Mpe nafasi nyingine, ujue huku sekondari kuna wengine wanafaulu kwasababu wamezoea kusimamiwa na wamebanwa uhuru.
Wakifika chuoni wanakuwa washamba wa uhuru na hawasimamiwi kama sekondari, huu mda sio ajabu kukuta hata aliefaulu sekondari anafeli, Kuna baadhi ya watu lazima waipitie hii stage ili waondoe ushamba wa uhuru.
nilikuwa na dada yangu nae alikuwa hivyo, alipofika chuoni alikuwa mshamba wa uhuru akaharibu.
Mzee alishakataa kumsomesha ila akapewa ushauri akaufata na ukazaa matunda.
Baada ya kudisco, sista alikaa nyumbani mwaka mzima ajitafakari, hapo nyumbani aliishi maisha ya kupitishwa msoto kwa maksudi, mzee alikuwa hampi hela, kila siku kuwahi kuamka alfajiri kufanya usafi na kuandaa chai, hakuna kutoka toka ovyo. ulikuwa msoto mkali sana kwa sista.
sista alijutia sana makosa, mwaka ujao kwenye maombi ya vyuo ndio mzee akamruhusu kwenda chuo, aliporudi chuoni akapewa onyo hio ni nafasi ya mwisho, chuoni aliweza kubalance maisha ya uhuru na kilichompeleka na alifaulu vizuri tu na Sasa ana ajira.