Ushauri mpya kuhusu uvaaji wa Barakoa (Masks) kujikinga na maambukizi ya Covid-19: Tujielimishe ili tuamue vema

Ushauri mpya kuhusu uvaaji wa Barakoa (Masks) kujikinga na maambukizi ya Covid-19: Tujielimishe ili tuamue vema

Hahahahaha

Wote waliokuwa wanapiga vita niqaab na hijab za Kiislam, sasa watafunika nyuso zao wakipenda wasipende.

Allahu Akbar.
Kwa hio Iran walikuwa hawavai!? Mbona maambukizi yapo juu
 
.
Ushauri wa barakoa na mkanganyiko wake

Jana Marekani na Uingereza, ambazo ni nchi zenye nguvu kiuchumi na kuongoza katika ugunduzi na tafiti za kisayansi, zimetoa kauli zinazokinzana kuhusu uvaaji wa barakoa (masks) kama njia ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa mtu ambaye hajaambukizwa (mass masking).

Nina hofu kwamba maamuzi yao (hasa ya Marekani) yanakwenda kuongeza taharuki Afrika katika janga la Corona. Hii ni kwa sababu hadi sasa ushahidi unaonesha kwamba nchi nyingi Afrika zinaparamia mapendekezo au maamuzi yanayochukuliwa na nchi za Maghararibi bila kutazama mazingira ya utekelezaji wake katika nchi zetu.

Walichokisema kinaweza kabisa kuchukuliwa kama ushahidi wa kisayansi na nguvu zote zikahamishiwa kwenye uvaaji wa barakoa. Naomba nielezee mkanganyiko huu kwa kifupi, maana yake na tunavyoweza kuutumia.

Hadi juzi, taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya Marekani (CDC) walikua na msimamo kwamba uvaaji wa barako hauna msaada kumkinga mtu kupata maambukizi. Ila jana walisema watapitia upya mapendekezo (recommendations) yao maana kuna dalili kwamba zinaweza kuwa na msaada. Leo wameibuka na mapendekezo mpya kwamba watu wanaweza kuvaa barakao zisizo za tiba kama njia ya kujikinga na maambukizi. Hata hivyo rais Trump yeye kasema hatava barakoa maana hayo ni mapendekezo tu.

Wakati huohuo, serikali ya Uingereza imeendelea na msimamo uliokua unajulikana katika viunga vya wanasayansi kwamba hakuna msaada kwenye kuvaa barakoa kwa mtu mzima. Katika kuweka msisitizo, wamesema wamewasiliana na watafiti wenzao kule Hong Kong (watu wanaposingizia barakoa zimesaidia) na wamewathibitishia kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba zina msaada.

Nini msingi wa hoja za kisayansi kwa jambo hili?
Tangu maambukizi ya Corona yaliposhika kasi, kumekua na mjadala mkubwa wa matumizi ya barakoa kama moja ya vitu vinavyoweza kusaidia mtu kujikinga na maambukizi. Baadhi ya wanasayansi/watafiti wamekua wakijenga hoja kwamba barakoa zina msaada na hivyo watu washauriwe kuvaa. Hata hivyo nchi nyingi pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) wamekua wakishauri kwamba uvaaji wa barakoa hauna msaada kumkinga mtu anayehudumia wenye maambukizi pekee
(TAZAMA HAPA). Wanashauri parakoa kuvaliwa na mwenye maambukiki kupunguza uwezo wake wa kusambaza virusi anapokosa, kuongea au kupiga chafya.

Ukiachilia mbali hoja za kisayansi, wanananchi wa kawaida wamekua na mtizamo kwamba barakoa zinazuia kuambukizwa Corona. Fikra hii inahusishwa na ukweli kwamba tangu Corona ilipoanza kilichokua kinaonekana kule China ni watu waliozivaa kila mahali. Hii ikachukuliwa moja kwa moja kwamba ile ni kinga ya Corona. Ila ukweli uliopo ni kwamba uvaaji wa barako kwa China na hata Hong Kong ni utamaduni wa kila siku unaosababishwa na uchafuzi mkubwa wa hali ya hewa. Barakoa zinajulikana kitaalamu kwamba zina uwezo wa kusaidia kupunguza uvutaji wa hewa chafu. Hivyo kule China kutokuvaa barakao hasa kwenye miji mikubwa inachukuliwa kama uzembe (being irresponsible). Corona imewakuta wachina wakivaa barakoa na sio kwamba barakoa zimeanza kuvaliwa kama kinga ya Corona.

Lakini hata tukichukulia kwamba wachina walizivaa kujikinga na Corona, bado sio njia sahihi ya kuhitimisha kwamba ni kinga. Tukumbuke wao walipata ugonjwa huu wakiwa hawajui unatoka na nini na unaambukizwaje. Hivyo kwa taharuki waliyokua nayo walijaribu kila njia kutafuta kujikinga bila kujali njia hizo zina tija au la kwa sababu mwenye njaa hachagui chakula. Ila kwa sasa ulimwengu una uelewa mpana kwa kiasi fulani kuhusu ugonjwa wa Corona na unavyoenea hivyo sio sahihi kuendelea kuchukua hatua kwa taharuki au kubahatisha iwapo kuna nafasi ya kutumia akili na ushahidi wa kisayansi.

Kuna machapisho mengi ya kisayansi yanayojadili jambo hili ila katika ujumla wake, yanakubaliana kwamba hadi sasa hakuna ushahidi wowote wa kitafiti kuthibitisha kwamba barakoa zina uwezo wa kumkinga mtu mzima na maambukizi ya Corona. Kama zingekua kinga, ni wazi China wangeweza kuudhibiti ugonjwa mapema sana maana wao kuzivaa ni utamaduni. Pia nchi ambazo zinavaa kwa wingi kama Hong Kong na Korea zisingekua zinatoa taarifa ya wagonjwa wapya na vifo kila siku kama tunavyoona. Wanasayansi wanaotetea uvaaji wa barakoa, wanasema kutokuwepo kwa ushahidi wa kwamba zinasaidia, haimaanishi kuwa ni uthibitisho wa kutokua na msaada. Nikitafsiri hoja yao katika mazingira yetu nitasema: wewe ukisema hujawahi kuona paka anayepaa, haiwezi kutumika kama ushahidi kwamba hakuna paka anayepaa. Inawezekana kabisa tukiendelea kuchunguza paka wote tukakuta yuko anayepaa.

Nini ushahuri wangu?
Nina mambo makuu mnne ya kugusia kwenye jambo hili kama ushauri.

  1. Hakuna ushahidi kwamba barakao zinasaidia kujikinga na maambukizi. Haijalishi nani katoa mapendekezo, ila kisayansi na tiba, maamuzi hata kama yanaonekana ni mazuri kama hayana ushahidi wa kutosha wa kitafiti. Sio mapendekezo yote yanatumia ushahidi wa kisayansi. Mengine yanatolewa kulingana na mazingira hasa watu wanapokua kwenye taharuki au hawana njia mbadala ya kuitegemea. Tusichukulie mapendekezo ya CDC kama vile ndio amri ya 11 tukaanza kukimbizana na barakoa tukazua mengine na tija tusipate. Bado nafuatilia kujua CDC wamechukua ushahidi gani kufikia mapendekezo haya (bado natafuta desa walilotumia).
  2. Kuna baadhi ya tafiti za kisayansi zimeonesha kwamba uvaaji wa barakoa kwa wananchi (mass masking) unaweza kuwa na msaada wa kisaikolojia. Bila kujali kwamba zina kinga au vinginevyo, tafiti zimeonesha kuna watu hujisikia salama au wamekingwa kwa kiasi fulani wao wenyewe wanapokua wamevaa barakoa au/na watu wengine wanaowazunguka wamevaa pia. Hivyo, kwa kuwa jamii nzima ina taharuki na madhara ya kisaikolojia ya ugonjwa huu ni makubwa sana, tiba ya kisaikolojia inahitajika pia. Hivyo, kama mtu au watu wanajisikia salama zaidi wakivaa barakoa, wavae na watu wengine wasiwashangae wala kuwakosoa wakizivaa.

  3. Ninafahamu serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa elimu hukusu mlipuko wa Corona. Ila ninawashauri wahusika waendelee kutoa elimu zaidi kwenye eneo hili kuhusu uhalisia wa msaada wa barakoa. Walizungumzie katika dhana ya kinga (based on existing scientific evidence) na katika dhana ya tiba ya kisaikolojia (mitigating psychological effects). Watu wajue kwamba sio lazima kuvaa lakini kama wanaona kuvaa kunawapa amani ya moyo zaidi, basi wavae. Elimu hii ni muhim sana kwani iwapo watu wengi watazivaa huku wakiwa hawana uelewa wa kitaalamu wa namna bora ya kuzivaa, kuzitumia, kuzitunza, na usafi wake, ni wazi zinaweza kuwa sababu ya maambukizo zaidi au kuleta madhara mengine ya kiafya.

  4. Kwa kuwa Marekani wamebadilisha mapendekezo yao, na tunajua nguvu yao kwenye taasisi ya kimataisa, kuna uwezekano mkubwa kabisa kwmaba WHO nao watabadilisha mapendekezo yao na kuhamasisha uvaaji wa Barakoa. Jana nimesikia afisa mmoja wa WHO akikaririwa kusema nao watapitia upya mapendekezo yao kuhusu barako baada ya Marekani kubadili. Tusishangae tukiona nao wanaaza kutushawishi kuvaa barakoa. Bado tukumbuke, sio kila mapendekezo tupewayo ni sahihi na yatatekelezeka.

    Imeandikwa na MM Togolani (mmtogolani@gmail.com)
    Mtafiti wa mifumo ya digitali katika ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa
IMG-20200404-WA0030.jpeg

Jr[emoji769]
 
Sasa wewe mleta mada unajichanganya, kwa nini madaktari na manesi ambao hawana Corona wavae Mask kujikinga kuambukizwa na wenye Korona halafu wakati huo utoke hapo useme eti wanasayansi wamedai kuwa hakuna msaada mkubwa wa mask kwenye kuzuia maambukizi?

Kama barakoa ni nzuri kwa madaktari na manesi basi ni nzuri pia kwa raia wa kawaida maana huko kwenye madaladala tunayopanda hatujui ni nani kasthirika. Je akipiga chafya au akakohoa si utaambukizwa kama hujavaa mask?
 
Kama ukweli ni ukiambukizwa ndani ya dakika chache na wewe una anza kuambukiza, barakoa ni muhim Sana maana chanzo cha maambukizi ni pua na mdomo. Pia kusema china wana utamaduni wa kuvaa barakoa sidhani kama ni Sahihi!
Kwenye wa china 10,000 kabla ya ugojwa unaweza mkuta mmoja tu kavaa. Serikali ya China tuliona sana ikisisitiza uvaaji wa barakoa na Mimi pia kwa ufaham wangu Nina pendekeza uvaaji wa Barakoa!!

Tusiwaamini Sana hawa wanao jiita wa kubwa wana mengi juu yetu. Wao wana gombania barakoa Sisi tusivae!!!
Adi Muda huu ni Mungu ana tulinda. Waruke vikwazo walivyo weka kwa kupokea barakoa Sisi tusitumie barakoa!!

Putin’s U.S. Virus Aid Flight May Have Carried Sanctioned Goods!

fundi25 Hiki ulichosema kuhus uuvaaji wa barakoo China umetoa wapi ndugu yangu. Nilichoongea sio fikra zangu wala habari za kupika. It is a documented fact. Unaweza kujipa muda kidogo tu ukaingia youtube kutafuta matukio ya China, Hong Kong na kwingine kabla ya Covid-19 kisha upime ukweli.
 
Thanks brother for your digital based research.

Binafsi naona kuna haja saana ya kuzipa nguvu taasisi zetu za utafiti zitakazo fanya utafiti na kutoa mapendekezo kulingana na mazingira yetu.

Nadhani kama vilivyo bize vyuo vya wenzetu kufanya tafiti nasisi tulitegemea vyuo vyetu pale udsm conas wawe bize kutafiti... muhimbili bugando udom n.k lakini sijui wanasubiri paka wanasiasa waseme?

Nilitegemea miongozo mingi itoke from them kuliko kutoka kwa wanasiasa. Yani wanasiasa wamekuwa watoaji maelekezo kuliko hata watalaam wa afya?

Kwakweli mapendekezo na tafiti nyingi za hawa mabeberu zinaonekana hazifiti saana kwa sisi Africans mpaka tunafikia kuhisi kama wananjama zidi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umenena vema. Niliandika kwenye uzi mwingine kujadili nafasi ya watafiti/wasomi wetu kwenye janga hili. Umegusia moja ya mambo niliyoajdili: Mapambano dhidi ya Covid-19 Tanzania na kwingineko Afrika: Watafiti na wanasayansi wetu mko wapi na munasemaje? - JamiiForums
 
MM Togolani,

Kwanini wanashauri watu wakae 1 m apart,watu wanawe mikono na kutojishika usoni?Ni kwa sababu virus hawa wanaaffect respiratory system, wanaingia kupitia mfumo wa hewa.Kwa akili ya kawaida tu na hata sio mpaka uende medical school, uvaaji wa mask unasaidia sana kweny kujikinga kuvuta hewa yenye infected airdroplets lakini pia kujishika shika usoni ambako kunawez pelekea kuvuta virus kutoka kwenye mikono in case kama umeshika sehem virus hivyo vimeachwa au kama ur infected itasaidia kuepusha the spread.1 m distance apart, kuvaa masks, kunawa mikono na sabuni thouroghly kwa maji tiririka , using hand sanitizers, kuepuka crowded areas...hizi ndio kinga kwetu huku uswahilini. Tusiangalie kitu kimoja tu kwa sababu kujikinga na hii kitu depends on many factor not just a single method.

Uko sahihi kabisa ndugu Dystonia7 ila kama wewe ni mwanasayansi nadhani unaelewa kwamba ili ushauri utolewa kuhusu effectiveness of any practice, kunahitajika scientific evidence na sio matumizi ya "akili ya kawaida isiyohitaji kwenda medical school".

Ni kweli masks ni kinga ya magonjwa yanayoweza kuambukizwa kwa hewa au droplets. Ila kila ugonjwa una infectious characteristics zake ambazo zinaweza zisikabiliwe kirahisi kama magonjwa mengine yanayaofanana nao. Ukisoma nilichoandika, nimeuliza swali kwamba kama masks ni kinga yenye tija kama watu wengi wanavyotaka kuaminisha wengine, kwa nini South Korea, Hong Kong, Czech, China, nk wana maambukizi hadi leo wakati wanavaa muda wote nakuchukua tahadhari nyingine nyingi?

Nadhani ushauri mzuri nimeutoa namba 2. Kwa yeyeote anajisikia salama kuvaa barako kama kinga afanye hivyo ila umakini unahitajika watu wasidhani kuna uhakika wa kinga. Bado tunacheza na bahati naasibu.

MM Togolani

MM Togolani
 
Nijibu swali lako ndugu lukonge :
Nilichorekebisha ndicho sahihi. Nadhani hujasoma vizuri nilichoandika kwenye uzi wangu. Kuna maelezo ya kutosha juu ya ushauri wa kitaalamu na unaotolewa na WHO ya nani anahitajika kutumia barakoa kama kinga na kwa nini. Nimekuwekea na link.

Uko sawa kuhusu ushauri wa kuzivaa. Ila kwa sasa ushauri sahihi ni kuzitazama kama tiba ya kisaikolojia kuliko msisitizo wa kinga maana hakuna uthibitisho.

Wataalamu wanaoshauri mass masking (uvaaji wa watu wengi/wote) hawashauri kutumia medical masks. Maana ni gharama isiyo lazima. Hata ushauri wa CDC wameshauri watu kuvaa non-medical masks. Wanashauri improvisation kutumia hata vitambaa vya kawaida. Nimeona wengine wamependekeza hijabu hapa.

Ukisema umerekebisha, ina maana mgonjwa wa Corona kuvalishwa mask pamoja na mtaalamu wa afya kuvaa mask havina msaada kwao katika kuambukiza ugonjwa kati yao? Kwa nini sasa hawa watu wanashauriwa na wataalamu wa afya katika mazingira ambayo mtu ni suspect kuvalishwa/avae mask na mtaalamu wa afya hutakiwa kuvaa mask?

Naunga mkono hoja ya kwamba, kwa kuwa watu/mtu anaweza kupata ugonjwa wa Corona na kulingana na kinga zake asionyeshe dalili au akakaa na ugonjwa siku 14 mpaka 21 ndipo akaonyesha dalili na wakati huohuo anao uwezo wa kusambaza ugonjwa, ni vyema basi tukasema kila mmoja wetu ni "suspect until proven otherwise". Hivyo, ni vyema kuunganisha taratibu ziwe: barakoa+nawa mikono kwa sabuni kwa maji tiririka/sanitizer+social distance inaweza kutusaidia sana.

Sina uhakika kama nchi ikiingia gharama ya kusambaza mask za N95 kwa wananchi(ingawa upatikanaji ni issue) ni sawa au inazidi huduma ya janga hili pale linapoingia kikamilifu ili tuanze kukimbizana na wagonjwa wakati huo hata ventileta 200 hatuna nchi nzima.
 
fundi25 Hiki ulichosema kuhus uuvaaji wa barakoo China umetoa wapi ndugu yangu. Nilichoongea sio fikra zangu wala habari za kupika. It is a documented fact. Unaweza kujipa muda kidogo tu ukaingia youtube kutafuta matukio ya China, Hong Kong na kwingine kabla ya Covid-19 kisha upime ukweli.
Hayo ya Hongkong angalia iyo video utajuwa kwa nini walivaa barakoa!
Nimezunguka china Sana kwenye viwanda na mashamba suala la kuvaa barakoa kwenye masuala ya safety kwa china sio kipaumbele sana!! Kama ilivyo kwa nchi za magharibi!
 
Sasa wewe mleta mada unajichanganya, kwa nini madaktari na manesi ambao hawana Corona wavae Mask kujikinga kuambukizwa na wenye Korona halafu wakati huo utoke hapo useme eti wanasayansi wamedai kuwa hakuna msaada mkubwa wa mask kwenye kuzuia maambukizi?

Kama barakoa ni nzuri kwa madaktari na manesi basi ni nzuri pia kwa raia wa kawaida maana huko kwenye madaladala tunayopanda hatujui ni nani kasthirika. Je akipiga chafya au akakohoa si utaambukizwa kama hujavaa mask?

Ndugu Missile of the Nation nahofia sijajichanganya ila ni wewe hujasoma kwa utulivu. Ila ngoja nijichanganue. Ukisoma vizuri nimeleza ushauri wa kitaalamu unasema ni watu gani wanashauriwa kuvaa na kwa nini (waathirika na wanaohudumia waathirika). Nimekuwekea na link kabisa.

Vinginevyo nilichotoa ni uchambuzi wa hoja zote mbili: kuvaa na kutokuvaa kama kinga kwa mtu ambaye hajaathirika. There is a lot of publications on this subject ningezirejea hapa uzi ungekua mrefu. Ila conclusion ni moja hadi sasa: kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba mass masking (uvaaji wa kila mtu hata ambaye hajaathirika) una tija katika kuzuia maambukizi.

MM Togolani
 
Nashukuru kwa sumaary hii. Ila tunapozungumzia uvaaji wa masks lazima tujue ni variable moja kati ya nyingi sana za equation ya Covid-19. Bado kuna unknown nyingi juu ya kazi ya maambukizi ya ugonjwa huu. Ndio mana uvaaji masks umekua ni mjadala na mvutano mkubwa miongoni mwa wanasayansi iwapo kweli zina msaada kukabiliana na maambukizi ya huyu shetani wa familia ya Corona
 
Para hiyo imemaliza kila kitu.

Kwa vile tangu mtu kuambukizwa hadi kuonyesha simptoms ni 14 days, huwezi jua nani ameambukizwa na nani bado, hivyo to be on a safe side, barakoa zivaliwe na wote!

Sisi Tanzania anaetulinda ni Mungu tuu kufuatia kuushtukia Corona ni shetani hivyo rais wetu Magufuli akaikabidhi shetani Corona kwa kiboko ya shetani ambaye ni Mungu mwenyewe vinginevyo...!

P
Watu wavae tu barakoa kama alivyoshauri Paskari sababu huwezi jua Nani kaambukizwa so kuavoid more spreading ya ugonjwa huo barakoa is unenevitable

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi Waafrica ni kama bendera tu, kokote upepo utapovuma ndio tunapoelekea,
Naamini kabisa likitokea jopo la madaktari wazungu wakatuthibitishia kua bange ni kinga dhidi ya Corona, Nina uhakika Mashehe na Mapdri wetu huku lazima nao watasokota tu.
Tena nmekumbuka hivi Jamaica [emoji1135] maambukizi yamefika huko?
 
Ndugu Missile of the Nation nahofia sijajichanganya ila ni wewe hujasoma kwa utulivu. Ila ngoja nijichanganue. Ukisoma vizuri nimeleza ushauri wa kitaalamu unasema ni watu gani wanashauriwa kuvaa na kwa nini (waathirika na wanaohudumia waathirika). Nimekuwekea na link kabisa.

Vinginevyo nilichotoa ni uchambuzi wa hoja zote mbili: kuvaa na kutokuvaa kama kinga kwa mtu ambaye hajaathirika. There is a lot of publications on this subject ningezirejea hapa uzi ungekua mrefu. Ila conclusion ni moja hadi sasa: kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba mass masking (uvaaji wa kila mtu hata ambaye hajaathirika) una tija katika kuzuia maambukizi.

MM Togolani

Kama mask inamkinga daktari basi inaweza kumkinga raia pia.

Ni commonsense tu huhitaji publication kwenye scientific journal kuliona hilo.

Kama mimi ni asymptomatic lakini nina virusi vya Korona bila kujijua tukakutana na wewe kwenye daladala tukakaa karibu karibu kisha nikapiga chafya, kama umevaa mask utanusurika, kama hujavaa mask utaupata

Ni logic simple tu, wala huhitaji research kujua kuwa leo ni jumamosi, it is just a fact!

Reason kubwa kwa nini Asia imeweza kucontain hii kitu haraka na damage kuwa minimal ni kwa sababu ya combination ya measures huku Kuvaa mask kwa kila mtu kukiplay major role
 
Nijibu swali lako ndugu lukonge :
Nilichorekebisha ndicho sahihi. Nadhani hujasoma vizuri nilichoandika kwenye uzi wangu. Kuna maelezo ya kutosha juu ya ushauri wa kitaalamu na unaotolewa na WHO ya nani anahitajika kutumia barakoa kama kinga na kwa nini. Nimekuwekea na link.

Uko sawa kuhusu ushauri wa kuzivaa. Ila kwa sasa ushauri sahihi ni kuzitazama kama tiba ya kisaikolojia kuliko msisitizo wa kinga maana hakuna uthibitisho.

Wataalamu wanaoshauri mass masking (uvaaji wa watu wengi/wote) hawashauri kutumia medical masks. Maana ni gharama isiyo lazima. Hata ushauri wa CDC wameshauri watu kuvaa non-medical masks. Wanashauri improvisation kutumia hata vitambaa vya kawaida. Nimeona wengine wamependekeza hijabu hapa.

Hawa WHO nao ni complicit kwenye kuiletea dunia hii janga, hawaminiki kwa sasa.
Hawa walitoa ushauri mbovu kuwa huu ugonjwa siyo human to human transmissible, kwa ushauri wao huu potofu wamemislead nchi na watu wengi sana, no wonder tupo hapa tulipofikia.

Sasa ukisema tuwafate hawa WHO kuhusu kupinga mask ni misleading nyingine kutoka kwa hawa jamaa
 
Ndugu yangu Missile of the Nation, hakuna mtu anachagua baba bila kujali ni mlevi, kasoma au ni mjinga lazima umsikilize kwenye majukumu yake ya kibaba. Nafasi ya WHO ni kubwa sana kwenye afya ya jamii hasa katika nchi zetu na huwezi kuipuuza. Hata hivyo simaanishi kila wanalosema ni sahihi 100% maana hata wao wako wanaowaburuza

Ila kwa hili la masks, huu sio ushauri "from the blue" bali umetokana na systematic review from scientific studies.

Kwenye kupotosha kuhusu Covid-19 (sijauona), hivi wa kuwalaumu ni wao au ni wachina amboa walikua hawasemi ukweli wa kinachoendelea? China ndio waliingiza dunia chaka na wakakata hata wataalamu wa nchi nyingine wasiende kusaidia kujua tatizo. Hadi leo wanaumiwa pia kwa kupotosha kuhusu idadi kamili ya wagonjwa na vifo.
 
Nijibu swali lako ndugu lukonge :
Nilichorekebisha ndicho sahihi. Nadhani hujasoma vizuri nilichoandika kwenye uzi wangu. Kuna maelezo ya kutosha juu ya ushauri wa kitaalamu na unaotolewa na WHO ya nani anahitajika kutumia barakoa kama kinga na kwa nini. Nimekuwekea na link.

Uko sawa kuhusu ushauri wa kuzivaa. Ila kwa sasa ushauri sahihi ni kuzitazama kama tiba ya kisaikolojia kuliko msisitizo wa kinga maana hakuna uthibitisho.

Wataalamu wanaoshauri mass masking (uvaaji wa watu wengi/wote) hawashauri kutumia medical masks. Maana ni gharama isiyo lazima. Hata ushauri wa CDC wameshauri watu kuvaa non-medical masks. Wanashauri improvisation kutumia hata vitambaa vya kawaida. Nimeona wengine wamependekeza hijabu hapa.

MM Togilani,
Nadhani wakati unafanya masahihisho haukufuatilia vizuri paragraph alitoichukua Pascal. Nenda fanya reference ta marekebisho yako uone kama yanaendana na hali halisi.

Kama unasema practice ya N95 ni effective je hiyo ni gharama sana unalinganisha na nini? Kusubiru maambukizi utibie wagonjwa na wengine wafe au u-sabsidize tool na watu wapate kwa gharama ya chini au bure ili kuilinda jamii/protection?
 
Back
Top Bottom