Mzee Mwafrika
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 203
- 104
Nimemaliza mwaka wa kwanza medicine ila ninaweza chagua kuendelea mwaka wa pili na Medicine au Dental Surgery.MD ni miaka saba na Dental Surgery ni miaka 5(Sio Tanzania tafadhali).Naombeni ushauri;niendelee na Medicine au nirukie Dental Surgery mwaka wa pili?Izingatiwe soko,muda na mengineyo.(Nakumbusha hii haiwezekani Tanzania ila inawezekana nilipo mimi kutokana na mfumo wa elimu wa huku)
-Hujasema uko wapi
-Hujasema unataka kufanya kazi wapi
-Hujasema kinachokusukuma kufanya kazi ni nini, pesa, huduma au hujui?
-Unataka tuzingatie soko na muda, soko la wapi? Uko uliko? Tutalizingatiaje bila ya kulijua?
Kwa ujumla hujatoa habari za kutosha kumfanya mtu anayeelewa vihusika kwa undani kukupa ushauri mzuri, seuze wasiojua lolote kuhusu hii sekta ambao ndio wengi hapa bodini.
Kwani wakati unaanza hukulijua hilo??
Ulienda huko kusoma kitu gani,MD a DS au kitu kingine tofauti??
Ulienda ukijua utasoma kwa muda gani??
Kama huna majibu ya maswali hayo basi ushauri ni huu
"Huo muda usikutishe kabisa maana kama utachukua MD hata hautajua jinsi muda utakavyokuwa unaenda.Na kama utarudi Bongo basi chukua hiyo MD,DS haina dili Bongo ukilinganisha na MD,na nina hakika hata hapo ulipo na sehemu yeyote ile DS haiwezi kuipiku MD,so acha haraka soma taratibu tu utafika"
Na nakukumbusha kuwa TZ watu wa MD na DS huwa wanaanza pamoja then wana-separate njiani.