USHAURI: Maumivu ya kifua upande wa kulia (Chest side pain)

Jiggy El Jefe

Senior Member
Joined
Aug 10, 2017
Posts
143
Reaction score
170
Habari za Muda huu ndugu zangu.

Tusaidiane kidogo kwa mawazo au ushauri kwa yoyote mwenye ufahamu au uelewa wa jambo hili.

Kwenye kipindi cha mwezi ww tatu mwishoni nlikua najiskia maumivu upande wa kulia ww kifua yaliopanda mpaka shingoni, begani na kichwani kidogo upande huo uko wa kulia. Yalikua nayasikia nikivuta hewa kawaida (kupumua), kukohoa au muda mwingi nikiwa nimelala.

Nilienda hospital ya private, wakasema wanipime pneumonia, ila hakukua na dalili halisi, hivyo doctor akanishauri nitumie antibiotics za pneumonia, week moja baaae tatizo halikuisha, nikarud hospital nyingine, nikamuelezea daktari akanipa dawa za pink- ethromycin (Sina hakika na spelling). na sindano ya maumivu...wakat natumia maumiv yanaenda kama yanapungua ila dose ikiisha yapo palepale. Mara ya tatu nikaenda kupima H.pylori wakasema iko positive, hivyo nikapewa Heligo kit ya siku 7...wakat natumia tatizo linapotea ila ikiisha linarudi

Mara ya nne nikaenda hospital tena nikapigwa xray ya kifua, doctor akasema anaona kama moyo umetanuka kidogo, so niende kwa daktari maalum wa magonjwa ya moyo pengine hilo ndo tatizo.

Nilionana na daktar wa magonjwa ya moyo katika clinic yake, akanipima vipimo viwili, ECHO na ECG. na alinambia kua haoni tatizo linalohusiana na moyo, na pia nlimueleza kuhusu Hpylori kuwa positive last time nilivyopia, akaniuliza kama nna dalili za vidonda, nikamwambia sina...since sijawah sumbuliwa na tumbo ama hata nikila vyakula ambayo haviendani na vidonda sijawah kuumwa. Daktar akasema Kua positive haimaanishi una ulcers ila ye alisema anaona kama kifua kinabana upande mmoja, alinipa dawa nikatumia, tatizo likaisha kwa muda....ila sasa limerud tena kuna maumiv sana upande wa kulia wa kifua kama vile kuna kidonfa ndani au kama mtu aliegongwa na chuma eneo hilo...hasa nikiwa nimejilaza au kukohoa ama ata kupiga chafya.

Naombeni ushauri kwa yoyote mwenye ufahamu ama hata uelewa juu ya hili, tafadhali.
 
Pole mkuu Jiggy El Jefe. Sijajua mara ya mwisho ulipifanya ECHO na ECG ulipewa dawa gani exactly kwa jina. Ila kwa jinsi unavyoyaelezea maumivu unayoyapata inafanana na kitu kinaitwa ANGINA PECTORIS, ingawa mara nyingi maumivu huwa upande wa kushoto ila kwa baadhi ya watu inaweza kuwa upande wa kulia.
CHANZO
-Ukosefu wa damu katika eneo mojawapo la moyo kutokana na mishipa ya damu inayopeleka damu eneo hilo kufa/kusinyaa kupita kawaida.
Hii hupelekea maumivu kama vile mtu anachomwa na kitu chenye ncha kali/stubbed with a knife au kama mgandamizo fukani/pressing like.
Maumivu hayo huhisiwa yakisambaa/irradiating kuelekea eneo la shingo, shavu, mgongo, bega au mkono wa upande husika yalipoanzia.

Mara nyingi huanzishwa/aggrevated na shughuli/physical exhaustion kwasababu moyo unakosa damu ya kutosha eneo athirika hivyo tissue kufa na kupelekea maumivu hayo makali.
MSAADA/TIBA
Dawa zinazoweza kutanua mishipa ya damu iliyosinyaa, ie NITROGLYCERIN tablets, unaweka chini ya ulimi/sublingual, inayeyuka na kuwa absorbed/kufyonzwa.
Huwa inatumika unaposikia hayo maumivu tu, ie PRN based.
NB
Kama itaweza kuondoa maumivu yako ndani ya dakika tano, basi jua kuwa hilo ndilo tatizo lako, ukivuka dakika 15-20 bila kupata nafuu basi tatizo litakuwa lingine.
Jaribu hiyo dawa kisha uone nini matokeo mkuu.
 
Shukran sana Mkuu, Asante sana. Nitafanya hivyo. [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Hili tatizo ata mm ninalo ila mm Mara nying huchukua Kama dk 3 kuuma baada ya Hapo nakuwa Kama kawaida
 
Hata mm mkuu kuna muda nakua sisikii mpaka ntapofanya jambo linalogusa eneo husika moja kwa moja...mfano, kujikunja au kulala...Ila muda mwingi nkiwa nimekaa au kutembea huwa siskii...
 
Habari za Muda huu ndugu zangu.

Tusaidiane kidogo kwa mawazo au ushauri kwa yoyote mwenye ufahamu au uelewa wa jambo hili.

Kwenye kipindi cha mwezi ww tatu mwishoni nlikua najiskia maumivu upande wa kulia ww kifua yaliopanda mpaka shingoni, begani na kichwani kidogo upande huo uko wa kulia. Yalikua nayasikia nikivuta hewa kawaida (kupumua), kukohoa au muda mwingi nikiwa nimelala.

Nilienda hospital ya private, wakasema wanipime pneumonia, ila hakukua na dalili halisi, hivyo doctor akanishauri nitumie antibiotics za pneumonia, week moja baaae tatizo halikuisha, nikarud hospital nyingine, nikamuelezea daktari akanipa dawa za pink- ethromycin (Sina hakika na spelling). na sindano ya maumivu...wakat natumia maumiv yanaenda kama yanapungua ila dose ikiisha yapo palepale. Mara ya tatu nikaenda kupima H.pylori wakasema iko positive, hivyo nikapewa Heligo kit ya siku 7...wakat natumia tatizo linapotea ila ikiisha linarudi

Mara ya nne nikaenda hospital tena nikapigwa xray ya kifua, doctor akasema anaona kama moyo umetanuka kidogo, so niende kwa daktari maalum wa magonjwa ya moyo pengine hilo ndo tatizo.

Nilionana na daktar wa magonjwa ya moyo katika clinic yake, akanipima vipimo viwili, ECHO na ECG. na alinambia kua haoni tatizo linalohusiana na moyo, na pia nlimueleza kuhusu Hpylori kuwa positive last time nilivyopia, akaniuliza kama nna dalili za vidonda, nikamwambia sina...since sijawah sumbuliwa na tumbo ama hata nikila vyakula ambayo haviendani na vidonda sijawah kuumwa. Daktar akasema Kua positive haimaanishi una ulcers ila ye alisema anaona kama kifua kinabana upande mmoja, alinipa dawa nikatumia, tatizo likaisha kwa muda....ila sasa limerud tena kuna maumiv sana upande wa kulia wa kifua kama vile kuna kidonfa ndani au kama mtu aliegongwa na chuma eneo hilo...hasa nikiwa nimejilaza au kukohoa ama ata kupiga chafya.

Naombeni ushauri kwa yoyote mwenye ufahamu ama hata uelewa juu ya hili, tafadhali.

1. kama tungekigawa kifua katika sehemu tatu i.e Juu ya titi(supramammary),kwenye titi na chini ya titi(infra mammary),je wewe maumivu hayo unayasikia upande upi wa kulia?
2. Na je kabla ya hayo maumivu kuanza ulipata kikohozi maana kuna mahala nimeona unasema ukikohoa ndo unapata maumivu
maana yake una kikohozi ningependa kujua hicho kikohozi kilianza kabla ya hayo maumivu au vilinza vyote?
3.Ulienda hospitali wakasema wakupime pneumonia je ulifanya X-Ray?
4.Walikupa dawa za kutuliza pneumonia je unaweza kuzitaja?
5. kuna mahala unasema dawa za Eligo Kit za siku saba zilikutuliza...dawa za idonda vya tumbo minimum ni 14 days na kuna dawa moja unaendeleza mpaka hata week 8.
6.Daktari wako wa moyo alikupa dawa ambazo zilikutuliza...je unaweza kuzitaja hizi?
Maana mpaka hapo ushatulizwa na dawa za aina mbili za vidonda vya tumbo na zile za daktari wamoyo
7.je unavuta sigara au kuishi na chronic cigar smoker?
8.je,unafanya kazi ambako kuna uchafuzi wa hewa?
9.je uliapata ajali au kuangukia kitu kabla ya haya maumivu kuanza?
usijekua ume fracture rib moja wapo upande wa kulia

Maumivu upande wa kulia nisingefikiria sana moyo japo watabibu wana msemo kuwa "Diseases do not read books" wakimaanisha magonjwa hayata present kwako kama yalivoandikwa kwenye kitabu.
Japo maumivu yako yana taswira ambayo inafanana kabisa na tatizo la moyo kukosa oxygen japo maumivu yake mengi yanaweza kuwa ukifanya kazi au wakati mwingine ukiwa umepumzika/unstable angina na tatizo hili maumivu hayanaga uhusiano wowote na kupumua,kupiga chafya au kukohoa.
Ningeona hiyo ECG paper yako ningefurahi sana maana alokuona kama sio specialist wa moyo anaweza kui miss.
Japo ukirudia ECG kama tatizo ni lenyewe bado litaonekana maana halijaisha ila pia kuna kitu kinaitwa ECG Stress Test kinaweza kukuhusu.

Kuna tatizo jingine ambalo linaweza kuwa la mapafu au la moyo ambalo kwangu mimi nalipa asilimia kubwa zaidi kuliko hilo la kwanza lilotangulia,naomba kueleza kama ifuatavyo.
Ni vema kuzingatia hapa kwamba maumivu kuwa upande wa kulia naupa moyo kuwa na tatizo probability ndogo zaidi ila nayaunganisha magonjwa haya mawili kwa sasa maumbile ya moyo na mapafu yana kitu kinafanana.

Moyo na Mapafu siku zote viungo hivi viko kwenye Motion i.e moyo unavyo Pump damu unasinyaa na kutanuka kuzalisha mapigo ya moyo,au unapovuta na kutoa hewa nje mapafu upanda na kushuka....hivo basi kwa kuwa viungo hivi viko katika motion maumbile yao yamefanywa vifunikwe na na kiukuta kidogo au waweza kukiita utando mwepesi ambako katikaukuta huo na viungo hivyo kuna Lubricant ambayo inasaidia kuondoa friction/msuguano.

Hivo tatizo lolote mara nyingi Infection itakayoenda kwenye kiukuta hicho itapeleka ile Lubricant kuondoka hivo kuwepo msuguano kati ya kuta na kiungo hicho.

Hili tatizo litazarisha kitu kinaitwa Pleurisy kwa mapafu ambayo naipa silimia kubwa zaidi au Pericaditis kama ni upande wa moyo,AU yote yanaweza ku co exsist na kuzalisha kitu kinaitwa PLuera-Percardial Friction rub ambayo inakupa maumivu makali kwenye kifua pale unapokohoa,unapopumua au kupiga chafya sababu wakati huu mapafu na moyo yanakua kwenye motion kubwa zaidi.

mara nyingi kama ni Pleurisy itakua labda una tatizo kwenye mapafu e.g Pneumonia au una Occupational lung disease na ndo maana mwanzo nkaanza kwa kuuliza hayo maswali yangu nane.
Kama tatizo lipo kwenye moyo mara nyingi cause ni Viral infections na unatibiwa tu kwa anti-inflammatory agents na ukifanya ECG lazima iwe abnormal kwenye tatizo kama hili!

Labda ujibu kwanza hayo maswali ili kusaidia kutoa real picture!
 
Tafuta hiyo dawa ya kuchua ujipake.
IMG_20180407_162433.jpg
 
Nianze kwa kukupa pole ...

Kwa kweli ukisasa ndo unatuponza, mimi nilishaacha kabisa kutumia madawa ya hospitali kwa sababu nilibahatika kuonana na mfamasia mmoja - jambo alilonieleza lilinifungua akili.

Madawa mengi ya hospitali yanahairisha tatizo; hayamalizi tatizo moja kwa moja. Madawa yenye uwezo wa kumaliza tatizo moja kwa moja yana bei ghari kiasi kwamba wabongo wa kawaida hawawezi ku-afford. Mfano products za AIM global au Superlife.

Mimi nilichokifanya ni kuzama kwenye vitabu na kujisomea aina ya mimea inayotibu maradhi mbali mbali. Ukifika nyumbani kwangu, sikosi vitu vifuatavyo:-
Mbegu za mpapai, majani ya mlonge, tangawizi, mbegu za mlonge, alovera, rosela, mchaichai, kitunguu maji, kitunguu swaumu.
Naendelea kujisomea ili niweze kujua mimea mingi inayotibu.

Jibu la tatizo lako;
Majuzi tu hata mimi nilikuwa na tatizo la maumivu ya kifuani upande wa kulia. Maumivu hayo yalinisumbua sana hasa wakati wa usiku.Kitu nilichofanya ni kunywa rosela asubuhi na jioni. Siku mbili tu sikusikia tena maumivu hayo.
 
Hata mm mkuu kuna muda nakua sisikii mpaka ntapofanya jambo linalogusa eneo husika moja kwa moja...mfano, kujikunja au kulala...Ila muda mwingi nkiwa nimekaa au kutembea huwa siskii...
Hili tatizo naona Kama tunafanana ila m Bado sjaendaga hospital kwakuwa halijawa kubwa kivile ila Nahis Hapo badae litakuwa kubwa
 
1. kama tungekigawa kifua katika sehemu tatu i.e Juu ya titi(supramammary),kwenye titi na chini ya titi(infra mammary),je wewe maumivu hayo unayasikia upande upi wa kulia?
2. Na je kabla ya hayo maumivu kuanza ulipata kikohozi maana kuna mahala nimeona unasema ukikohoa ndo unapata maumivu
maana yake una kikohozi ningependa kujua hicho kikohozi kilianza kabla ya hayo maumivu au vilinza vyote?
3.Ulienda hospitali wakasema wakupime pneumonia je ulifanya X-Ray?
4.Walikupa dawa za kutuliza pneumonia je unaweza kuzitaja?
5. kuna mahala unasema dawa za Eligo Kit za siku saba zilikutuliza...dawa za idonda vya tumbo minimum ni 14 days na kuna dawa moja unaendeleza mpaka hata week 8.
6.Daktari wako wa moyo alikupa dawa ambazo zilikutuliza...je unaweza kuzitaja hizi?
Maana mpaka hapo ushatulizwa na dawa za aina mbili za vidonda vya tumbo na zile za daktari wamoyo
7.je unavuta sigara au kuishi na chronic cigar smoker?
8.je,unafanya kazi ambako kuna uchafuzi wa hewa?
9.je uliapata ajali au kuangukia kitu kabla ya haya maumivu kuanza?
usijekua ume fracture rib moja wapo upande wa kulia

Maumivu upande wa kulia nisingefikiria sana moyo japo watabibu wana msemo kuwa "Diseases do not read books" wakimaanisha magonjwa hayata present kwako kama yalivoandikwa kwenye kitabu.
Japo maumivu yako yana taswira ambayo inafanana kabisa na tatizo la moyo kukosa oxygen japo maumivu yake mengi yanaweza kuwa ukifanya kazi au wakati mwingine ukiwa umepumzika/unstable angina na tatizo hili maumivu hayanaga uhusiano wowote na kupumua,kupiga chafya au kukohoa.
Ningeona hiyo ECG paper yako ningefurahi sana maana alokuona kama sio specialist wa moyo anaweza kui miss.
Japo ukirudia ECG kama tatizo ni lenyewe bado litaonekana maana halijaisha ila pia kuna kitu kinaitwa ECG Stress Test kinaweza kukuhusu.

Kuna tatizo jingine ambalo linaweza kuwa la mapafu au la moyo ambalo kwangu mimi nalipa asilimia kubwa zaidi kuliko hilo la kwanza lilotangulia,naomba kueleza kama ifuatavyo.
Ni vema kuzingatia hapa kwamba maumivu kuwa upande wa kulia naupa moyo kuwa na tatizo probability ndogo zaidi ila nayaunganisha magonjwa haya mawili kwa sasa maumbile ya moyo na mapafu yana kitu kinafanana.

Moyo na Mapafu siku zote viungo hivi viko kwenye Motion i.e moyo unavyo Pump damu unasinyaa na kutanuka kuzalisha mapigo ya moyo,au unapovuta na kutoa hewa nje mapafu upanda na kushuka....hivo basi kwa kuwa viungo hivi viko katika motion maumbile yao yamefanywa vifunikwe na na kiukuta kidogo au waweza kukiita utando mwepesi ambako katikaukuta huo na viungo hivyo kuna Lubricant ambayo inasaidia kuondoa friction/msuguano.

Hivo tatizo lolote mara nyingi Infection itakayoenda kwenye kiukuta hicho itapeleka ile Lubricant kuondoka hivo kuwepo msuguano kati ya kuta na kiungo hicho.

Hili tatizo litazarisha kitu kinaitwa Pleurisy kwa mapafu ambayo naipa silimia kubwa zaidi au Pericaditis kama ni upande wa moyo,AU yote yanaweza ku co exsist na kuzalisha kitu kinaitwa PLuera-Percardial Friction rub ambayo inakupa maumivu makali kwenye kifua pale unapokohoa,unapopumua au kupiga chafya sababu wakati huu mapafu na moyo yanakua kwenye motion kubwa zaidi.

mara nyingi kama ni Pleurisy itakua labda una tatizo kwenye mapafu e.g Pneumonia au una Occupational lung disease na ndo maana mwanzo nkaanza kwa kuuliza hayo maswali yangu nane.
Kama tatizo lipo kwenye moyo mara nyingi cause ni Viral infections na unatibiwa tu kwa anti-inflammatory agents na ukifanya ECG lazima iwe abnormal kwenye tatizo kama hili!

Labda ujibu kwanza hayo maswali ili kusaidia kutoa real picture!
1. Maumivu yapo chini ya titi (infra mammary) la upande wa kulia, kias kwamba hata nikibonyeza panauma.
2.Kukohoa sio ugonjwa yaan nikijaribu tu kujikoholesha ili nipime maumiv...ila sikuwah kukohoa kama ugonjwa, nlikua nafanya kama nakohoa ndo nikawa naskia maumiv pia.
3.x-ray nilifanya, na doctor alisema moyo unaonekana kama umetanuka kidogo sana, ila baada ya ECG na ECHO, doctor wa moyo alisema moyo kwa size uliotanuka sio tatizo kubwa la kufanya kuwe na maumiv, na alishaur tu nikifanya mazoez litaisha hilo, ila yeye alisema anaona kama kifua kinabana upande huo, kama mtu alietumia sigara ama kufanya kazi kwenye mavumbi sana.
4.Dawa za pneumonia nazokumbuka walinipa tu Ethromycin kama skosei jina...na zingine zilikua antibiotic za rangi mbili(kijani na nyeupe) sizikumbuk jina.
5.Dawa za Heligokit nlitumia kabla ya kuonana na mtaalam wa moyo, ila nlivomaliza maumiv yalipogoma kutoka, ndio nkaonana na huyo mtaalam akaniuliza kama nna dalili za vidonda, nikamwambia hapana...akasema tatizo haliwez kua ni vidonda.
6. Dawa za daktar wa moyo zilikua dose tatu, naikumbuka moja iliitwa "carbamazepina" na ingine ilikua ya rangi mbili mfumo wa antibiotics zile kama amoxlyn
7. Nliwah kutumia sigara kipindi flani ila nilishaamua kuacha., maana sikufikia pia stage ya kutokushindwa kuacha.
8. Sifanyi kazi mazingira hayo wala ya mavumbi.
9.Sijawah kupata ajali wala kuumia upande huu mmoja...yalianzaga tu kiutan kama shingoni nkajua nimelala vibaya...nikawa nachua na dawa ila yanarudi ndo yakashuka ad kifuani... mpaka so sasa ni kifuani tu chini ya titi...Sio sehem nyingine tena.

Vipimo vya ECG na ECHO ni hivi:
IMG_20180810_154314_8.jpg
IMG_20180810_154353_4.jpg
 
Nianze kwa kukupa pole ...

Kwa kweli ukisasa ndo unatuponza, mimi nilishaacha kabisa kutumia madawa ya hospitali kwa sababu nilibahatika kuonana na mfamasia mmoja - jambo alilonieleza lilinifungua akili.

Madawa mengi ya hospitali yanahairisha tatizo; hayamalizi tatizo moja kwa moja. Madawa yenye uwezo wa kumaliza tatizo moja kwa moja yana bei ghari kiasi kwamba wabongo wa kawaida hawawezi ku-afford. Mfano products za AIM global au Superlife.

Mimi nilichokifanya ni kuzama kwenye vitabu na kujisomea aina ya mimea inayotibu maradhi mbali mbali. Ukifika nyumbani kwangu, sikosi vitu vifuatavyo:-
Mbegu za mpapai, majani ya mlonge, tangawizi, mbegu za mlonge, alovera, rosela, mchaichai, kitunguu maji, kitunguu swaumu.
Naendelea kujisomea ili niweze kujua mimea mingi inayotibu.

Jibu la tatizo lako;
Majuzi tu hata mimi nilikuwa na tatizo la maumivu ya kifuani upande wa kulia. Maumivu hayo yalinisumbua sana hasa wakati wa usiku.Kitu nilichofanya ni kunywa rosela asubuhi na jioni. Siku mbili tu sikusikia tena maumivu hayo.
Asante kwa ushauri mkuu, nitaufanyia kazi pia.
 
Au godoro lako bovu
Hahaha Hapana mkuu, nna uhakika nalo, liko vyema. eneo lenye maumiv ni sehem ndogo tu kwa ujumla...sidhan kama godoro pia lingeweza ku-attack eneo dogo kama hapa, kama lingekua bovu...
 
Mengine yote ngojera, fanya CT SCAN, Medicine imebadirika sasa hivi. mambo ya Orthodox medical practice or Apollo physician way of practice yameisha pitwa na wakati. ndomaana mnapewa dawa nyingi. Wenzetu nchi zilizo endelea Investigation ndo ina toa 100% ya diagnosis. na CT Scan ni kama basic investigation regarding any chest pain.
Mimi charles dotter ushauri wangu ndo huo
 
Ct scan kwa chest pain ambayo hujajua kama ni ya moyo au mapafu...hii ni kutoelewa maana ya CT scan labda!
Kila kipimo kina maeneo yake...hauwezi kuwa na tatizo la moyo ukafanya CT scan wakati kuna ECHO na ECG.
 
1. Maumivu yapo chini ya titi (infra mammary) la upande wa kulia, kias kwamba hata nikibonyeza panauma.
2.Kukohoa sio ugonjwa yaan nikijaribu tu kujikoholesha ili nipime maumiv...ila sikuwah kukohoa kama ugonjwa, nlikua nafanya kama nakohoa ndo nikawa naskia maumiv pia.
3.x-ray nilifanya, na doctor alisema moyo unaonekana kama umetanuka kidogo sana, ila baada ya ECG na ECHO, doctor wa moyo alisema moyo kwa size uliotanuka sio tatizo kubwa la kufanya kuwe na maumiv, na alishaur tu nikifanya mazoez litaisha hilo, ila yeye alisema anaona kama kifua kinabana upande huo, kama mtu alietumia sigara ama kufanya kazi kwenye mavumbi sana.
4.Dawa za pneumonia nazokumbuka walinipa tu Ethromycin kama skosei jina...na zingine zilikua antibiotic za rangi mbili(kijani na nyeupe) sizikumbuk jina.
5.Dawa za Heligokit nlitumia kabla ya kuonana na mtaalam wa moyo, ila nlivomaliza maumiv yalipogoma kutoka, ndio nkaonana na huyo mtaalam akaniuliza kama nna dalili za vidonda, nikamwambia hapana...akasema tatizo haliwez kua ni vidonda.
6. Dawa za daktar wa moyo zilikua dose tatu, naikumbuka moja iliitwa "carbamazepina" na ingine ilikua ya rangi mbili mfumo wa antibiotics zile kama amoxlyn
7. Nliwah kutumia sigara kipindi flani ila nilishaamua kuacha., maana sikufikia pia stage ya kutokushindwa kuacha.
8. Sifanyi kazi mazingira hayo wala ya mavumbi.
9.Sijawah kupata ajali wala kuumia upande huu mmoja...yalianzaga tu kiutan kama shingoni nkajua nimelala vibaya...nikawa nachua na dawa ila yanarudi ndo yakashuka ad kifuani... mpaka so sasa ni kifuani tu chini ya titi...Sio sehem nyingine tena.

Vipimo vya ECG na ECHO ni hivi:
View attachment 831976View attachment 831979

Safi sana mkuu umejibu vizuri maswali!
kilichonistua ni huyo mtaalamu wa moyo kukupa dawa kama Carbamezapine.
ECHO yake sio standard!

ila kama Xray na ECG zote zinaonesha moyo umetanuka si ajabu kuna kitu kinakusumbua kwenye moyo!

ECG ambayo tulitegemea iondoe mzizi wa fitina kama tatizo lina originate kwenye moyo umeiweka nusu yake.

labda nkuoneshe ECG paper inakua hivi na mawimbi fulani hivi kama hapa chini.

download.jpeg

vinginevyo ume fall kwenye mikono isiyo sahihi!
 
Back
Top Bottom