Ushauri: Mwanamke amenipigania sana nilipoumwa lakini dini imekuwa kikwazo kwetu kuoana, ndugu zangu wanataka pia nimfukuze sehemu ya kazi! Nifanyeje?

Ushauri: Mwanamke amenipigania sana nilipoumwa lakini dini imekuwa kikwazo kwetu kuoana, ndugu zangu wanataka pia nimfukuze sehemu ya kazi! Nifanyeje?

Kuna mwanamke nilikuwa nae kwenye mahusiano ni mtu ambae alinipenda na mm nilimpenda sana , kuna kipindi niliumwa sana kama miezi mitatu alipambania uhai wangu hadi dakika ya mwisho maana ilikuwa nusu nife...

Yaan unamuacha mtu aliekupigania kisa ndugu? Hv uanaume wako uko wapi, labda ungeachana nae kisa sabab nyingine, lkn eti ndugu mara dini.

Na ukimuachisha hio kazi utaumwa ufe unajuta sana maana Karma is a bitch
 
kuna kipindi niliumwa sana kama miezi mitatu alipambania uhai wangu hadi dakika ya mwisho maana ilikuwa nusu nife.
Kama ndugu walishiriki kupambania katika kipindi hicho lipa fadhila kwa mpatia mtaji au kwakumtafutia Sehemu ya kufanyia kazi badala ya hapo ila kama hawakushiriki watajua hawajui endelea nae
 
Kwan huyu Binti hakua tayari kubadili dini ???

Moyo wangu umeumia ila aah

Fanya kile unachoona ni sahihi na Mungu atam,bariki huyu zaidi

Maisha huwa yanabadilka dakika 1 tu
 
Mimi katika maisha yangu nilishasema DINI haiwezi kunitenganisha na mpendwa wangu hata siku moja wala ndugu yoyote yule! Maamuzi yangu ni Yangu Nilizaliwa Peke yangu nikapigana na kupambana peke yangu alafu mtu huku mwenye ndevu zake wanakuja kuleta ujinga.

Mimi Nikiwa Mkristo naoa vizur tu Muslim na maisha yanaenda kila mtu na dini yake ili mradi maisha yanakwenda watoto watachagua wapi waende.

Mkuu Roho nzuri haitafutwi Inaletwa na mwenyezi Mungu. Huyo manzi ndio chaguo lako. Angalia usije piga Mark Time.
Ogopa sana mtu aliyepigania Uhai wako leo hii unamuacha kisa DINI tofauti na kisa ndugu zako.
 
Fanya vile roho yako na moyo wako umefunuliwa ya kuwa ni kitu chema. Yaliwahi kunikuta enzi hizo, lakini baada ya kukaa kwenye msimamo aisee walewale waliosema yule binti hakufai kwasababu ni mpagani, wazazi wake wachawi sana leo hii wanaona ndiye mtu mwenye ndoa njema, yenye mafanikio makubwa na amani kuliko wenyewe

Kaa kwenye msimamo wako
 
Kuna mwanamke nilikuwa nae kwenye mahusiano ni mtu ambae alinipenda na mm nilimpenda sana, kuna kipindi niliumwa sana kama miezi mitatu alipambania uhai wangu hadi dakika ya mwisho maana ilikuwa nusu nife...
Itapendeza kama utamweka mbali na ndugu zako Kwa kumtafutia kitu kingine cha kufnya. Na ikiwezekana hata ndugu wasijue unaweza mfungulia biashara n.k
 
Back
Top Bottom