Ushauri kwa zao langu la nyanya

Ushauri kwa zao langu la nyanya

Foxhunters

Senior Member
Joined
Nov 25, 2019
Posts
160
Reaction score
108
Wataalamu wa kilimo mnishauri,Nimelima nyanya Miche 5000 .Ina mwezi mmoja Toka nimeipanda mbegu nimetumia. Tomato mwanga.

Kuna changamoto imejitokeza majani kubadilika rangi .ngoja niambatanishe picha ,hali hii ilijitokeza baada ya kupilizia sumu aina ya power Cron, snow tiger ujazo wa 30mls/16litre.

Mborea ya kuyeyusha kwenye maji Master k. Vijiko vinne +dawa ya ukungu vijiko vinne. Yame athilika matuta manne kama Miche 160

IMG_20220905_173554_500.jpg
 
Nyanya inahitaji usafi ndugu. Zao lolote likizungukwa na magugu lazima libadili rangi achilia mbali magonjwa
 
1. Je unamwagilia maji ya kutosha? Kama hapana yawezekana ikawa ndio sababu.
2. Kama unamwagilia maji ya kutosha, je umeweka mbolea yenye madini ya calcium lini? Kama hujaweka jitahidi uweke mbolea ya CAN au yoyote yenye madini ya calcium.
3. Weka shamba lako katika hali ya usafi muda wote.
 
1. Je unamwagilia maji ya kutosha? Kama hapana yawezekana ikawa ndio sababu.

2. Kama unamwagilia maji ya kutosha, je umeweka mbolea yenye madini ya calcium lini? Kama hujaweka jitahidi uweke mbolea ya CAN au yoyote yenye madini ya calcium.
3. Weka shamba lako katika hali ya usafi muda wote.
1.Namwagilia maji kila baada ya siku Tano.
2.niliweka mborea ya kupandia bsiku saba baada ya kupandikiza nilichanganya yara otesha na yara winner kwa uwiano sawa. Kizibo cha chupa ya maji. Sasa hivi ni wiki ya tatu tangu nimeweka. Natarajia kuwekea mbolea ya yara liva nitrabor.
Naombeni ushauri hata kwa matumizi. Na madawa sahihi kwa shamba langu hili.
 
Wasi wasi wangu ni madawa nikiyotumia kupilizia. Kwa wakati mmja yaani kwenye lita 16 za maji . Mfano. Nilichanganya. Mls30. Za sumu ya power Cron, snow tiger, dawa ya ukungu vijiko vinne na mbolea ya majani master k vijiko vinne. Kulikuwa na unyevu mpk maji yalituama. Lakini ni eneo dogo matuta manne . Lakini. Maeneo mengine maendeleo ni mazuri
 

Attachments

  • IMG_20220905_173641_588.jpg
    IMG_20220905_173641_588.jpg
    863.6 KB · Views: 52
  • IMG_20220905_173931_725.jpg
    IMG_20220905_173931_725.jpg
    606.6 KB · Views: 51
Back
Top Bottom