Ushauri kwa Wizara ya ardhi ili kupunguza migigoro ya ardhi

Ushauri kwa Wizara ya ardhi ili kupunguza migigoro ya ardhi

hassan123

New Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
3
Reaction score
1
Kumekuwepo na migogoro ya ardhi ambayo inatokana na wananchi kununua maeneo ambayo yameuzwa kwa watu wengine, kuuziwa maeneo yaliyotengwa kwa shughuli maalum (open spaces). Hali hii inatokana na ugumu wa wananchi kupata taarifa sahihi za umiliki wa maeneo hayo kupitia ofisi za ardhi, ambapo mnunuzi hulazimika kwenda ofisi za ardhi na nyaraka muuzaji ili kuthibitisha ikiwa nyaraka husika za muuzaji zinatambulika na wizara ya ardhi.

Hali hii imeleta mianya ya rushwa kwa maafisa ardhi kutaka kupewa chochote kitu ili kufanikisha zoezi tajwa la uhakiki wa nyaraka na pengine baadhi ya wananchi kulazimika kununua maeneo ambayo hawana uhakika wa umiliki wake na baadae kuingia katika migogoro.

Nashauri Wizara ya Ardhi pamoja na OR-TAMISEMI kuanzisha "portal" ya uhakiki wa maeneo yaliyopimwa ili wananchi waweze kupata baadhi ya taarifa za umiliki wa maeneo kupitia simu janja kwa kujaza taarifa wanazopewa na wauzaji wa maeneo kama vile majina ya mmiliki, coordinates za kiwanja n.k.

Vilevile ili kupunguza gharama za utengenezaji wa portal mpya, portal ya TAUSI inaweza kuongezwa dirisha maalum kwaajiki ya uhakiki wa uhakiki wa maeneo.

Portal kama hii imefanya kazi kwa weledi kwa Muhimili wa mahakama, ambapo mwananchi anaweza kumtambua wakili anayempa huduma za kisheria kujua kama amesasiliwa, amelipa ada ya mwaka husika au lah.

Wako katika "Upauaji wa Taifa"
Baba Naa.
 
Back
Top Bottom