Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Hii gari haina complications kabisa kwa maelezo ya mtaalamu mmoja mwenye uzoefu wa hii gari kwa miaka mingi.
Anasema hii gari akienda kufanya service ya engine oil. Huwa hahangaiki kuulizia oil gani n.k. anasema ni oil ambayo kwa siku hiyo itapatikana hapo garage ndo itawekwa na kagari wala hakana tatizo nayo.
Hapo tena ni mpaka miaka kadhaa akija kumbushwa na mafundi kuwa sasa abadili oil ndo anabadili. Anasema ni kagari ambako unaweka mafuta kituo chochote hata kama yamechanganyika kidogo na ...katapiga chafya mbili tatu then katakubaliana na hali yako.
Kuhusu spares anasema zipo nyingi tu na sometimes ni kuangalia kama size yake ina fit na kufunga. Basi ikikubali na kenyewe kanakubaliana nayo. Pia kanakubali barabara karibia zote ili mradi kaweze tu kupita basi.
Haka kagari TOYOTA VITZ old model ndo Kagari kanakofaa kwa mazingira ya Kitanzania.