shuka chini
JF-Expert Member
- Feb 27, 2024
- 842
- 1,928
Andika hivi umeshawahi kula tunda kimasihara.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walokole hatutendi dhambi ila "tunaanguka kiroho" nyie ambao hamjaokoka ndio mnatenda dhambiHivi kuna binadamu asiyetenda dhambi kweli! Walokole acheni unafiki.
naamini mimi lilikuwa mtenda dhambi kuliko wote au pengine sawa na wale walioko huko. tofauti yetu ni kwamba dhambi za uzinzi zile ambazo ningezisimulia hapa, hakika ni nyingi mno, na baada ya kuokoka, MUNGU AMEZIFUTA, zimefutika. sihitaji hata kuzikumbuka kwasababu hazipo tena kwangu. nawaasa na wote waliotenda kama yale mimi nilikuwa natenda, wamrudie Mungu, anawasubiri warudi, atawasamehe.Kula tunda kimasihara.
Twende kwenye uzi wetu pendwa basi tukawahubirienaamini mimi lilikuwa mtenda dhambi kuliko wote au pengine sawa na wale walioko huko. tofauti yetu ni kwamba dhambi za uzinzi zile ambazo ningezisimulia hapa, hakika ni nyingi mno, na baada ya kuokoka, MUNGU AMEZIFUTA, zimefutika. sihitaji hata kuzikumbuka kwasababu hazipo tena kwangu. nawaasa na wote waliotenda kama yale mimi nilikuwa natenda, wamrudie Mungu, anawasubiri warudi, atawasamehe.
soma kwa umakini threat pale awali, utaelewa nilichomaanisha.
Kuna kuokoka?ikiwa haujaokoka, unakuwa mbali na uso wa Mungu.
Dhambi WAFANYE WATU WENGINE kisha DHAMBI ZENU azibebe mtu mwengine WEWE KUWEZA?Ninajiita mtenda dhambi ila niliyesamehewa, kwasababu hakika ninafichwa na kafara la Damu ya Yesu Kristo tu mbele za Mungu, na hii ni baada ya kukabidhi maisha yangu kwake kwa maana ya kuokoka. Amekuwa Mungu wangu, mwokozi wangu, akiniangalia hanioni mimi, anaona kafara la Damu ya Yesu kwasababu nimekabidhi maisha kwake kwa njia ya Kumkiri Yesu, na hiyo Damu ndio Damu ya Agano Jipya iletayo ondoleo la dhambi.
Simaanishi kwamba kwasababu Neema ipo hivyo niwe natenda dhambi kwasababu nimeshakabidhi maisha kwake, Noo, najiona kila siku mimi ni mdhaifu nahitaji msaada wa Mungu, najitakasa kila siku na kuukimbia uovu kwa msaada wake, ili niishi maisha matakatifu. Biblia inasema
Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.. (UFUNUO 22:11)
Maishani mwangu nilishawahi kuwa mtenda dhambi sana, nilimuudhi sana Mungu, tena nikiwa naijua kweli, nilikuwa kwenye kifungo cha uzinzi, ujeuri, kiburi na kila kitu, ilifika mahali nikawa naamini pengine kilichobaki kwangu ni adhabu tu, dhambi zangu ni nyingi mno, labda Mungu asingenisamehe. Lakini baada ya kusoma Neno lake, nilikuja kugundua kuwa, pamoja na kwamba huwa anaadhibu pia, Mungu ni mwenye huruma mno kwetu, siku zote anasubiri tugeuke, tutubu ili atusamehe, ni mwenye hasira lakini hashiki hasira zake milele, huwa anaghairi kutufanyia mabaya, naye hurufahia rehema. Yaani pale anapoturehemu huwa anafurahia.
La kufahamu ni kwamba, ukitenda dhambi usiitubie, lazima itakutafuna tu, it is just a matter of time, na hata isipokutafuta katika ulimwengu huu, itakusababisha uende moto wa milele. Ila ukijijua una dhambi, ukatubu kwa kumaanisha kuziacha, Mungu huzifuta na kuzitupa kwenye kilindi cha bahari, hatazikumbuka tena, hata kama wewe utazikumbuka yeye Mungu ameamua kuzisahau kwasababu anazifuta kabisa kabisa na unabaki bila dhambi.. mimi dhambi zangu mtu akinikumbusha huwa nawaambia, MUNGU ALISHANISAMEHE, ALISHAZIFUTA, MIMI SINA DHAMBI, KAMA UNAZIKUMBUKA KAJADILIANE NA MUNGU HUKO, USIJADILIANE NA MIMI. Na huu ndio ukweli.
ISAYA 43:25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
Yoe.2:12-13 "Lakini sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza, RARUENI MIOYO YENU, WALA SI MAVAZI YENU; Kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira ni mwingi wa rehema; naye hughairi mabaya"
MIKA 7: 18 – 19. Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hashiki hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema. Atarejea na kutuhurumia; atayakanyaga maovu yetu, nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari.
Zaburi 103:11-13"Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao."
USHAURI WANGU KWENU: siku zote mshahara wa dhambi ni mauti, ila ukitubu Mungu anakupa uzima wa milele. Hivyo asiwepo mtu wa kuwavunja moyo, kwamba labda mmekuwa watenda dhambi sana hamtasamehewa, No. Mungu atawasamehe. Haijalishi umetenda dhambi gani, labda ukiondoa ile ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Tubu,rudi kwa Mungu, atakusamehe, atasahau dhambi zako, utakuwa kiumbe kipya. Kwa lugha nyingine, Mungu hana kisirani, hakasiriki milele, huwa anasamehe ukijirudi.
kwa bahati mbaya usichojua, hata waganga wenu wa kienyeji wanapotoa makafara yawe ya wanadamu au wanyama, wameiga kwa Mungu. Tabia ya Mungu ni kwamba, bila kumwagika damu hakuna ondoleo la dhambi. hata mnavyochukua kuku weupe au njia weupe kupeleka kwa mashehe wenu wanaouza madawa ya suna, ni makafara waliyoiga kwa Mungu. Shetani aliiba hii kitu kwa Mungu.Dhambi WAFANYE WATU WENGINE kisha DHAMBI ZENU azibebe mtu mwengine WEWE KUWEZA?
Kuna mijitu DUNIANI NI MIPUNGUANI SANA.yani MIPUNGUANI ya kutisha.
Ndio, unatakiwa kuokoka hata wewe hapo.Kuna kuokoka?
Mathayo 19:25-26Ndio, unatakiwa kuokoka hata wewe hapo.
wewe sijui ni padre au mchungaji, uwe unasoma mistari yote. anzia mstari wa 23.Mathayo 19:25-26
25 Wafuasi waliposikia hili walishangaa. Wakauliza, “Sasa ni nani ataweza kuokoka?”
26 Yesu akawatazama na kuwaambia, “Hili haliwezekani kwa wanadamu,”
sio watu wote ni wafuasi wa papa lakini ndugu. sisi wengine hata tukimkuta hapo mwenge anatembea wala hatustuki kama kuna mtu anapita, hatuhusu kabisa, ila tunamwombea kwa Mungu aokoke badala ya kufuata mapokeo ya dini, amwabudu Mungu wa kweli na wafuasi wake wote pia.
😁😁😁 Nacheka kama mazuri akili zenu ndogo sana,kila binadamu atabeba dhambi zake, mbona hamna sehemu iliyo andikwa MKIFANYA MAZURI ATABEBA MAZURI YENUkwa bahati mbaya usichojua, hata waganga wenu wa kienyeji wanapotoa makafara yawe ya wanadamu au wanyama, wameiga kwa Mungu. Tabia ya Mungu ni kwamba, bila kumwagika damu hakuna ondoleo la dhambi. hata mnavyochukua kuku weupe au njia weupe kupeleka kwa mashehe wenu wanaouza madawa ya suna, ni makafara waliyoiga kwa Mungu. Shetani aliiba hii kitu kwa Mungu.
Zamani hizo, kwenye desturi za wayahudi zote hata kabla mood hajazaliwa, walikuwa wanatoa makafara ya wanyama kwa kuteketeza ili wafunike dhambi walizozitenda, sasa swali likaja kwa wasio na wanyama watatoa kafara gani kwa dhambi zao, Mungu akawa ameweka mpango tangu awali kwamba, itabidi itolewe kafara moja tu yenye thamani kufuta (sio kufunika) dhambi za wanadamu wote. Nafsi ya Mungu ikavaa mwili akazaliwa kama Yesu, akafa kwa ajili ya kutoa kafara la Damu kwa dhambi za ulimwengu wote. amekufia hata wewe ili abebe dhambi zako kama utamruhusu, kama haumruhusu utazibeba mwenyewe ukahukumiwe nazo siku ya mwisho, wala hulazimishwi.
Huyu Yesu ni Mkuu kuliko mitume wote, kuliko hata mood ambaye amekufa na hajafufuka na hajawafia ninyi, alikufa kwa dhambi zake tu. unakaribishwa kwenye ukristo, huko uliko ni upotevuni ndio maana hauelewi kabisa hii hoja.