Ushauri: Mpenzi wake anaumwa lakini hospitali hawaoni ugonjwa wowote, achukue hatua gani?

Ushauri: Mpenzi wake anaumwa lakini hospitali hawaoni ugonjwa wowote, achukue hatua gani?

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
878
Reaction score
2,014
Nina rafiki ambaye jana kufunguka kile alichokuwa anapitia kwenye mahusiano yake, ana mwanamke ambaye anaishi naye huu mwaka wa pili sasa ila mambo yamebadilika tangu mwezi November mwaka jana; mwanamke anaumwa magonjwa ambayo hospitali hayaonekani, anakosa hamu ya kula, kapungua uzito, hedhi yake imekua irregular sana, usiku halali vizuri anaona kama pumzi inambana.

Mpaka sasa vimepimwa vipimo vingi na ugonjwa hauonekani (kuanzia kuangalia matatizo ya tezi mpaka cholesterol).

Jamaa yangu anakaribia kuchanganyikiwa
 
Bony Mwaitege once sang ...njoo ufanyiwe maombi...

Mwilini mwako unahisi kunavitu vinatembea madaktari hawalioni tatizo hilo, tatizo hili linakuchannganya mama polee waganga hawawaliwezi trtizo hilo.

Njoo ufanyiwe maombi, huu ndio ushauri wangu kwako ndugu yanguu eeeeh[emoji3495]

Christopher Mwahangila~ Kwa Mungu yote yanawezekana
 
Mtu akifikwa na matatizo akakusimulia huwa ni rahisi kuchukulia poa/kucheka/kukejeli but ngoja yakupate wewe ndio utaona dunia imekuelemea
Pole yake huyo mkuu asikate tamaa MUNGU yupo ndie daktari mkuu, hata me hii wiki mama kaugua sana kiasi cha kuzidiwa kaongezwa maji na damu ila leo kapata nafuu hata kaweza kuongea...
Aende hospital kubwa mf. CCBRT,muhimbili,Bugando,KCMC atapona naamini hilo 100%
 
Nina rafiki ambaye jana kufunguka kile alichokuwa anapitia kwenye mahusiano yake, ana mwanamke ambaye anaishi naye huu mwaka wa pili sasa ila mambo yamebadilika tangu mwezi November mwaka jana; mwanamke anaumwa magonjwa ambayo hospitali hayaonekani, anakosa hamu ya kula, kapungua uzito, hedhi yake imekua irregular sana, usiku halali vizuri anaona kama pumzi inambana
Mpaka sasa vimepimwa vipimo vingi na ugonjwa hauonekani (kuanzia kuangalia matatizo ya tezi mpaka cholesterol)

Jamaa yangu anakaribia kuchanganyikiwa
Kama wanamiliki gari waliyopewa zawadi waichome moto.
 
Muulize huyo rafiki yako, Kuna Mwanamke alimwahidi kumwoa akabadili mawazo na kumwoa huyo mwingine?

Mwambie aende kwenye tiba mbadala, otherwise anaweza kumpoteza mpenzi wake

Maana vita za Wanawake huwa haziishi wakiamua
 
Ameshamtolea mahari?

Kwao kwa huyo binti wanajua kama anaishi naye?

Wameshazaa naye ama bado?

Kama wanaishi ki-sogea tuishi tu, cha kwanza afanye mpango kwao na binti wajue anaumwa na wao ndiyo wahusike zaidi, mwamba yeye aendelee kumsupport binti kama bf wake tu.

Yani namaanishaa, likitokea la kutokea asije akajikuta anasusiwa maiti na ndugu wa.binti watamgeuka.
 
Pole Sana .

Jaribu kwenda katika hosptali kubwa zaidi.

Hakikisha hosptalini wameshindwa kabisa ndo ufikirie tiba mbadala Kama za mitishamba.


Mpe hope zaidi mgonjwa hasa nyakati hizi za magumu.

Don't leave her alone.
 
Angalia background yake, msongo wa mawazo kwa muda mrefu pia husababisha kitu hicho.
Kwa kifupi tatizo Kama Hilo hua ni matokea Yanayo sababishwa na hitilafu kweny mfumo wa ubongo.
Fanya hivi
1. Badilisha mazingira hata mwezi mmoja, aende sehemu ambayo sio mgeni Sana mfano wa sehemu hizo ni Kama nyumbani kwao. Yaan aende sehemu ambayo atakua huru.

2. Badili aina chakula mnachotumia.
Tafta sato wa mwanza walio kaangwa na ugali wa sembe pamoja na maziwa kwa muda wa mwezi mmoja.

3. Apunguze matumizi ya simu, computer, tv n.k baadala yake atafte vitabu vyenye story ngumu ili atumie nguvu nying kuelewa hio pia inaongeza afya ya ubongo.

4. Afanye mazoezi pia kuchangamsha mwili ili mzunguko wake wa damu uwe sawa.

Kwa kifupi shida yake ipo kweny ubongo na Hadi kufikia hatua hio maan ake tatizo lilianza muda mrefu kwa hio hata kurudi kwenye hali yake ya kawaida itachukua muda mrefu kidogo piaa.
 
Mtu akifikwa na matatizo akakusimulia huwa ni rahisi kuchukulia poa/kucheka/kukejeli but ngoja yakupate wewe ndio utaona dunia imekuelemea
Pole yake huyo mkuu asikate tamaa MUNGU yupo ndie daktari mkuu, hata me hii wiki mama kaugua sana kiasi cha kuzidiwa kaongezwa maji na damu ila leo kapata nafuu hata kaweza kuongea...
Aende hospital kubwa mf. CCBRT,muhimbili,Bugando,KCMC atapona naamini hilo 100%
Pole mkuu
 
Back
Top Bottom