Ushauri: Milioni 5 ni kiwango ambacho hunisumbua kukivuka, Nifanyeje ili nivuke hii hatua?

Shozylin

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
341
Reaction score
699
Wasalaaam ndugu Wana jf

Sjui ni kwangu tu au na kwako ipo hivi yaani kuna kiwango flani Cha pesa kukivuka kinakua na vizuizi vingi Sana mwisho wa siku unajikuta unacheza mule mule tu, sjui shida hua ni Nini.?

Kwa upande wangu Mimi mwaka 2021 nilikua na milion 5 biashara iliyo nipatia hiyo pesa ni hii ya huduma za kifedha.

Visanga vikaanza:

Kuna siku nilikosea kutuma pesa kimakosa sh 600,000 skubahatisha kuokoa hata Mia,

maumivu ya kupoteza wakati hayajaisha wezi wakaja kubomoa flame na kuiba mpaka mwisho wa siku nikajikuta Nina 3.8

Nikachukua maamuzi ya kutoka eneo Hilo kwenda kutafuta changamoto mikoa mingine japo flame niliacha chini ya uangalizi wnagu ili nikiferi kule nirudi, na nikaferi kweli

Mwaka Jana mwezi wezi wa 9 nikarudi nipo hoi nimepauka kuanzia muonekano mpaka uchumi, nimepambana kujiimalisha hatimaye nimefika kiwango nilicho kua nacho awali Cha 5.ml kinatimia mwezi huu.

Nimekua mtu wa kutafakari namna ya kuvuka kiwango, mawazo mengine yanambia nifunguo biashara nyingine, ila aina ya biashara ndo sjapata kwanza ninahofu ya kupoteza hiki kidogo nilicho kusanya.

Mawazo mengine yananambia nitunze akiba tu naishia kuwaza ntatunza mpaka lini wakati nataka kutanuka ki biashara.?

Umewahi kukutana na situation Kama hii na uliivukaje.?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa nakutana na hali kama yako. Njia mojawap nyepesi, tafuta supplier wakubwa wanakuuzia bidhaa,na unaowaamini, lipia bidhaa in advance ,chukua risiti zako zitunze kwenye email.

Automatically mzunguko wa bishara utakuwa hapo umekuwa na akiba imekua. Ukihitaji cash, unakusanya mauzo kwa muda bila kuagiza bidhaa mpya.

By the way, unatoka kuziona milioni 5 cash kwa akaunti ili iweje? Ndio mwanzo wa kwenda kuwekeza Kalynda au kwa wale walima Vanilla wa mchongo.
 
Tatizo bado nafanya biashara ile ile huduma za kifedha mkuu. Siuzi bidhaa

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa nakutana na hali kama yako. Njia mojawap nyepesi, tafuta supplier wakubwa wanakuuzia bidhaa,na unaowaamini, lipia bidhaa in advance ,chukua risiti zako zitunze kwenye email.

Automatically mzunguko wa bishara utakuwa hapo umekuwa na akiba imekua. Ukihitaji cash, unakusanya mauzo kwa muda bila kuagiza bidhaa mpya.

By the way, unatoka kuziona milioni 5 cash kwa akaunti ili iweje? Ndio mwanzo wa kwenda kuwekeza Kalynda au kwa wale walima Vanilla wa mchongo.
Mkuu ulikuwa kwenye mawazo yangu. NAKAZIA HII COMMENT
 
Mawazo mengine yananambia nitunze akiba tu naishia kuwaza ntatunza mpaka lini wakati nataka kutanuka ki biashara.?

Umewahi kukutana na situation Kama hii na uliivukaje.?
Nunua simu aina ya Nokia 105
  • Bei ya jumla ni TZS 15,000 hadi 20,000
  • Kwa kuanzia nunua simu za TZS. 500,000 ( laki Tano) | Yes, Tunajaribu biashara kwanza kabla ya kuweka mtaji mkubwa
Mtaji ukikuwa utaongeza simu za zingine na ikiwezekana utaagiza ambako wengine huziagiza kwa jumla na sio kupitia tena kwa mdau.

Bei ya wewe kuziuza hapo hapo kwenye kibanda chako:
  • Bei ya kuanzia ni TZS. 45,000
  • Bei yako ya mwisho ya kuuza isiwe chini ya TZS. 30,000 | Itategemea na mnunuzi ambavyo analalama kupunguziwa bei ( hivi visimu mikoani huuuzwa kati ya 45,000 hadi 60,000)

Wapi utazipata hizi simu:
- Anza kwa kuchukua kwa huyu mwana JF | Kama Unamtaji Kuanzia Laki Moja Fanya Biashara Hii

Uzuri wa biashara hii ya simu | Fedha yako haipotei
 
Back
Top Bottom