe kutoa mpaka watakapo staafu.

mtumishi ana 50m ya mafao na bado hajastaafu achukue milioni 40 aweke UTT(mfano) wakati anastaafu atakua na zaidi ya atakachokipata akiweka huko NSSF/PSSF

Nadhan nimeeleweka
 
Sijui PSSF mnaishije, lakini huku NSSF kuna ka offer ka bima ya Afya.. UTT wataweza kutoa hiyo offer?

Pia wangeweka hata mtu aweze kupata mkopo kupitia mafao yako walau hata asilimia kadhaa kwenye 💯

Ila hawawezi fanya hayo bila NRNE
 
Mtumishi wa Serikali ana bima ya NHIF haitaji double bima
huwezi kukopea mafao(dunia nzima) mafao hayakopewi sababu wanajua kabisa kuna watu hawatalipa na watastaafu hawana kitu
 
Kwahiyo mtumishi pekee ndio apendelewe kisa ana bima mbili??
Hizo hizo NHIF mnazozilalamikia kila siku?
 
Huu ni Ushauri tu ila najua kwasababu mtu mweusi ni mnyimina mbinafsi hamtaupokea kwasababu unagusa maslahi ya fedha

Ni hivi, Wafanyakazi wa serikali/binafsi wanakatwa pesa yao kila siku kwa ajili ya mafao baada ya kustaafu ila ukweli ni kwamba pesa ile haizalishi chochote kile zaidi ya kutumiwa isivyo halali na taasisi hizo-tuliona jinsi pesa hivyo zilivyopigwa hadi mafao yanakosekana

SASA basi, sasa hivi tuna UTT na takataka kibao za UWEKEZAJI, kwanini watumishi wasiruhusiwe ku "roll over" mafao yao kwenye hizi taasisi za uwekezaji ili wapate faid(kwasababu pesa inakua na kujizalisha) ila wasiruhusiwe kutoa mpaka watakapo staafu.

mtumishi ana 50m ya mafao na bado hajastaafu achukue milioni 40 aweke UTT(mfano) wakati anastaafu atakua na zaidi ya atakachokipata akiweka huko NSSF/PSSF

Nadhan nimeeleweka
NSSF na PSSF ni njia ya serikali kuwanyonya wafanyakazi
 
Kwahiyo mtumishi pekee ndio apendelewe kisa ana bima mbili??
Hizo hizo NHIF mnazozilalamikia kila siku?

Depal naongelea watumishi wa sekta binafsi na serikali kuwa mafao yao waweze kuyawekeza ingali wapo kazini bado siongelei bima ya afya

pia UTT kuna kifurushi kina bima pia ni wewe uchaguzi wako tu
 
Hauwatakii mema,unataka watu wastaafu bila senti?
Kivipi? yaani uwekeze utt ufe masikini??? ukiwekeza milioni arobain leo unajua unakua na salio mara zaidi ya serikali itakachokupa ukistaafu hapa umeweka 40m kwa 25years kwa rate ya 10% kwa mwaka
uttaa.jpg
 
Back
Top Bottom