Ushauri kwenu ACT Wazalendo, msifanye makosa yaliyofanywa na CHADEMA ya kuratibu maandamano na migomo. Jikiteni kwenye mikakati na mipango

Ushauri kwenu ACT Wazalendo, msifanye makosa yaliyofanywa na CHADEMA ya kuratibu maandamano na migomo. Jikiteni kwenye mikakati na mipango

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Ushauri huu ni mahususi kwa ajili ya ACT Wazalendo na vyama vingine vyenye muelekeo kama huu wa kuratibu maandamano na 'attention seeking' na nimetumia neno 'attention seeking' kwa sababu za ushiriki wao wa siasa za matukio ,kunapokuwa na tukio Chama kinaibuka na baadae kinapotea.

Kwa mazingira ya nchi yetu, ni vema vyama vikafahamu mambo yafuatayo badala ya kukimbillia siasa za matukio.

Kwanza, ieleweke kwamba mazingira ya siasa za Tanzania ni za kuhimiza amani na usalama. Kitendo Cha kuratibu maandamano, kinawakwaza sana wapenda amani. Maanadamano Mara nyingi kwa mtazamo wa wengi yanaambatana na matendo maovu na kutokana na hofu ya kufanyika uhalifu wakati wa maandamano wenye biashara huzifunga kwa muda. Mfano rahisi ni Kenya hapo, waandamaji waliharibu mali na kufanya uporaji wa kutisha.

Hivyo ,siasa za nchi zimejengwa katika misingi ya amani na usalama na hiki ndicho Wananchi wanatamani sana. Hali inaonesha kuwa maandamano hayajawahi kufanikiwa kuleta mabadiliko chanya bali ni maumivu tu.

Pili, Kila Jambo na wakati wake. Wengi wanaratibu maandamano ni wenye uelewa mdogo juu ya kanuni hii. Kanuni kubwa inayotumiwa na waandamaji ni kushinikiza hata Kama Sheria na utaratibu unakataa na wanatumia lugha 'tunataka'.

Katika utawala wa sheria, ni ngumu sana kumhakikishia muandamaji anachotaka. Hivyo bila hata maandamano, kwenye utawala wa sheria ni muda ndio kuamua. Maandamano ni kubariki uvunjifu wa taratibu zilizowekwa.

Tatu, ni vema vyama vijikite kwenye mipango na mikakati ya muda mrefu ambayo itawasaidia kujiimarisha. Kuratibu maandamano ni kusema kwamba Chama hakina malengo ya muda mrefu, kila tukio chama kinabeba na kwenda nalo. ACT ni Chama kidogo kwa umri hivyo kinatakiwa kujiimarisha zaidi kimkakati.

Nne, meza ya majadiliano ni bora zaidi kuliko maandamano. Kama tunaamini katika kutumia mabavu na kuacha maridhiano basi vina safari ndefu sana Kuzielewa siasa za Tanzania za sasa na kumuelewa Rais wetu. Mhe.Rais haamini katika migomo na maandamano ila katika majadiliano. Kuna njia nyingine nyingi za kufikisha ujumbe bila maandamano. Maandamano maana yake ni 'kujimwambafy'.

Kwa yeyote mpenda amani, suala la maandamano hawezi kukubaliana nalo kamwe na kitendo kilichofanywa na ngome ya vijana wa ACT-Wazalendo kimetusikitisha sana.

Natambua ACT bado ni kichanga na kinajaribu kila njia kuonekana, kukubalika lakini njia mnayotumia ya maandamano sio sahihi muda si mrefu kifo chenu kitatokea tena kibaya kuliko kile Cha CHADEMA.
 
Back
Top Bottom