Ushauri: Michuano ya Azam Sports Federation Cup ifutwe

Hadrianus

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2020
Posts
2,112
Reaction score
5,229
Habari wanamichezo.

Kwa miaka ya hivi karibuni tangu kurejea kwa michuano hii ya F.A. Tanzania bara, nimeiona haina tija kwa soka la Tanzania bara sana imekaa kufaidisha kikundi cha watu wachache.

Sababu kubwa inayonifanya niamini hii michuano ipo "kimchongo" zaidi ni upangaji wa droo wa mechi hizi, umekua upangaji wa "kimkakati" zaidi kuliko uhalisia.

Hivyo napendekeza michuano hii ifutwe kwasababu kubwa moja, anakua anatafutwa Bingwa ambaye anajiweza kiuchumi ambaye atawakilisha taifa katika michuano ya vilabu Afrika hivyo kupelekea droo ipangwe kwa tahadhari ya kuziondoa mapema timu ndogo (dhaifu kiuchumi).

 
Thibitisha....
Ongea fact na sio hisia zako.
Unaweza kuweka vielelezo na ushahidi wa hicho ulichokiandika, utakuwa umewasuta sana waandaaji, watajiuzulu wenyewe
 
Kwahiyo ifutwe baada ya Yanga kukosa kombe? Kumbe mmeumia sana
Hoja ya mleta mada ni dhaifu lakini wewe ni marehemu kabisa. Umesababisha mleta mada aonekane kaleta kitu cha maana kumbe cha kawaida Sana.
 
Kwani zinatolewa na mapanga? Kwa hoja hizi Namungo, Yanga, Mtibwa na Biashara wasingehudhuria huko na badala yake Simba tu ambae yupo vizuri kiuchumi na soka. Naungana mkono na waliosema hoja hii ni mufilisi,dhaifu na imetolewa toka shimo la kunyea na sio ubongo.
 
Kufutwa hapana,labda utoe mapendekezo nini koboreshwe mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…