Benjamin mnyawa Sylver
New Member
- Jul 16, 2021
- 2
- 2
Moja ya sifa za kupata mikopo hii kikundi kinapaswa kuwa na watu kwanzia 10 na kuendelea, na kwa wenye ulemavu wanaanzia watano na kuendelea.
Hoja yangu ni kwamba, kwa upande wa vijana hii sifa imeangalia kundi la vijana ambao hawana elimu kwa mapana kwasababu ni rahisi mno kwa vijana waliokaa vijiweni bila kazi kuungana na kukubaliana kufanya shughuli za ujasiriamali kama kilimo, ufugaji nakadhalika.
Kuna kundi kubwa la vijana ambalo linaachwa nyuma na mikopo hii kwa kukosa sifa au kupitia changamoto nyingi kwa mfano.
1. Vijana wenye shughuli za kibunifu inawawia vijana wengi ugumu wa kupata mikopo hiyo kwasababu ni vigumu kwa vijana 10 kuwa na ubunifu wa aina moja au kipaji kimoja hivyo kukubaliana kufanya kitu kimoja.
2. Vijana ambao wana taaluma mbalimbali, katika jamii zetu kuna kundi kubwa la vijana ambao wanahitimu masomo ya taaluma mbalimbali mfano ualimu, utaalam wa maabara, uhasibu, fundi wa makenika, afisa ugavi nk.
Inakua ni vigumu kukuta kundi la vijana 10 wa mtaa/ sehemu moja wana taaluma moja hivyo kuwa na wazo la biashara au ubunifu linalofanana, hivyo kutofautiana na taaluma hizo ni vigumu kwa vijana hawa kuunda kikundi cha biashara na kuchukua mikopo hii.
Hivyo basi nashauri ufanyike upembuzi yakinifu ila kuwasaidia vijana hawa na wengine wanaopitia changamoto kama hizi ili waweze kunufaika na mikopo hii ya bila riba.
Ahsante