Ushauri: Maumivu ya kwenye joint za goti

Ushauri: Maumivu ya kwenye joint za goti

Joined
Nov 18, 2016
Posts
14
Reaction score
2
Habari zenu wakuu,

Takribani wiki moja sasa imepita nimekuwa nikikabiliwa na tatizo la maumivu ya magoti,hali hii imesabababishwa na mazoezi ya kukimbia kila siku asubuhi uwanjani katika jitihada za kutengeneza afya.

Naomba kupata ushauri kutoka kwa wataalamu na wenye uzoefu na hili jambo kunijuza,je kukimbia kunaweza kusababisha maumivu ya goti?

Je, nifanyeje niweze kupata tiba ya magoti ili niweze kuendelea na mazoezi asubuhi?

Hali hii imekuwa ikitokea mara kwa mara pale ninapoamua kuanza mazoezi asubuhi,kila ninapoanza mazoezi baada ya wiki 2 nalazimika kuacha kutokana na maumivu ninayoyapata kwenye viunga vya goti.
 
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu.
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Unakimbia kwenye sehemu ngumu au viatu unavyotumia havifai kukimbilia. Angalia soli za viatu vyako.
 
Nakimbia kuzunguka uwanja wa mpira,natumia raba za kawaida (wanaziita simple zina soli ya kawaida). Huenda ikawa ni sababu ya maumivu ya magoti...........Je nitumie raba zenye soli ya aina gani,na sehemu gani ambayo napaswa kufanyia mazoezi ya kukimbia?
 
Habari zenu wakuu...
Takribani wiki moja sasa imepita nimekuwa nikikabiliwa na tatizo la maumivu ya magoti,hali hii imesabababishwa na mazoezi ya kukimbia kila siku asubuhi uwanjani katika jitihada za kutengeneza afya.Naomba kupata ushauri kutoka kwa wataalamu na wenye uzoefu na hili jambo kunijuza,je kukimbia kunaweza kusababisha maumivu ya goti?je nifanyeje niweze kupata tiba ya magoti ili niweze kuendelea na mazoezi asubuhi?
Hali hii imekua ikitokea mara kwa mara pale ninapoamua kuanza mazoezi asubuhi,kila ninapoanza mazoez baada ya wiki 2 nalazimika kuacha kutokana na maumivu ninayoyapata kwenye viunga vya goti.
Kula matango sana na bamia nipe majibu baada ya week, punguza kugegeda kama ulikuwa unagonga tatu kwa siku piga kamoja tu
 
Nakimbia kuzunguka uwanja wa mpira,natumia raba za kawaida (wanaziita simple zina soli ya kawaida). Huenda ikawa ni sababu ya maumivu ya magoti...........Je nitumie raba zenye soli ya aina gani,na sehemu gani ambayo napaswa kufanyia mazoezi ya kukimbia?
Kuna raba maalum za kukimbilia ambazo zina damp effect unapokimbia hasa ukiwa na maumivu ya magoti. Uwanja wa mpira ni mgumu?
 
NKamuone daktari wa mifupa ufanye vipimo. Labda umeishiwa vilainishi.
 
Habari zenu wakuu,

Takribani wiki moja sasa imepita nimekuwa nikikabiliwa na tatizo la maumivu ya magoti,hali hii imesabababishwa na mazoezi ya kukimbia kila siku asubuhi uwanjani katika jitihada za kutengeneza afya.

Naomba kupata ushauri kutoka kwa wataalamu na wenye uzoefu na hili jambo kunijuza,je kukimbia kunaweza kusababisha maumivu ya goti?

Je, nifanyeje niweze kupata tiba ya magoti ili niweze kuendelea na mazoezi asubuhi?

Hali hii imekuwa ikitokea mara kwa mara pale ninapoamua kuanza mazoezi asubuhi,kila ninapoanza mazoezi baada ya wiki 2 nalazimika kuacha kutokana na maumivu ninayoyapata kwenye viunga vya goti.

Mkuu umetibiwa kwa dawa gani?? Nami nina shida kama hiyo.
 
Mkuu sijapata dawa,bado natafuta suluhisho.Tatizo hilo limenifanya nipunguze zoezi la kukimbia asubuhi
 
Aseee kama ni kijana ambaye bado unamalengo yako ushauri wangu mwepesi tu.....punguza sex na kula bamia walau Mara mbili kwa siku(fanya kama wiki mbili) au tafuta kaa ule.....kwa hosptali waeza fanyiwa operation ya goti
 
Sawa chief nadhani ntaanza dozi ya bamia very soon niweze kurejea kwenye ulingo wa mazoezi ili kuijenga vyema afya yangu
 
Sawa chief nadhani ntaanza dozi ya bamia very soon niweze kurejea kwenye ulingo wa mazoezi ili kuijenga vyema afya yangu
Sio kuwaza kurudi mazoezini haraka.., la hasha.,kwa mwanamichezo ungekuwa nje ya mchezo hata miezi miwili au mitatu(kibongo bongo)....ila ukitaka kuona ni jinsi gani ungetakiwa kutulia pasipo kulazimisha mazoezi....mtafute DIABY yule wa arsenal ,nadhani kwa sasa yupo ufaransa alikaa zaidi ya miaka tatizo ni magoti tu...,huku TZ kwetu dawa ya haraka ni Bamia au virudisha vilainishi mguuni..,bado sijasema yawezekana magoti yana maji..,n.k ila cha msingi usiharakishe kuwahi mazoezi ,kula bamia kama nilivyosema ila jizuie mazoezi haswa haswa wanaziita squat(kuulazimisha kukunja goti hadi mwisho ) ukilazimisha utajitafutia kilema

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru kwa ushauri wenu wakuu,naufanyia kazi ntawapa feedback baada ya muda flani
 
Back
Top Bottom