Ushauri kwa watenda dhambi wenzangu

Kula tunda kimasihara.
naamini mimi lilikuwa mtenda dhambi kuliko wote au pengine sawa na wale walioko huko. tofauti yetu ni kwamba dhambi za uzinzi zile ambazo ningezisimulia hapa, hakika ni nyingi mno, na baada ya kuokoka, MUNGU AMEZIFUTA, zimefutika. sihitaji hata kuzikumbuka kwasababu hazipo tena kwangu. nawaasa na wote waliotenda kama yale mimi nilikuwa natenda, wamrudie Mungu, anawasubiri warudi, atawasamehe.
 
Twende kwenye uzi wetu pendwa basi tukawahubirie
 
Kwanza naomba nikukumbushe mkuu, unajinadi wewe ulikuwa mtenda dhambi ila ujatufunulia hiyo dhambi yako ulijikita kwenye Mambo yapi.Tambua hata kwenye majukwaa humu tuna ndugu zetu walio fanya matendo ya kutisha sana zaidi yako na mwisho wa yote wametubu mbele.ya Mwenyezi Mungu na kusamehewa, ila kwako naona ni vifungu tu vya bible unatushushia🙆🏿‍♂️


Kabla ya kujiita mtenda dhambi na sisi tuishi kwa kuamini ndugu yetu amekombolewa kwa damu ya yesu, basi ungekuja na mkasa ulio pitia hadi kufikia hatua ya kujipa cheo cha mtenda dhambi haswa. Na ukijua ushuhuda ndio kutubu basi utafika mbali ila kuificha dhambi ni kuishi ndani ya dhambi.






.... Am OUT!!!
 
Dhambi WAFANYE WATU WENGINE kisha DHAMBI ZENU azibebe mtu mwengine WEWE KUWEZA?

Kuna mijitu DUNIANI NI MIPUNGUANI SANA.yani MIPUNGUANI ya kutisha.
 
Namshukuru Mungu tangu mwaka uanze sijachepuka, majaribu ni mengi sana, Mungu anatushindia
 
Dhambi WAFANYE WATU WENGINE kisha DHAMBI ZENU azibebe mtu mwengine WEWE KUWEZA?

Kuna mijitu DUNIANI NI MIPUNGUANI SANA.yani MIPUNGUANI ya kutisha.
kwa bahati mbaya usichojua, hata waganga wenu wa kienyeji wanapotoa makafara yawe ya wanadamu au wanyama, wameiga kwa Mungu. Tabia ya Mungu ni kwamba, bila kumwagika damu hakuna ondoleo la dhambi. hata mnavyochukua kuku weupe au njia weupe kupeleka kwa mashehe wenu wanaouza madawa ya suna, ni makafara waliyoiga kwa Mungu. Shetani aliiba hii kitu kwa Mungu.

Zamani hizo, kwenye desturi za wayahudi zote hata kabla mood hajazaliwa, walikuwa wanatoa makafara ya wanyama kwa kuteketeza ili wafunike dhambi walizozitenda, sasa swali likaja kwa wasio na wanyama watatoa kafara gani kwa dhambi zao, Mungu akawa ameweka mpango tangu awali kwamba, itabidi itolewe kafara moja tu yenye thamani kufuta (sio kufunika) dhambi za wanadamu wote. Nafsi ya Mungu ikavaa mwili akazaliwa kama Yesu, akafa kwa ajili ya kutoa kafara la Damu kwa dhambi za ulimwengu wote. amekufia hata wewe ili abebe dhambi zako kama utamruhusu, kama haumruhusu utazibeba mwenyewe ukahukumiwe nazo siku ya mwisho, wala hulazimishwi.

Huyu Yesu ni Mkuu kuliko mitume wote, kuliko hata mood ambaye amekufa na hajafufuka na hajawafia ninyi, alikufa kwa dhambi zake tu. unakaribishwa kwenye ukristo, huko uliko ni upotevuni ndio maana hauelewi kabisa hii hoja.
 
Mara ya Mwisho kutenda dhambi sijui ilikua ni lini
 
Ndio, unatakiwa kuokoka hata wewe hapo.
Mathayo 19:25-26

25 Wafuasi waliposikia hili walishangaa. Wakauliza, “Sasa ni nani ataweza kuokoka?”

26 Yesu akawatazama na kuwaambia, “Hili haliwezekani kwa wanadamu,”
 
Mathayo 19:25-26

25 Wafuasi waliposikia hili walishangaa. Wakauliza, “Sasa ni nani ataweza kuokoka?”

26 Yesu akawatazama na kuwaambia, “Hili haliwezekani kwa wanadamu,”
wewe sijui ni padre au mchungaji, uwe unasoma mistari yote. anzia mstari wa 23.

MATHAYO 19: 23
Hapo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kweli nawaambieni itakuwa vigumu sana kwa tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. 24 Tena nawaambieni, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” 25Wale wanafunzi waliposikia hivyo walishangaa sana, wakamwuliza, “Ni nani basi, awezaye kuokoka?” 26Yesu akawatazama, akasema, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.”

Anapokwambia, kwa binadamu haiwezekani ila kwa Mungu yote yanawezekana, unafikiri amemaanisha kwamba haiwezekani kuokoka? jaribu kutafsiri kama mtu ambaye hajawahi kwenda shule kabisa ili usiiaibishe elimu.

Matendo 2:47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
 
😁😁😁 Nacheka kama mazuri akili zenu ndogo sana,kila binadamu atabeba dhambi zake, mbona hamna sehemu iliyo andikwa MKIFANYA MAZURI ATABEBA MAZURI YENU
 
Dhambi ni Asili yaani Adamu alipokula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya aliingingiza Dunia Dhambini,
Na Dhambi ni Moja tu yaani Uasi ila matokeo ya Uasi yakaleta Uharibifu mara elfu elfu,
Tangu Adamu alipoasi kilikua hakuna msamaha wala ondoleo la Dhambi bali Dhambi ilifunikwa kwa Damu ya mnyama yaani mshahara wa Dhambi ni mauti ilimpasa Mungu kumwaga Damu ya mnyama ili Adamu aishi ni mnyama kuraruliwa na Damu ikamwagika na Adamu akavalishwa ngozi na kutolewa Eden na kutupwa nje,
Kipindi cha Israelites wanatoka Misri iliwapasa kufunika Asili yao ya Dhambi kwa kutoa sadaka ya Dhambi kwa kuhani mkuu Haruni yaani kumwaga Damu ya mnyama kufunika Dhambi na ilitolewa mara Moja kwa Mwaka patakatifu pa patakatifu kwa ondoleo la Dhambi Mwaka mzima na wasipofanya hivyo hasira ya Mungu inawaka maana wanakua wapo nje ya Utakatifu na Mungu hakai pamoja na kitu kichafu yaani chenye Asili ya Dhambi maana yeye ni Mtakatifu kwa Asili,

Mpango wa wokovu Uliandaliwa tangu Mwanzo ili hii kitu ije ifike mwisho maana ilikua ni hatari sana nje ya Israelites yaani mataifa walikua hawana Mungu yaani kina sisi mataifa tulikua pure siners tuna Asili ya Dhambi mpaka Kiama ila kwa wema wa Mungu alishatabiriwa mkombozi atakaekuja kuwakomboa watu wote Duniani kutoka katika utumwa wa Dhambi na huyo ndie Yashua Amashiach Nazarene tunamjua kama Yesu Kristo wa Nazareth
ndie pekee aliyekuja kumaliza msala maana kwanza ilimpasa awe Mtakatifu wa Mungu yaani ana Asili ya Uungu then awe na mwili wenye Asili ya Dhambi ili afanye upatanisho kwa kafara na ndio maana alizaliwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu (Mungu)
kwa bikira Mariamu (Mwanadamu)

Kwa kulinganganisha Agano la kale la mnyama kutolewa kafara ili kufunika Dhambi waliolotumia Israelites
Hapa Yesu Kristo ndie aliyetolewa kafara kwa niaba ya Mnyama kwa ondoleo la Dhambi Milele na hili ndio jambo la msingi kila Mwanadamu alitambue Asili ya Dhambi iliondolewa kwa kafara la mtu Mtakatifu yaani kusulubiwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo kuliondoa Asili ya Dhambi na tunapokea msamaha kea kulikubali hilo tu yaani kumkiri Yesu Kristo kua ndie Mungu aliyefanyika mwili na akajitoa kafara kwa ajili ya ondoleo la Dhambi Milele,
Kiufupi ni hivi ukumkiri Yesu kua ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako unakua umezaliwa mara ya pili yaani umeacha Asili ya Dhambi (Shetani) na kuingia Asili Haki (Utakatifu wa Mungu)

Hivyo basi ndugu zanguni Dhambi haindolewi kwa maneno tu bali ni Asili na inaondolewa kwa Damu tu,hivyo wote mnaodili na kuomba msamaha wa matokeo ya Dhambi yaani Matendo ya sheria na hamjaondolewa Asili ya Dhambi yaani kumkiri Yesu kua ni Bwana na Mwokozi wa maisha yenu mpo chini ya Laana na ndugu yenu ni Ibilisi na Ibilisi atatupwa Jehanam na huyo huyo Bwana Yesu Kristo!

Hivyo Yesu Kristo hakwepeki!

Mengine tutaendelea kupeana elimu!
 
Kingine kwa sisi watenda dhambi kuna namna shetani anakufanya ujione mhalifu mwenye dhambina haustahili tena kupata msamaha! Yaani unakuwa unajiona kwamba wewe ni lijambazi lisugu hata ufanyaje wewe ni wa kufa hivyohivyo! Au kama ni mzinzi/malaya unajiona hivyo ulivyo ndivyo ulipaswa uwe na haiwezekani kabisa kuwa mtu wa tofauti au kama ni mwizi, jambazi n.k KUMBE SIVYO! Shetani anakufanya ujisemee kimoyo moyo "ya nini kutubu wakati najua nitaanguka tena dhambini" kumbe sisi tu wadhaifu ni kawaida kuanguka dhambini ila cha muhimu ni kuinuka mara unapoanguka bila kuchoka! Neno la Mungu linasema hivi katika Isaya 1:18
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Haijalishi wewe ni mdhambi wa aina gani, hata dhambi zako ziwe nyeusi kiasi gani, uwe jambazi sugu, malaya, kahaba uliyekubuhu Yesu anasamehe 100%!

Umeshawahi kuadhibiwa mara kwa mara kwa kosa fulani enzi za shule, mfano kila mara unafeli hesabu au unakuwa mtukutu fulani na unaadhibiwa kiasi kwamba unajisemea moyoni nimeumbiwa kufeli hesabu hivyo hauna haja ya kufanya juhudi yoyote na unakubaliana na hali, ndivyo shetani anakufanya ujione pale unapokuwa mdhambi! Hataki uinuke anakwambie wewe ni jambazi sugu, malaya, kahaba sugu,muuaji, mwizi kaa utulie! Kumbe sivyo!
Ukigeuka na kumrudia Mungu hata dhambi zako ziwe nyekundu kama damu, zitang'arishwa na kuwa nyeupe kama theluji na haimanishi hautaanguka tena HAPANA itatokea umeanguka tena lakini muhimu usichoke kuinuka tena! Hivyo hivyo! Njia ya uzima si nyepesi!

Tumsifu Yesu Kristu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…