Ushauri na Msaada wa kwenda masomoni Marekani

Ushauri na Msaada wa kwenda masomoni Marekani

Omba kujiunga na jeshi lao, uende ukaserve ukitoka kutumikia jeshi unapewa na uraia kabisa tofauti na wale wenzako wanaosoma ili baadae wafukuzie kazi itawachukua miaka zaidi ya kumi kupata uraia.

Ila wewe ukitoka zako kutumika jeshini ambazo huwa mission zake sio ndefu sana unapata nishani ya heshima na tuzo, malipo juu ya kuanza maisha plus uraia juu ukae unavyotaka.
fafanua hii mkuu
 
Acha nitie neno hapa. Mkuu kwanza nikupe shout out sana kwa hatua uliyofikia, nimeusoma uzi wako umenigusa sana!

Me nataka nikutie moyo keep moving! Usirudi nyuma wala kukata tamaa, nenda mbele mwanangu huwezijua labda huko ndipo yalipo mafanikio yako. Hiyo scholarship ndio link ya kupata kazi.


NB: watu wema bado wapo kwenye hii Dunia yetu na ndio hao wanaishikiria Dunia kwa Imani zao na maombi yao kwa Mungu ili asije kuiangamiza tena kwa dhambi zetu tunazokufuru kila siku, otherwise ingeshatokea kama gharika au sodoma & gomora
 
Acha nitie neno hapa. Mkuu kwanza nikupe shout out sana kwa hatua uliyofikia, nimeusoma uzi wako umenigusa sana!

Me nataka nikutie moyo keep moving! Usirudi nyuma wala kukata tamaa, nenda mbele mwanangu huwezijua labda huko ndipo yalipo mafanikio yako. Hiyo scholarship ndio link ya kupata kazi.


NB: watu wema bado wapo kwenye hii Dunia yetu na ndio hao wanaishikiria Dunia kwa Imani zao na maombi yao kwa Mungu ili asije kuiangamiza tena kwa dhambi zetu tunazokufuru kila siku, otherwise ingeshatokea kama gharika au sodoma & gomora
Ahsante sana Mkuu, nashukuru sana kwa ushauri wako, sitarudi nyuma abadan, ikiwa nimevumilia suluba za mashariki ya kati, Marekani sitashindwa,Mungu atakuwa nami.
 
1. F1 utafanya kazi on campus ya chuo chako au kama utapata connection ufanye undercover mtaani.
2. A na B ni majibu, itategemea
3. Bank statement iliyoshiba, unafikia wapi( I hope ni on- campus ya chuo), maswali mengine yanategemea na siku + anaekuhoji
4. Elimu ni oversaturated but why usomee dini?
NB; pole kwa masaibu ila mi naona kama una insufficient funds ni heri uvumilie hapa tu, kikawaida US si mchezo unless unaenda Nebraska huko
Una akili kichwani kweli? Au kichwa kimebeba meno tu?
 
Mungu akuongoze.

Pia naomba nielekeze namna ya kuomba hizo scholarship.
Nenda Youtube kuna huyo jamaa IBM scholar kila kitu kipo hapo, weka bundle lako GB 1 tulia huko download hizo video na audio clip.

Wabongo wengi bado internet haiwasaidii kwa sababu wanatumia muda mwingi kwenye hizi site za chatting tu na umbea.
 
Wakuu salaam,

Awali ya yote namshukuru sana M. Mungu kwa nafasi hii adhmu niliyobahatika kupata. Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikihangaika kuboresha maisha yangu ndani na nje ya nchi.

Mara tu baada ya kuhitimu tu masomo ya elimu ya juu, niliamua kusafiri kwenda bara la Asia nchi za Gulf kutafuta maisha, nikakaa huko kwa kipindi cha miaka miwili nikifanya vibarua vya hapa na pale hadi COVID-19 ilipoanza nikaamua kurejea nchini.

Nikafika na nikaanza maisha, maambukizi yalipopungua na mipaka kuanza kufunguliwa tena, nilijaribu mara nyingi sana kurudi kwenye kibarua changu bila mafanikio, sababu kuu ilikuwa ni kukoswa chanjo - utakumbuka wakati huo uongozi ulikuwa tofauti na huu tulionao leo (utofauti wa sera). Mwisho nikapoteza kibarua changu.

Nikakutana na changamoto kubwa ya maisha baada ya miezi kadhaa tu kupita, nikaanza kuishiwa pesa,maana sehemu ya kipato changu nilikuwa nikitumia kuhudumia wazazi na wadogo zangu wawili waliokuwa masomoni elimu juu. Wamehitimu wote, wapo nyumbani hawana kazi pia.

Baada ya kusota, nikaamua kiasi kile nilichobakiza (nilichokuwa napanga kutumia kwa ajili ya safari) nikiweke biashara, nikachukua pesa nikaweka kwenye biashara, biashara ikafa kabisa bila kupata faida yoyote.

Baada ya hapo, kuanzia mwaka jana mwezi wa tano, nikawa sina chochote kabisa hata hela ya kununua bundle.

Kidogo kidogo nikaanza kupoteza marafiki na jamaa zangu, hata wale niliokuwa nawasaidia wakanidharau kabisa, sikuwa chochote kabisa mbele zao.

Nikakataa tamaa kabisa, maana hata mpenzi wangu,niliempenda sana, niliyetaka kumuoa akaniacha akaolewa na mtu mwingine, sikuwa tena na uwezo wa kumtimizia mahitaji,na wakati alipohitaji ndoa,ndio kabisa mimi hata pesa ya kujihudumia mwenyewe sina, nikabaki mwenyewe.

Nikatoka mjini, nikaamua kurudi nyumbani wazazi wakanipa moyo sana, lakini baadae mambo yakabadilika, kwa ndugu zangu sikuwa na ile heshima niliyokuwa nayo mwanzoni,kila mtu nikaona anajitenga na mimi,nikadharaulika wakawa wananiita mchizi wa Bongo ( In Alikiba's voice).

Mwanzoni mwa mwaka huu, nikifanya maamuzi mugumu, nikaamua nitoke nyumbani, baada ya kukaa huko miezi kadhaa, nikaenda mjini kwa mshikaji, bila kuwa na sent mfukoni, jamaa akanipokea maisha yakaanza, tukipata tunakula tukikoswa tunalala.(Mungu ambariki sana huyu jamaa).

Baadae nikapata wazo, nikasema kwa namna yoyote lazima nitoke hii nchi, nikaamua niende Canada au USA, mwisho wa siku baada ya kutafiti sana nakaamua USA will be the best option.

Nikaamua kuwa niuze eneo langu, ambalo nilinunua wakati nikiwa nje, nikauza japo kwa bei ya kutupa, nikampatia mshikaji aliyenipokea Tsh 500K (nilimpatia maana maisha yake ni magumu sana na kwa kipindi nikiwa pale alinipambana sana kuhakikisha mkono unaenda kinywani, so nilimpatia kama shukran).

Nikabaki na 1.5 M, nikasafiri kuelekea Dar, huko nina mshikaji mwingine, kufika Dar mradi nina pesa nikatafuta wakala (Agent) wa kazi za Arabia (Qatar), nikaenda ofisini kwake Kariakoo, tukaandikishana, nika submit documents alizohitaji pamoja na agency fee 500K. Akaanza kunizungusha sana mwisho wa siku nikajua tu nimepigwa[emoji4], nikamshukuru Mungu, nika move on, mfukoni ikabaki 900K.

Nikasema ngoja nipambane niende US kama wazo langu la kwanza lilivyokuwa, nikamshirikisha mshikaji akaanza niambia kuwa naanza kuchanganyikiwa maana Nina waza mawazo nisiyo endana nayo, nikapiga kimya nikaamua nifanye kimya kimya, nikamua niombe visa ya kwenda masomoni baada ya kupata ushauri wa jamaa mmoja humu jukwaani, nikiwa huko kila kitu kitafunguka.

Nikaanza kuomba vyuo kwa fujo, kuanzia, course zote nilizoona nina vigezo, NOTE; lengo sio kusoma TU ila nikiwa nasoma niwe nafanya KAZI na baada ya masomo nitengeneze mazingira mazuri ya kubaki.

Mwezi wa 3 mwishoni, nikaomba vyuo sita, nikalipa application fees, ina range from 50 - 65 USD per university, nikaishiwa pesa nikakaa sasa kusubiri majibu.

Majibu yakaanza kutoka, chuo cha kwanza nimekoswa, cha pili nimekoswa, cha tatu vivyo hivyo, cha nne nimekoswa pia . Nikahisi kuchanganyikiwa, nikawa nimepoteza kila kitu, nikasema hapa nachanganyikiwa sio muda mrefu, nikawa mtu wa kujitenga tu na kulala tu, nawaza kufa kufa tu. Kumwambia rafiki yangu siwezi, maana sikumshirikisha, nikabaki kulia na Mungu wangu.

Sababu kuu iliyosababisha nikoswe nilikuwa naomba, nikilipa pesa mwisho kabisa kwenye application checklist, wananiambia nitume jaribio la ujuzi wa lugha (English Language Proficiency Test - mojawapo kati ya IELTS, DUOLINGO na TOEFL) tafrani ikawa hapa, maana pesa ya kufanya IELTS pekee inaanzia 700K (laki saba) na pia wakataka niwatumie matokeo yangu ya undergraduate kwa kupita wakala ( WES - course by course evaluation ) ambao gharama zake ni 300K.

Nikaendelea hivyo hivyo, mwisho kabisa, namshukuru Mungu vyuo viwili vilivyobaki vimenikubalia, tayari vimenitumia ADMISSION LETTER na I - 20 FORM kwa ajili ya kwenda kuchukua Visa - US EMBASSY.

Vyuo vyote nimepata partial Scholarship, moja ya Masters ya masomo ya DINI na nyingine ni masuala ya ELIMU, sasa nipo kwenye kuhangaika pesa kwa ajili ya visa, nauli na mambo mengine ya safari. Natakiwa kuwa MAREKANI kabla ya 16 August.

Napenda kutumia fursa hii kuwauliza wajuzi wa mambo, kunisaidia yafuatayo.

JE,

1. F 1 visa itaniruhusuruhu kufanya kazi halali?

2. Naweza kwenda USA na kufanikiwa kwa kutumia Partial Scholarship? wakati nikipambana kujilipia sehemu inayobakia kwa kufanya kazi?.(maana uchumi wangu umeyumba mno).

3. Ni vitu gani natakiwa kuzingatia wakati wa kwenda kuomba visa, ili niwe na uhakika wa kupata?

4. Nichague kusoma Masters ipi ya DINI au ELIMU? itakayonifanya nifanikiwe?

Karibuni kwa ushauri na msaada wowote tafadhali.
Mpaka hapo upo mguu mmoja ndani ya Marekani, nitasikitika sana kama utakosa viza kwa hatua hii iliyobaki ya bank statement ya mtu wa kukusponsor.

Ukiona siku zinakimbia bado haujafanikiwa kupata kampuni au mtu wa kukusponsor nitafute pm yangu iko wazi.
 
Nenda Youtube kuna huyo jamaa IBM scholar kila kitu kipo hapo, weka bundle lako GB 1 tulia huko download hizo video na audio clip.

Wabongo wengi bado internet haiwasaidii kwa sababu wanatumia muda mwingi kwenye hizi site za chatting tu na umbea.
Ahsante sana Mkuu, nimeanza kumfuatilia tangu jana, kweli kuna mambo mengi nimepata, nashukuru mno.
 
Mpaka hapo upo mguu mmoja ndani ya Marekani, nitasikitika sana kama utakosa viza kwa hatua hii iliyobaki ya bank statement ya mtu wa kukusponsor.

Ukiona siku zinakimbia bado haujafanikiwa kupata kampuni au mtu wa kukusponsor nitafute pm yangu iko wazi.
Nafurahi sana kupata watu wanaotia moyo kama wewe, ubarikiwe popote ulipo.
 
simamia lengo lako mkuu na pole kwa yaliyokukuta mimi naona Elimu ni nzuri zaidi endapo utarudi hapa kwetu Tanzania utapata kwa kushika, dini kumbuka kwamba nchi yetu haiamini masuala ya kidini kwa hiyo kutoboa ni ishu
 
Iko hivyo Kaka Kwa mana tafuta mtu benki NMB or.... Mpe akugushie statement au wamsingizie doni mmoja kama ndo sponsa wa masomo yako. Ili hapo ubalozi I wasikusmbue.. Haiwezekan useme utaenda kujisomesha mwenyew alafu wakuulize una kias gani benki useme una laki 2. Hutapew visa mkuu na vipi kuhusu NOC!?

Sent from my VTR-L29 using JamiiForums mobile app
umempa wazo zuri mimi nilishindwa kulitumia hili nilipopata nafasi ya kusoma Cardiff nchini UK walitaka niwe na account kutoka kwa sponsor wangu isiyopungua 25mil nikashindwa kwa kigezo hicho
 
Nenda Youtube kuna huyo jamaa IBM scholar kila kitu kipo hapo, weka bundle lako GB 1 tulia huko download hizo video na audio clip.

Wabongo wengi bado internet haiwasaidii kwa sababu wanatumia muda mwingi kwenye hizi site za chatting tu na umbea.
Kwanza jamaa anaitwa EBM na siyo IBM,jamaa huyu anaongea mambo mengi sana lakn yote ni magumu sana kwa wa Tz,anaongelea scholarship zenye masharti ya IELTS na TOEF yaani kiufupi yupo more complicated sana hana plan B kabisa.
 
Back
Top Bottom