Ushauri muhimu kwa wajumbe wa bunge la katiba

jebibay

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2012
Posts
1,431
Reaction score
640
Mimi naomba nitoe ushauri ambao ninaamini utaondoa utata wa matumizi ya kura ya siri au ya wazi kwenye bunge la katiba, kwani naona hili swala linaleta mvutano mkubwa kwa wajumbe wa bunge. Kwanza nitaangalia kwa kifupi mitizamo hii miwili halafu nitashauri njia muafaka ya kufuata :

Kura ya wazi
Kura hii ina faida ya kuweka record na kuwawezesha wananchi kujua exactly kila mjumbe alivyoshiriki katika kufikia maamuzi kuhusiana na katiba, na hii taarifa inaweza ikawa muhimu huko mbeleni, ikiwa ni pamoja na kutusaidia katika michakato ya kuchagua viongozi wetu katika nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya nchi yetu. Nchi zilizoendelea na hasa Marekani wamekuwa wakitumia njia hii kwenye mabunge yao.

Kwa mfano, maamzuzi (ya kura) ya masenata wa Marekani katika mambo mbali mbali yanayohusu nchi yao, huwa sio siri. Mfano wakati Bush anataka kwenda kuivamia Iraq, Mama Clinton alipiga kura kukubaliana na Bush na Obama alipiga kura na hapana. Obama aliutumia uamuzi huo kama sehemu muhimu ya campaign hasa ukizingatia mwaka 2008 wamerekani walikuwa wamechoshwa sana na vita vya Iraq.

Vile vile mwaka 2007, rais wa Marekani, George W. Bush aliamua kuongeza idadi ya majeshi ya marekani kwa kiwango fulani nchini Iraq (Iraq war troop surge) ili wajaribu kuleta amani iraq halafu baadaye ndio waondoke. Hii ilipingwa na
Obama pamoja na waziri wa sasa wa ulinzi (Chuck Hagel) ambaye anatoka chama kimoja na Bush. Huu uamuzi wa troop surge ulikuja kuonekana baadaye kwamba ulikuwa uamuzi sahihi kwani ulikuwa na mafaniko makubwa. Wakati huyu
waziri wa ulinzi anahojiwa na masenata wenzake kabla hajawa confirmed kuwa waziri wa Obama katika kipindi chake cha pili, (kura yake) maamuzi ya Hagel kuhusiana na surge yalikuwa kati ya vitu ambavyo vilikuwa mwiba kwake, katika kuthibitishwa kwake kuwa waziri wa ulinzi. Kwa watu waliofuatilia ile hearing watakuwa wanakumbuka jinsi Mccain alivyombana huyu Bwana.

Pamoja na faida zinazoweka kupatikana kutokana na kura ya wazi, nadhani kwa nchi zetu hizi inabidi tufikiri kidogo kabla ya kuamua kufanya kama wanavyofanya wenzetu. Ninaamini wengi tutakuwa tunakubaliana kwamba nchi zetu nyingi za kiafrika, ubabe na ulipizaji wa kisasi kutoka kwa watawala wetu bado ni kitu ambacho bado kimeshamiri, hivyo ukisema watu wapige kura za wazi, wanaweza wakafanya maamuzi kinyume na utashi wao especially kama maamuzi yao wanaona yanakwenda kinyume na maamuzi ya viongozi wao. Matokeo yake hatutapata maamuzi sahihi ya wajumbe na nadhani hii itaondoa dhana nzima ya maamuzi sahihi, kwani maamuzi yatakuwa ni ya watu wachache tu ambao wengine watakuwa wametumika kama rubber stamp tu...


Kura ya siri
Kura ya siri ina uzuri kwamba mtu anakuwa na uhakika kwamba maamuzi yake ni siri yake mwenyewe. Hii itampa mtu confidence ya kuamua kile anachokiamini ni sahihi kwani ana uhakika kwamba maamuzi yake hayatatumika na yeyote kumfanyia hujuma huko mbeleni. Pamoja na kwamba kwa kutumia njia hii, records za wajumbe pamoja na maamuzi yao hazitakuwepo, lakini tutakuwa na uhakika wa maamuzi sahihi ambayo ndio yenye umuhimu zaidi ya hizo records. Mimi ninaamini hii njia ni nzuri kwa jamii kama yetu, ambapo mambo ya intimidation na matisho kutoka kwa watawala bado yapo kwa wingi.


Nini kifanyike ?
Kuna mjumbe mmoja wakati anachangia kwenye bunge la katiba jana alisema amepata simu kutoka kwa wananchi wake wakisema wanataka wabunge wafanye maamuzi kwa uwazi ili wafahamu wabunge wao wamefanya maamuzi gani. Hiyo ni sawa na lazima kutakuwa na wengine wengi tu wenye mawazo kama hayo. Vile vile ninaamini kuna wananchi wengine (kama mimi) ambao wanataka maamuzi yawe ya kura ya siri. Katika hili, watu mbali mbali wanaweza wakawa na misimamo tofauti.

Namna sahihi ya kuamua nini kifanyike ni kujua wengi wanataka kitu gani na hicho watakachoamua wengi ndicho kifanyike. Kama wengi wanataka kura ya siri, itakuwa wazi wengi wanaamini kwamba kura za namna hiyo ndio zitatota maamuzi sahihi na hivyo itabidi zipigwe kura za siri. Na kama wengi wanataka kura za wazi basi itabidi zipigwe kura za wazi. Sasa hakuna namna tunaweza tukapiga kura wote na kujua tunataka nini, ila tuna wabunge wa katiba ambao baadhi yao ni wawakilishi wa wananchi wa kuchaguliwa na wengine ni wa kuteuliwa (ambao nao originally walitoka kwenye makundi ya wananchi). Hawa wanaweza kupiga kura kwa niaba yetu, na watakaloamua ndilo tutakuwa wote tunalitaka na ndilo lifanyike.

Ninachoshauri ni kwamba KURA HII ya kuamua whether maamuzi ya Bunge la Katiba yawe kwa kura za wazi au za siri, yafanyike kwa KURA YA SIRI. Kama wataamua kura ziwe za wazi sawa, kama wataamua ziwe za siri sawa, ila kura hii ya kati ya haya maamuzi mawili iwe ya SIRI. Nadhani kwa wale wanaotaka kura za wazi hoja yao kubwa ni kwamba wananchi wajue wabunge wao walifanya maamuzi gani kuhusu katiba, na hii kura ninayoizungumzia hapa haihusu katiba bali inahusu tu maamuzi ya kanuni ya upigaji kura.
 
Inajulikana kabisa kuwa kura ya siri itakuwa ni pigo kubwa kwa chama tawala, kwa sababu ndo wanaowaburuza wabunge wao wakubaliane na matakwa ambayo hata wao hawayaafiki
 
hapa ni kura ya siri tu, hawa ccm wametufikisha hapa kwa ujinga wa kuburuza wengine fikiria wakti wa kupitisha bajeti wanaitwa mmoja mmoja kwa majina na anaanza waziri mkuu, wakiona waziri mkuu amesema ndio basi ccm wote ni ndio ulishaona wapi wote mkawa na mawazo yanayofanana! au kupiga kura ya ndiyoo au siyooo halafu spika anasema nadhani waliosema ndiyoooo wameshinda, hatutaki mambo hayo hii ni katiba ya nchi inayoamua mstakabali wa nchi mambo ya mzaha hayana nafasi this time.
 
Kuna mambo mengi ya maana ya kuzungumziwa na kujadiliwa katika Bunge hili maalum la Katiba, lakini kinachosikika sana ni kipengele cha Muundo wa Muungano wa serikali mbili au tatu. Binafsi sioni mantiki ya wana CCM kung'ang'ania muundo wa serikali mbili kwa kutumia hoja hafifu ya "hii ni sera yetu"! Hivi hawajui sera ni mkakati wa muda maalum na ukiisha timiza au fanikisha lengo lake unaachwa.Sera hii ni ya miaka ya 1970's na 1980's! Sasa ni miaka ya 2000 hawaoni muhimu wa kuachana na sera hii au ni kigezo cha kuzidi kula nchi? Hoja ya kung'ang'ania hoja ya SERIKALI MBILI kwa wana CCM, ni hoja ya kutaka KUVUNJA MUUNGANO kwa sababu wana MAPINDUZI WA ZANZIBAR hawawezi kuachia Serikali yao na nchi yao ambayo imeshapata karibu kila kitu kinachohitajika kuwa na nchi pamoja na dola huru. Wana CCM TAFAKARINI HILI KWA FAIDA YA TANZANIA, TANGANYIKA NA ZANZIBAR!
 
Suala la nyongeza, kama kuna mtu aliyefuatilia taarifa na ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Tanzania Comunications Regulatory Authority (TCRA) kuhusu suala la upatikanaji wa matangazo ya TV, atakubalina nami kuwa si Watanzania wengi wana ving'amuzi vya kuwawezesha kufuatilia mahojiano haya ya Bunge Maalum la Katiba kutoka Dodoma; kwa sababu hiyo kwamba wananchi wengi hawana ving'amuzi, hivyo eti hoja ya kutaka wananchi wawasikie wamefanya maamuzi gani wakati wa kupiga kura hayana mashiko. Pia ni ukweli ulio wazi kuwa watu wengi walisha kata tamaa kuangalia mahojiano ya Bunge letu baada ya kufumuka mtindo wa matusi, kejeli na ubabaishaji katika Bunge la JMT ambao wajumbe wake (ambao ni almost majority) ni wajumbe wa Bunge hili maalum! Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…