Ushauri na mawazo kuhusu biashara ya vijora na vitenge

Ushauri na mawazo kuhusu biashara ya vijora na vitenge

Mpombote

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
1,944
Reaction score
1,496
Habari wakuu! Jana katika mizunguko yangu nilitembelea k/koo mtaa wa sokoni kule nilienda kufanya utafiti kuhusu bei za Vijora vya Mombasa kwa ajili ya biashara na si mzoefu kwa hili ila bei niliyoikuta ni hii je ni sahihi au wapi naweza pata iliyopoa zaidi.

1. Vijora vyenye mtandio kwa 12000 jumla
2 Vijora bila mtandio 6000.jumla
3. Vijora vile vya Shiffon bila kamba 6000.jumla
4. Vijora vya shiffon na kamba 12000 jumla.

Nilijaribu pia kuuliza machinga wachache wa maeneo yale kuhusu hizi bei walijibu kwamba ni kweli mdo bei zao.

Baada ya hapo nikaelekea kitumbini moja kwa moja hapa nilienda angalia vitenge nilikutana na hali hii ya bei;-

1. Java zile za china zisizopauka bei 20000 hadi 19500 Jumla, hapa ni (oriental au Disco) kulingana na nilivoshauriwa na moja kati ya mfanya hii biashara kuwa hizi brand mbili ndo nzuri hasa hii ORIENTAL ila nikikosa hiyo basi ni DISCO.
2. Java no 2 ambazo ni brand nyingine au wanasema nyepesi bei ni 15000 hadi 14000 jumla.

3. Nikaja wax hapa sikujua brand gani ni nzuri ila kuna dada aliniambia ANGEL ndo haichuji na kupauka huwa inatoka china ambayo bei ni 21000 hadi 20000 jumla.

4. Wax no 2 ambazo hizi za moro na nyingine nyingi kuna za 10000 hadi 15000 jumla.

5. Vitenge vya kawaida nikakuta na vile vya pc 2 kwa bei ya 7000 kwingine 5000 kwingine 6000. Nikauliza urafiki wakasema saaa hivi haifanyi kazi ko hawana mzigo wake

Nimeleta hapa ili kama kuna yeyote anafahamu wapi ntapata mzigo mzuri kw bei nzuri zaidi pia napokea ushauri kipi kibaya kipi kizuri kabla ya kufanya maamuzi ya kuingiza pesa.Karibuni sana.
 
Nb, mzigo unauona kabisa kisha ndio unalipia
 
Kwanza kabisa tungejua unalenga soko la mkoa/jiji gani?
 
Hongera kwa utatifti ....mkuu mm ninatoa vijora mombasa naleta Tanzania ila siuzi rejareja nauza jumla , ni pm nikufikishie mzigo wako
Ungekua open kaka, kwenye biashara unatakiwa uwe wazi pia waweza kupata wateja wengine, sasa ukianza mambo ya pm sio kabisa, pia namshaur mfanya utafiti awe makini asije kutapeliwa maana pm c pazuri kabisa.
 
Ungekua open kaka, kwenye biashara unatakiwa uwe wazi pia waweza kupata wateja wengine, sasa ukianza mambo ya pm sio kabisa, pia namshaur mfanya utafiti awe makini asije kutapeliwa maana pm c pazuri kabisa
Haha sawa Mshauri usijali mi mwenyewe mtoto wa mjini ila naamini hana nia mbaya.
 
Hongera kwa utatifti. Mkuu mm ninatoa vijora mombasa naleta Tanzania ila siuzi rejareja nauza jumla, ni pm nikufikishie mzigo wako.
Samahani Mimi naomba unisaidie process za kufika huko Mombasa . Natamani niende mwenyewe naomba unielezee kidogo nijiandaaje.
 
Back
Top Bottom