Ushauri, Maoni na Msaada: Kwa wanaotaka kujilipua nje ya nchi kusaka maisha, kusoma na kuwekeza

Mkuu izo naomba ni host japo mtu 1 plzz kwenye awamu ya kwanza sitokuangusha
 
"....Tanzania ki uwezo bado ni changa, fursa za kutoka ni chache na hata changamoto ni nyingi. Huko kwa wenzetu fursa ni nyingi ndio maana imekuwa chanzo cha kuvuta wahamiaji wengi sana toka mataifa masikini."

Hapa ndio sikubaliani na wewe, nchi yetu ina fursa nyingi zaidi za kutoka kuliko huko unakokusema wewe! Ushaona huko nje biashara ya kuchajisha simu? kuingiza nyimbo kwenye simu? hivi utoke huku useme unataka kuwa mkulima wa kati au mkubwa utaweza kweli ukiwa US?

Narudia tena fursa zipo hapa hapa zimejaa tele kwani nchi yetu bado ni changa inakua..... ngoja ninywe maji kwanza maana.....

P.S Hauwezi kuwa tandale uwashauri watu namna ya kwenda kwa DJT
 
Acheni kuleta huu Ujinga kwenye Mjadala wa Mambo Serious
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Kila siku asubuhi na jioni lazima nipitie huu Uzi.
Kwa wale wa nje endeleeni kutupa link za kusoma,undergraduate na post graduate.
 
Mkuu izzo, baada ya kuwa mtu amesoma hii kozi ya English na kupata 70 or above, unahisi ni kitu/vitu gani muhimu unatakiwa kukamilisha?

Vijana wengi wanahangaika na scholarships (nikiwemo mwenyewe) pamoja na wengi kuwa na admission za vyuo wanavyotatajia kusoma.

Msaada wako ni muhimu sana kwani wengi wanadhani unaweza kusoma hizo kozi za english na bado wakakunyima scholarship.
 
Sasa huna sababu ya kwenda inje ya inchi passport KUBWA ya nn?kama ni suala la kwenda Kenya na Burundi.. Utapewa tu hata WILAYANI..ile ya karatasi
.ila passport kubwa sometimes materials yanakwisha...na watu wenye malengo na safari wanashindwa kusafiri lakini kuna watu mamilioni wameziweka passport chini ya MCHAGO.hawana malengo ya kusafiri..wao passport ni kama fashion tu...ndy maana lazima ueleze una mipango gani na passport... na sio kwl kwamba hata huko inchi zilizoendelea unapata tu kama KUNUNUWA VOCHA...hapana...huna sababu ya kuwa na passport kama huna safari... ID tu...inatosha kusafiri..ULAYA..kwa ULAYA..
 
Fursa za kufoji vyeti zipo lakini za kutoka kimaisha sahau

Jiulize kitu, hapo unapoishi unaweza kulima tuta ukapanda mchicha ukatengeneza hela yako ya kwanza. Na fursa ipo zaidi ukihitaji kutanua hii biashara (huu ni mfano tu). Sasa wewe nenda nje uone kama utaweza kuwa na hilo tuta tu la mchicha!!

Acheni kudanganyana, nenda nje kusoma rudi bongo fursa zimejaa tele hapa. Otherwise kama una utaalamu wako nenda nje ukaajiriwe, kumbuka technologia imesogea zaidi kule hivyo waajiriwa ni wachache. Ukitaka kabebe box, ila kumbuka muda utakaotumia kijana mwenzio anaweza kuongeza biashara yake ya mboga mboga hapa hapa akiisimamia vizuri by the time unarudi huna hata pa kuanzia, mwenzio anakunyoosha tu na greenhouses zake!!
 
Unalima tuta unamwagilia mkojo wako mwenyewe au mate? Unaweza kulima malori mangapi ya mchicha na unauza kwenye masoko gani hapa bongo? Huko shambani kuna barabara zakufikisha huo mchicha wako unakotaka kwenda?

Serikali yako imekuwekea mazingira mazuri yakwenda kuuza mchicha russia na nchi nyingine? Hukusikia msimu uliopita nyanya zilioza mashambani na zikawa malisho ya mbuzi na nguruwe?

Hata hao unaowasikia wako ulaya sikwamba bongo hawana vitega uchumi. Wapo wenye majumba wamepangisha, wapo wenye mashamba makubwa wanalima large scale agriculture sio tuta moja la mchicha uanze kutembeza na beseni mitaani. Wapo wengi wamekeza bongo, mitajo wameitoa mbele huko.

Kama ulifoji cheti huwezi kuwazia kusoma mbele, waache vijana wakapige shule mbele wakirudi sawa wakibaki hukohuko sawa tu.
 


Kunywa maji kidogo kwanza.....haujaona nimesema washaurini vijana wakasome mbele....ninachopinga ni kusema tu nataka niende mbele nikafanye kazi yoyote maana kule fursa ni nyingi kuliko huku! Mchicha was a metaphor....hebu nitajie mtanzania gani aliyeko nje anayefanya large scale agriculture huko nje? Nina mifano kadhaa ya watu wanaoexport mazao yao na kusambaza kwenye european markets, wanalimia hapa hapa bongo arusha na tanga huko. Anyways Akili za kuambiwa changanya na za kwako!
 
Ushauri mzuri sana ila nimesoma kama kuna website za watu wanatafuta wafanyakazi wa hiyari so naomba utumie muda wako hata utupe link maana mm binafs nimekuelewa sana[emoji106]
 
Its like u spoke by my voice ila ntakuja kujieleza na mimi kivyangu kwa herufi kubwa

Kwakweli nimejifunza mengi sana kupitia huu uzi heshima kwako muanziasha uzi na wachangiaji hai kama mkuu izzo, tokyo, chillah, kaka, kaveli and mkuu Daby ofcoz na wengine ambao sijawataja salute sana;
May God bless u guys maana naona kama ndoto zangu za mda mrefu zinaelekea kutimia

amsr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…