Ushauri kwa watenda dhambi wenzangu

Ushauri kwa watenda dhambi wenzangu

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Ninajiita mtenda dhambi ila niliyesamehewa, kwasababu hakika ninafichwa na kafara la Damu ya Yesu Kristo tu mbele za Mungu, na hii ni baada ya kukabidhi maisha yangu kwake kwa maana ya kuokoka. Amekuwa Mungu wangu, mwokozi wangu, akiniangalia hanioni mimi, anaona kafara la Damu ya Yesu kwasababu nimekabidhi maisha kwake kwa njia ya Kumkiri Yesu, na hiyo Damu ndio Damu ya Agano Jipya iletayo ondoleo la dhambi.

Simaanishi kwamba kwasababu Neema ipo hivyo niwe natenda dhambi kwasababu nimeshakabidhi maisha kwake, Noo, najiona kila siku mimi ni mdhaifu nahitaji msaada wa Mungu, najitakasa kila siku na kuukimbia uovu kwa msaada wake, ili niishi maisha matakatifu. Biblia inasema

Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.. (UFUNUO 22:11)

Maishani mwangu nilishawahi kuwa mtenda dhambi sana, nilimuudhi sana Mungu, tena nikiwa naijua kweli, nilikuwa kwenye kifungo cha uzinzi, ujeuri, kiburi na kila kitu, ilifika mahali nikawa naamini pengine kilichobaki kwangu ni adhabu tu, dhambi zangu ni nyingi mno, labda Mungu asingenisamehe. Lakini baada ya kusoma Neno lake, nilikuja kugundua kuwa, pamoja na kwamba huwa anaadhibu pia, Mungu ni mwenye huruma mno kwetu, siku zote anasubiri tugeuke, tutubu ili atusamehe, ni mwenye hasira lakini hashiki hasira zake milele, huwa anaghairi kutufanyia mabaya, naye hurufahia rehema. Yaani pale anapoturehemu huwa anafurahia.

La kufahamu ni kwamba, ukitenda dhambi usiitubie, lazima itakutafuna tu, it is just a matter of time, na hata isipokutafuta katika ulimwengu huu, itakusababisha uende moto wa milele. Ila ukijijua una dhambi, ukatubu kwa kumaanisha kuziacha, Mungu huzifuta na kuzitupa kwenye kilindi cha bahari, hatazikumbuka tena, hata kama wewe utazikumbuka yeye Mungu ameamua kuzisahau kwasababu anazifuta kabisa kabisa na unabaki bila dhambi.. mimi dhambi zangu mtu akinikumbusha huwa nawaambia, MUNGU ALISHANISAMEHE, ALISHAZIFUTA, MIMI SINA DHAMBI, KAMA UNAZIKUMBUKA KAJADILIANE NA MUNGU HUKO, USIJADILIANE NA MIMI. Na huu ndio ukweli.

ISAYA 43:25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.

Yoe.2:12-13 "Lakini sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza, RARUENI MIOYO YENU, WALA SI MAVAZI YENU; Kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira ni mwingi wa rehema; naye hughairi mabaya"

MIKA 7: 18 – 19. Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hashiki hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema. Atarejea na kutuhurumia; atayakanyaga maovu yetu, nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari.

Zaburi 103:11-13"Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao."

USHAURI WANGU KWENU: siku zote mshahara wa dhambi ni mauti, ila ukitubu Mungu anakupa uzima wa milele. Hivyo asiwepo mtu wa kuwavunja moyo, kwamba labda mmekuwa watenda dhambi sana hamtasamehewa, No. Mungu atawasamehe. Haijalishi umetenda dhambi gani, labda ukiondoa ile ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Tubu,rudi kwa Mungu, atakusamehe, atasahau dhambi zako, utakuwa kiumbe kipya. Kwa lugha nyingine, Mungu hana kisirani, hakasiriki milele, huwa anasamehe ukijirudi.
 
Wanadamu huwa wanatoa hukumu sana, asije mtu akakuhukumu kana kwamba dhambi zako/maisha uliyoishi haustahili msamaha. wanadamu wana tabia ya kupima viwango vya dhambi, ni kama wanaona dhambi hii huyu asamehewe, ila hii akafie mbali huko. Tofauti yake, Mungu hahukumu kama wanadamu wahukumuvyo, tunaona hata yule KAHAMA aliyemwendea Yesu, wengi aliona kwanini mtu mchafu anamsogelea Yesu? pia Yona kule NInawi, alisikitika kwanini kwa maovu mengi watu wa Ninawi walifanya, Mungu aliamua kusamehe baada ya kutubu? jibu nikwamba, Mungu ni mwenye rehema na neema, kuna wakati anatusamehe tu kwa neema hata kama tumemuudhi kwa kustahili kifo, naye hughairi kutuadhibia mabaya na hufurahia rehema. hivyo hivyo ulivyo, unavyojiona hufai, njoo kwa Mungu, atakusamehe, atafuta dhambi zako, utakuwa sawa na wale ambao hawana dhambi. huu ni ujumbe wa muhimu sana kwako.
 
Hivi kuna binadamu asiyetenda dhambi kweli! Walokole acheni unafiki.
wala sio uanfiki, hakuna mwanadamu asiye na mapungufu, ila inategemeana mwanadamu huyo yupo mikononi mwa nani, mwa Yesu ambaye alikufa hivyo dhambi zinafunikwa na Yesu au yupo kwa shetani. mwenye kujitakasa azidi kujitakasa, ndio maana tunamhitaji Mungu, tunajitakasa kwasababu huwa tunatenda dhambi pia.
 
Mhubiri 7:20
Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, atendaye mema pasipo kutenda dhambi
inategemeana upo mikononi mwa nani. sote huwa tunakosea here and there, ukiwa umeokoka upo mikononi mwake utatubu na anakusamehe, ikiwa haujaokoka, unakuwa mbali na uso wa Mungu.

1YOHANA 2:1 INASEMA; Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
 
Watenda dhambi wapo kwenye ule uzi pendwa sidhani kama kunamtu ataenda mbinguni.Kwahiyo wewe mtoa mada nenda kwenye ule uzi ukawahubilie.
 
Watenda dhambi wapo kwenye ule uzi pendwa sidhani kama kunamtu ataenda mbinguni.Kwahiyo wewe mtoa mada nenda kwenye ule uzi ukawahubilie.
sisi sote, mimi na wewe, tunahitaji neema ya Mungu. mara nyingi tunamkosea Mungu kwa mawazo na matendo, kwa kujua au pengine hata kwa kutokujua. tunahitaji neema ya Mungu. utofauti wetu tu ni mmoja anateleza akiwa mikononi mwa Mungu, mwingine anateleza akiwa kwenye laana kwasababu hajakabidhi maisha yake kwa Mungu. ila sote hapa au pale, humkosea Mungu. tunatofautiana tu tunamkosea kwa namna gani. hata mtoto wako haimaanishi siku zote yeye ni malaika, atakuudhi tu ila ni mtoto wako, utamvumilia na kumsaidia, ila asiye wako unaweza usimvumilie. ndio maana tunasema watu wakabidhi maisha kwa Mungu. wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina lake. manake wale wasiompokea sio watoto wa Mungu, kwasababu wamekataa kumpokea yeye aliye Mungu wa kweli. ni hiari yao. ila siku wakiamua kukabidhi maisha kwake, watakuwa watoto wa Mungu pia. Yohana 1:1
 
sisi sote, mimi na wewe, tunahitaji neema ya Mungu. mara nyingi tunamkosea Mungu kwa mawazo na matendo, kwa kujua au pengine hata kwa kutokujua. tunahitaji neema ya Mungu. utofauti wetu tu ni mmoja anateleza akiwa mikononi mwa Mungu, mwingine anateleza akiwa kwenye laana kwasababu hajakabidhi maisha yake kwa Mungu. ila sote hapa au pale, humkosea Mungu. tunatofautiana tu tunamkosea kwa namna gani. hata mtoto wako haimaanishi siku zote yeye ni malaika, atakuudhi tu ila ni mtoto wako, utamvumilia na kumsaidia, ila asiye wako unaweza usimvumilie. ndio maana tunasema watu wakabidhi maisha kwa Mungu. wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina lake. manake wale wasiompokea sio watoto wa Mungu, kwasababu wamekataa kumpokea yeye aliye Mungu wa kweli. ni hiari yao. ila siku wakiamua kukabidhi maisha kwake, watakuwa watoto wa Mungu pia. Yohana 1:1
Mkuu umesha tembelea ule uzi natamani nione kisa chako.
 
Mkuu ulisha tembelea ule uzi vipi umeshatupia kisa chako.
ni uzi gani? niende huko pia nikasaidie watu wamjue Mungu. hata ikiwa bar, hata kwenye danguro Neno la Mungu litafika. cha muhimu watu wajue, hii dunia kuna siku itakunjwa kama karatasi, wanadamu watahukumiwa kila mmoja sawasawa na matendo yake ambayo hakuyatubia. Neema ya msamaha wa dhambi, na wokovu kwa Yesu Kristo bado ipo, neema hiyo utaifaidi pale ukiwa hai, ukifa ndio deadline yako ya kutubu utasubiri hukumu tu, hawawezi kukuombea ukiwa maiti ukasamehewa dhambi zako. ni uongo wa watu wa dini kwamba wanaombea mfu asamehewe huko aliko au awekwe mahali pema. Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu na kwamba Heri wafu wafao katika Bwana maana matendo yao yafuatana nao. mana yake ni kwamba, ukifa, matendo yako utaenda nayo ukahukumiwe nayo. hujui utakufa lini, hujui mwisho wako ni leo, jioni, kesho au lini, jiandae ili kama kufa ufe katika Bwana na kama kuishi uishi katika Bwana. usibahatishe, uzima wa milele sio wa bahati nasibu kwamba ikitokea nimekufa katika Bwana ije by chance, ni process ya uamuzi wako binafsi, kuamua wapi uende, Mungu ameshaweka mbele yetu njia mbili, ya uzima na mauti, sisi ndio wa kuchagua.
 
Back
Top Bottom