Ushauri mpya kuhusu uvaaji wa Barakoa (Masks) kujikinga na maambukizi ya Covid-19: Tujielimishe ili tuamue vema

Naona barakoa classic kwa ajili ya ma sister duu na ma brother men zikitengenezwa, trump kakataa kuvaa maana anaweza kuonekana kituko. Nakumbuka nilivyokuwa mdogo tulikuwa tunawavalisha mbuzi barakoa wasile mazao ya watu njiani wakati tukiwapeleka machungani.
 
MM Togolani,
Kwanza angalia paragraph aliyoizungumzia Pascal na wewe ukasema unafanya masahihisho. Maana yeye alichukulia mfano wa WHO na wataalamu wa afya kushauri pale kunapokuwa na suspect/mgonjwa pamoja na mtoa huduma wavae mask ili kujikinga na maambukizi kati yao. Sasa marekebisho yako yanalenga kupinga hilo, je ni sawa?

Pili, umapozungumzia effectiveness ya N95 na unasema ni gharama unalinganisha na nini?
Ina maana ni bora kutaokutumia N95 mask kwenye jamii hata kwa ku-subsidize cost yake, ila tusubiri janga ili tutibie wagonjwa na mambo mengine yote gharama zake zitakuwa chini zaidi?
 

Ndugu Missile of the Nation naheshimu hoja zako lakini sifhani kama ni sahihi sana kwa mwasayansi kutoa hoja kwa kudharau kiwango cha ufahamu kinachohitajika. Pia ni makosa makubwa kufanya assumption kwamba kiwango fulani cha uelewa kinatosha kutazama changamoto ya kisayansi katika ujumla wake.

Kwa mfano, hoja yako ina gap kubwa maana inatoa picha kwamba uvaaji wa masks pekee (bila ufahamu wa namna sahihi wa kuvaa, kuzitumia, kuvua, kuzitunza, nk ) ni toshelevu. Kama uvaaji wa masks una msaada kwa kiwango unachokisema, unaweza kutueleza kwa nini wahudumu wa afya wanaovaa sio masks tu bali full PPE muda wote wanakufa kwa makumi na huu ugonjwa?

Pili, unaweza kunionesha data au utafiti unaoenesha jinsi ambavyo ugonjwa umekua contained Asia? Asia ipi na wamecontain kwa kiasi gani ukilinganisha na nchi nyingine duniani? Mbona data za wagonjwa na vifo za kila siku hazioneshi hilo? Unaweza ukatoa statistics zinazothibitisha hii claim yako?

MM Togolani
 

lukonge ninashawishika hujanielewa na hujaelewa muktadha wa nilichomjibu Pascal.

Kwenye makala yangu nilikua nimekosea neno nililokusudia kuandika kwenye para aliyoinukuu. Alipo-comment na nikajua katafsiri kwa muktadha wa kosa kwamba zina kinga (katika ujumla wake) na akanukuu nilichoandika, ndio nikaona kosa na kumwambia nilikosea na nimerekebisha. Shida hapo iko wapi? Kwa nini unahangaika na nilichomjibu Pascal badala ya kusoma uchambuzi na kusema kosa lilipo? Ukisoma mada unaona inapingana na huo ushauri?

Pili, ili kuthibitisha practibaility ya ushauri wako, unaweza kutueleza angalau nchi moja duniani ambayo wananchi wake wote wamevaa au wanavaa N95? Unaweza ukatupa uchambuzi wa gharama zake kwa nchi nzima kwa muda wote ambapo tutakua na maambukizi ? Na mbona unaziongelea kwa uzito as if umethibitisha kuzivaa ndio kinga? Kama kuzivaa pekee ndio kinga, madaktari wanaofariki wakihudumia wagonjwa inakuwaje wakati wamevaa N95?

Kama umeshafanya kazi ya ushauri elekezi (consultancy) utakua unafahamu wazi kwamba hatukimbilii tu kuoa ushauri wa solution kwa kuwa inafanya kazi. Tunatazama factors nyingi kama vile ni practicability ya solution, gharama, hasara, sustainability, context, alternatives, etc.

MM
 

China, Taiwan, Singapore na Japan raia wake wote walivaa masks na zimesaidia sana
 
China, Taiwan, Singapore na Japan raia wake wote walivaa masks na zimesaidia sana

..naunga mkono maoni yako 100%.

..face mask zinaweza kusaidia.

..pia ni affordable kwa uwezo na mazingira yetu.

..tahadhari yoyote ile ambayo iko ndani ya uwezo wa waTz ni lazima tuichukue.

..kuna taarifa za mlinganisho wa athari za Corona kati ya South Korea[ face mask country] vs Italy[ non face mask country].

..It is better to ERR on the side of CAUTION.
 
Serikali kama inaogopa kuwa hakuna stock ya kutosha ya mask iwe wazi tu kuwa wenye nazo wavae, wasionazo wafuate taratibu nyingine mbali mbali za kuminimize chance za kuambukizwa, lakini isidiscourage mask wakati zimeinusuru Asia na wazungu wameanza kukiri sasa kuwa Asians walikuwa sahihi kwa watu wao wote kuvaa mask
 

..wananchi wanaweza ku-IMPROVISE kwenye mask.

..kipande cha kanga au baibui kwa maoni yangu it is better than having no mask.
 
China, Taiwan, Singapore na Japan raia wake wote walivaa masks na zimesaidia sana
View attachment 1408832

Napata shida kidogo mtu akisema ana data za kuthibitisha jambo halafu anachokileta ni news tena inayosema kabisa "ASIA MAY HAVE BEEN RIGHT..."..na sio "..ASIA ARE RIGHT".

Influence ya kimarekani inatutesa sana sisi waafrika na inatawala sana namna with think and view the world. Hadi juzi Marekani na nchi karibu zote zilikua na msimamo mmoja kwamba hakuna evidence. Hadi ninapoandika hapa WHO bado hawajabadili opionin yao. Ila leo kwa vile Wamarekani wametoa kauli tofauti (tena bila research data), tayari tunabadili narrative na tunawanukuu kama ndio ushahidi. This is a very serious intellectual problem we have to address.
 
Statistcs gani unazozitaka?, za idadi ya watu waliokuwa wanavaa masks huko katika nchi za Asia au unataka nini haswa?

Ngoja mimi nikupe statistics za Covid-19 kwa nchi ulizozitaja na nyingine za Asia (wanaovaa sio tu mask bali wengi wanavaa hijabu) halafu uniambie ni kwa jinsi gani zinaonesha masks zimedhibiti maambukizi. Tazama hapa.















 
Statistcs gani unazozitaka?, za idadi ya watu waliokuwa wanavaa masks huko katika nchi za Asia au unataka nini haswa?

Nchi nyingine inayosemekana imefanikiwa kudhibiti kwa kuvaa masks ni Czechia. Data zao hizi hapa. Naomba nisaidie kuelewa ni kwa jinsi gani hii graph inaonesha kudhibiti maambukizi kwa kuvaa masks. Mimi nikitizama naona an increasing number of cases from day one. Kama masks zinawakinga kwa kuwa wanavaa nchi nzima, kwa nini cases zinaongezeka kila siku?

 
Statistcs gani unazozitaka?, za idadi ya watu waliokuwa wanavaa masks huko katika nchi za Asia au unataka nini haswa?

Nchi gani kati ya hizo nilizoweka hapo imepunguza maambukizi? Kwa kiasi gani? Kwa nini idadi inaongezeka kila siku wakati wanavaa masks muda wote?

Niwashauri tena, musiongelee scientific ideas/data kwa habari za masimulizi ya mtaani au kwenye news pekee. Data za Corona za kila nchi duniani WHO inaziweka live online kila siku. Na hizi ni clinical data tu (watu waliokwenda hospital wakapimwa). Kuna maelfu wasiopimwa. Tazameni data kujiridhisha badala ya masimulizi ya kusikia.

Marekani rais wao mwenyewe hajakubaliana nao kwamba kuna evidence na kajibu mbele ya media dunia ikisikia kwamba wahta they have given are just recommendations. Sio sahihi sisi kukimbilia kuwakariri kama reference. Tumejiuliza wametumia data au utafiti gani kubadili recommendations zao? Tumeziona hizo data? Zinasemaje?
 
Nafananisha hizo masks na kondomu! Ili kuleta ufanisi wa kinga, ME na KE wanapaswa kuvaa zana (najua mabaharia mmenielewa, japo utekelezaji hukumbwa na wenge).
Swali la msingi: je zitapatikana kwa urahisi? Elimu sahihi ya matumizi imetolewa? Hasa huku Nanjilinji Rudinyuma
 

Tazama idadi ya waliopata huo Ugonjwa katika nchi za Asia kulinganisha na Ulaya na Marekani nchi ambazo hazivai hizo mask na pia uone RATE OF INCREASE ni wapi kubwa zaidi.

Laiti Asians wasingevaa masks hizo graphs zako zisingesoma few thousands katika maambukizi

kwa upande wa Asia zingekuwa kubwa sana at par na Ulaya na America au more kwa sababu ulianzia huko na walikuwa wa kwanza kudivise strategy ya kupambana nao

Hizo graph zako hujazipa right interpretation, ile kuonyesha graph kukua ni kitu cha kawaida maana cases zinaongezeka ila cha msingi angalia RATE OF GROWTH YA HIZO CURVE
 
Kwa sehemu uko sahihi kaka kwenye analysis yako. Shida kubwa tu ni kutoa conclusion kwamba kilichosaidia ni masks.

Tunajua hawa watu wanetumia combination of measures. They have been doing almost everything that seems to make sense kama kinga. Hivyo sioni usahihi wa ku-single out one factor or variable halafu ukatoa conlusion kwamba ndio imefanya kazi. Kwa mfano S.Korea walianza kuweka kila anayeingia karantini siku nyingi; wanatrace movementa za watu kwa simu zao; etc.

China kuwarejea data zao inahitaji ujasiri maana dunia nzima inajua how much wamekua wakindanganya kuhusu ukubwa wa tatizo from day one.

Ila cha pili cha kutazama unapolinganisha na Ulaya, ni vema kuitazama Covid-19 katika upana wake na factors zinazochangia vifo na mambukizi.

Tatu, ni lazima ujue rate ya kupima kwenye nchi ili uongelee kupungua kwa cases. Nchi nyingi hazipimi isipokua wale tu wanaozidiwa na kutafuta tiba. Kwa mfano UK ingekua inapima kila mtu, huenda ingekua na idadi sana na au kuzidi USA. Hivyo badala ya kusema new cases zinapungua, statement sahihi ingekua new critical cases zinapungua.

Sijatafsiri graphs zangu vibaya. Sema sijatafsiri kwa maana uliyomaniisha wewe. Kama ni rate ya new cases..yes wanapungua. Lakini kama nilivyosema kunahitaji kufahamu zaidi hizi ni cases zipi..kila mtu aliyeathirika au critical cases.

Ngoja nibandike graphs ambazo ndizo ulimaanisha wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nakubaliani na wewe kuwa combination of measures ndiyo jibu sahihi
Lakini sikubaliani na wewe kuidismiss mask kuwa haina msaada mkubwa kwenye kusaidia masses kupambana na hili janga

What I can say ni kwamba Mask ni ingredient kubwa kabisa katika fight hii. Kama nchi yetu inataka tutoke majumbani tukatafute rizki, na kwa kutoka huko tutapanda madaladala na mwendokasi basi pamoja na measures nyingine za kunawa mikono na kutumia sanitizers basi Masks haziepukiki ni kitu muhimu sana. Yaani kwenye medani ya kijeshi tungeilinganisha na kikosi maalum cha makomando kwenye hii fight
 

Nadhani ulimaanisha presentation ya data kuwa hivi:












 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…