Ushauri: Mwanangu ana kipaji cha mpira wa miguu

sokwee

Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
49
Reaction score
13
Wana jamvi naomba ushauri mtt wangu ana kipaji cha mpira anatumia mguu wa kushoto hata waalimu wa shule anayosoma amenieleza kuhusu kipaji hicho sasa naomba ushauri nikuzeje kipaji chake na diet gani nimpe ili awe na nguvu akiwa mdogo?
 
Hicho kipaji anacho kweli au anarusha mateke tu? Maana bongo unaweza ukaambiwa kipaji kumbe mashakatu.

Kama ni kweli hasa hali yako ya kimaisha ipo vipi? Unaweza kusafiri nae ukampeleka UAE au Qatar majiribuni kwenye acadamy zakule? nakama akikosa udhamini kumlipia je utaweza?

Kwa bongo utajisumbua tu. Ukishindwa kupata mchongo wa Ulaya jaribu nchi za kiarabu kuwa sirius juu ya ilo.
Jaribu kuwa na focus ya mbali mkuu.
 
Asante mkuu kwa ushari wako hali yangu ya uchumi hairuhusu ila nitaongea nawatu mkuu
 
Ongea na club ya Southampton ndo timu ambayo sheria zao ni rafiki au Chelsea; inngia kwenye tovuti vyao kupata jinsi ya kuwasiliana nao.

Kuanzia Leo anza kuchua video akiwa anacheza na wenzake.
Ushauri mzuri sana

Amfungulie YouTube akaunti na kumrecord matukio yake.
 
Kibongo bongo atasanda baadae. Ulaya utasanda sa hivi ila mambo yakikaa fresh baadae wewe ni kucheka tu.

Mtoto wako ana umri gani.?
 
Asante mkuu kwa ushari wako hali yangu ya uchumi hairuhusu ila nitaongea nawatu mkuu

Na tafuta njia ya kutinga nae Ulaya hio ndio njia bora kabisa. Ikiwezekana ata kikataa cha urithi sijui bodaboda na kilichokaa mbele piga bei upotee nae.
 
maswali ya msingi, anacheza nafasi gani?
umbo lake likoje hasije kuwa kama kichuya kupata itakuwa issue
 
Nimemkumbuka neymar aisee yaani analambwa mapesa ambayo yanaweza ongoza wizara mbili za magu kwa mwaka mzima!!

Ila anza kwanza na academy za hapa tz na kama una uwezo mpeleke nje. Ila hakikisha kwanza anauweza mpira!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…