Ushauri: Mimi mwajiriwa Serikalini, nataka nichukue mkopo (kwa kutumia ajira yangu) kisha niache kazi

Ushauri: Mimi mwajiriwa Serikalini, nataka nichukue mkopo (kwa kutumia ajira yangu) kisha niache kazi

Kuna opportunity nimeiona mahali.
Nishaifanyia intensive analysis na kuona potential yake (actually I want to take a Risk)

Tatizo nakosa vitu viwili, muda na mtaji. Ni muajiriwa serikalini na mtaji wangu bado mdogo.

Nimefikiria nichukue Mkopo taasisi yoyote ya fedha (kwa kigezo kuwa watakua wananikata kwenye mshahara) kisha niwekeze resource zote kwenye hiyo opportunity.

Pasingekua na figisu kwenye Mifuko ya pension ningeacha Kazi kisha nikachukua mafao yangu (kwa sasa yamefika almost 6 Milioni) nikatembea mbele kiroho safi.

Wakuu wangu nishaurini:
Nikisema nichukue mkopo paaap kwa kutumia ajira yangu (Mkopo nahitaji ni 5 Milioni tu) then niache kazi next month Je watanitafuta wanikamate wanipeleke mahakamani ama Makato yao watachukua kwenye Pension Fund yangu na hawatashughulika namie.

Hivi unapoacha kazi mwajiri akakuta unadaiwa Mkopo na taasisi ya fedha inakuaje hapo.

Mdogo wenu CCNP
Haya mambo si ya kuleta humu
Omba ushaur kwa marafiki lkin sio humu
 
Msimpotoshe mwenzenu hakuna mahusiano ya mkopo na mafao yako...japokuwa ukifanya uhalifu ama chochote kinyume na taratibu na ajira yako mwajiri na mamlaka zingine za kisheria zitapiga nyundo malipo yako yasifanyike maana mwisho wa siku lazima uende ukaweke sawa kwa mwajiri lakini utatuhumiwa kwa kosa la wizi endapo utapatikana (Mwajiri atawajibika kama mdhamini wako lakini kosa lipo pale pale)
Ni mtizamo wake huo
 
Jamaa chai nyingi. Kwanza unafanya hata wadau wamuone ONTARIO kuwa ni tapeli! Kwanza hiyo GPA kwa pale UD Engineering haipo. Pili kama ulipata tatu kisha ukaenda nje ya UD kusomea Engineering pia ni uzushi! Mzushimzushi mjinga fulani hivi mwenye utapeli wa kitoto unawaza juu ya 5M unajiita mhandisi... Wewe ni wa kuchapa makofi mshenzi wee!
 
Nakushauri usiache kazi maana hata mtaji wenyewe wa biashara ni wa kuungaunga ikiwemo utapeli unaotaka kuufanya wa kuchukua mkopo kwa kutumia ajira yako ya sasa. Wanaoacha kazi hujipanga kwanza. Hawaendi kichwa kichwa kama unavyotaka kufanya wewe. Tafakari!
 
Hahaha vipi forex ushaacha baada ya kutapeliwa???
Ontario keshabeba chake
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] so kumbe Ontario alikuwa tapeli jamani bongo nyosoa kweli
 
Kwani anaiba au anakopa ? kumbuka pesa yake ya pension ndio itakayolipa mkopo
Huo ni wizi kiongozi ksb hata hayo mafao unayoyasema sheria au mifuko husika hairuhusu bank kwenda kuchukua kisa mteja kadefault...unakopa ksb mshahara wake ndo unamsecure na siyo mafao labda akakope kwenye mifuko husika...
 
MKUU, HV UNASHNDWAJE KUSAVE M.5? AU MSHAHARA WAKO SH. NGAPI? KUWA MVUMILIVU, AMUA LEO KUSAVE HATA LAKI 3 KWA MWEZI, KUWA MBAHILI NDANI YA MIAKA MIWILI UTAKUWA NA M.6

USIKOPI LIFESTYLE
 
Mkuu ama kweli vyuma vimekaza, yaani uache kazi kwa ajili ya 5 m? Shame on you dude! Lakini mmeshauri kama vyuma vimekaza wekeni grease!
ndo grease yenyewe hiyo anataka kuweka😀😀😀😀
 
Huo ni wizi kiongozi ksb hata hayo mafao unayoyasema sheria au mifuko husika hairuhusu bank kwenda kuchukua kisa mteja kadefault...unakopa ksb mshahara wake ndo unamsecure na siyo mafao labda akakope kwenye mifuko husika...
Kweli mkuu huo ni wizi kama wizi mwingine ila hii mifuko haipo fair kabisa, yaani mijamaa ya mjengoni pale Dodoma wanakopa mpaka 200 million alafu sie wanachama wanatutosa
 
Wewe chukua hiyo pesa hakuna chanani atakaye kufuatilia wala nini mimi binafsi nililamba mnb bank nikaacha kazi nikaanza biashara zangu binafsi hakuna aliyewahi kunifualilia na mambo yangu yanakwenda
 
Sasa ndo akaibe bank? maisha huhitaji kulazimisha sana mkuu..hapo ni kosa kama kosa lingine kwa kuwa mwajiri lazima amdhamini na ili uache kazi kuna taratibu za kufuata ikiwemo kuandika notisi ya mwezi ama masaa 24 na mwajiri wako akubali...kama una deni atakubali ili kabla ya kusaini exit form na taratibu zingine atakutaka uweke sawa mambo yako ikiwa pamoja na kulipa madeni na ku-handle over mali za ofisi n.k ndipo anaposaini kuondoka (mpaka hapo ujiulize atafanyaje ili atoke kwa mwajiri vinginevyo atatuhumiwa kwa makosa mawili ya kukimbia mkopo bank na kutoroka kazini maana hawezi kuacha kazi kienyeji na hakuna mwajiri atakubali wakati ana mkopo)
Naomba ufafanuzi inawekana uchukua mkopo mkoa huu alafu biashara ukafanyie mkoa mwingine?,
 
Naomba ufafanuzi inawekana uchukua mkopo mkoa huu alafu biashara ukafanyie mkoa mwingine?,
Sidhani kwa utawala huu wa JPM labda kwa investment zile kubwa kubwa za makampuni ambayo unakuta yana branch sehemu mbalimbali lakini kwa sie walalahoi lazima bank ya mkoa husika itoe mkopo ili waweze kukufuatilia vizuri...unless kama unachukua mkopo wa wafanyakazi hapo unaweza ukawekeza mkoa mwingne maana dhamana ni ajira yako na mwajiri wako
 
Nakumbuka jamaa yangu mmoja hivi alikuwa mwajiriwa serikalini basi alipokuja mtaani kipindi cha likizo akakuta vijana wenzie wanapiga pesa balaa wana magari nk, jamaa akapagawa akaenda kwa mzee kuomba ushauri ili aache kazi arudi uraini kupambana Kama wenzake

Mzee akamwambia mwanangu Fanya mambo yote Usiache kazi kikubwa malengo na mipango ukiwa na malengo na mipango gari, nyumba nk utapata japo si kwa haraka kama wenzako hawa unao waona wewe utachelewa ila ukikipata basi uhakika hakikutoki tena hata kama ulikipata kwa njia ya mkopo wewe si mtumishi wa umma basi nenda kapige kazi

Hawa wenzio mtaani unaona wana magari, nyumba nk hizo pesa ni Siri zao ambazo kamwe hawawezi kuambia wengine wana mikopo bank usishangae unaenda ukija kurudi unakuta mtu nyumba hana gari hana biashara hana kakimbia mjini hivyo nenda Kafanye kazi kuwa na malengo tu

Anaendelea kusema mzee unajua watumishi wa umma mnadanganyana Sana kuhusu maendeleo

Mfano mnambiana ukaichukue mkopo ukajengea utaibika sasa nauliza utaibikaje ikiwa kipato chako ni mshahara hivyo tunategemea kuona maendeleo yako kutoka katika huo mshahara wewe si Mfanya biashara ambaye ukikopa basi ipo siku utakosa marejesho matokeo yake mnakopa naaanza biashara hatimae biashara zina washinda hapo ndio naaanza kuchukia kazi maana ulikopa ufanye biashara hatimae biashara huna, pesa huna Kitu cha kukufariji huna

Mzee akaongea mengi Sana ila alichosisitiza malengo na mipango akasema

Mfano kijana kajiliwa leo kaa kazini miezi mitatu bado ajajijenga ndani Mfano fenicha nk, anachukua mkopo ananunua gari, au anajenga nyumba hapo hata radio, kitanda hana

Mzee akasisitiza maisha ni hatua usitake ufanye kazi miaka mitatu uwe na nyumba gari ni vigumu pengine uwe mwizi
 
Back
Top Bottom