Kachelenga
Member
- Sep 11, 2012
- 26
- 6
Naomba ushauri wana jamii,mimi nimeoa mke miezi 7 iliyopita,ndoa ya kiserikali.Mimi na mke wangu tunaishi mikoa tofauti kutokana na mazingira ya kikazi,ndoa nilikwenda kufunga nae ktk mkoa anaefanyia kazi yeye,Baada ya kufunga nae ndoa ya KISERIKALI,mm nililudi ktk mkoa ninaoishi na kumuacha yeye huko ktk mkoa anakofanyia kazi ambako ndiko tulipofunga hiyo ndoa ya Kiserikali.Cha ajabu baada ya kufika ktk mkoa ninaoishi!mke wangu hakakata mawasiliano mimi na hukutaka tena kuwasiliana nami,nikimpigia simu hapokei,sms hazijibu,baadae niliamua kumtumia sms za kumlaumu,hizo alizijibu kwa malumbano,Baada ya muda,akaniambia hanitaki,nisiwasiliane nae tena!nilipomwambia ww ni mke wangu,alisema ndoa haitambui!.Nilipoendelea kumfuatilia,alidai tuvunje ndoa na akaniambia mm niende mahakamani nikatengue ndoa,mm nilikataa na kumwambia yeye ambae haitaki ndoa ndio aende mahakamani,alikataa na kudai niachane nae na nisimfuatefuate.je wana jamii ktk hali kama hii nifanyenini jamani wenzangu na mke nampenda au kama itashindikana kuwa nae taratibu zipi za kufuata??