mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,586
- 11,227
Mkuu tafuta mawasiliano ya Roma mkatoliki in case of any emergency
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23]Mkuu tafuta mawasiliano ya Roma mkatoliki in case of any emergency
Ahsante ndugu yangu.mungu akusimamie sana uko bro maana story yako inafundisha sana
Wakuu salaam,
Awali ya yote namshukuru sana M. Mungu kwa nafasi hii adhmu niliyobahatika kupata. Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikihangaika kuboresha maisha yangu ndani na nje ya nchi.
Mara tu baada ya kuhitimu tu masomo ya elimu ya juu, niliamua kusafiri kwenda bara la Asia nchi za Gulf kutafuta maisha, nikakaa huko kwa kipindi cha miaka miwili nikifanya vibarua vya hapa na pale hadi COVID-19 ilipoanza nikaamua kurejea nchini.
Nikafika na nikaanza maisha, maambukizi yalipopungua na mipaka kuanza kufunguliwa tena, nilijaribu mara nyingi sana kurudi kwenye kibarua changu bila mafanikio, sababu kuu ilikuwa ni kukoswa chanjo - utakumbuka wakati huo uongozi ulikuwa tofauti na huu tulionao leo (utofauti wa sera kuhusu COVID). Mwisho nikapoteza kibarua changu.
Nikakutana na changamoto kubwa ya maisha baada ya miezi kadhaa tu kupita, nikaanza kuishiwa pesa,maana sehemu ya kipato changu nilikuwa nikitumia kuhudumia wazazi na wadogo zangu wawili waliokuwa masomoni elimu ya juu. Wamehitimu wote, wapo nyumbani hawana ajira pia.
Baada ya kusota, nikaamua kiasi kile nilichobakiza (nilichokuwa napanga kutumia kwa ajili ya safari) nikiweke katika biashara, nikachukua pesa nikaweka kwenye biashara, biashara ikafa kabisa bila kupata faida yoyote.
Baada ya hapo, kuanzia mwaka jana mwezi wa tano, nikawa sina chochote kabisa hata hela ya kununua bundle.
Kidogo kidogo nikaanza kupoteza marafiki na jamaa zangu, hata wale niliokuwa nawasaidia wakanidharau kabisa, sikuwa chochote kabisa mbele zao.
Nikakataa tamaa kabisa, maana hata mpenzi wangu,niliempenda sana, niliyetaka kumuoa akaniacha akaolewa na mtu mwingine, sikuwa tena na uwezo wa kumtimizia mahitaji,na wakati alipohitaji ndoa,ndio kabisa mimi hata pesa ya kujihudumia mwenyewe sina, nikabaki mwenyewe.
Nikatoka mjini, nikaamua kurudi nyumbani wazazi wakanipa moyo sana, lakini baadae mambo yakabadilika, kwa ndugu zangu sikuwa na ile heshima niliyokuwa nayo mwanzoni,kila mtu nikaona anajitenga na mimi,nikadharaulika wakawa wananiita mchizi wa Bongo ( In Alikiba's voice).
Mwanzoni mwa mwaka huu, nikifanya maamuzi mugumu, nikaamua nitoke nyumbani, baada ya kukaa huko miezi kadhaa, nikaenda mjini kwa mshikaji, bila kuwa na sent mfukoni, jamaa akanipokea maisha yakaanza, tukipata tunakula tukikoswa tunalala.(Mungu ambariki sana huyu jamaa).
Baadae nikapata wazo, nikasema kwa namna yoyote lazima nitoke hii nchi, nikaamua niende Canada au USA, mwisho wa siku baada ya kutafiti sana nakaamua USA will be the best option baada ya kuangalia baadhi ya facts.
Nikaamua kuwa niuze eneo langu, ambalo nilinunua wakati nikiwa nje, nikauza japo kwa bei ya kutupa, nikampatia mshikaji aliyenipokea Tsh 500K (nilimpatia maana maisha yake ni magumu sana na kwa kipindi nikiwa pale alinipambana sana kuhakikisha mkono unaenda kinywani, so nilimpatia kama shukran).
Nikabaki na 1.5 M, nikasafiri kuelekea Dar, huko nina mshikaji mwingine, kufika Dar mradi nina pesa nikatafuta wakala (Agent) wa kazi za Arabia (Qatar), nikaenda ofisini kwake Kariakoo, tukaandikishana, nika submit documents alizohitaji pamoja na agency fee 500K. Akaanza kunizungusha sana mwisho wa siku nikajua tu nimepigwa[emoji4], nikamshukuru Mungu, nika move on, mfukoni ikabaki 900K.
Nikasema ngoja nipambane niende US kama wazo langu la kwanza lilivyokuwa, nikamshirikisha mshikaji akaanza niambia kuwa naanza kuchanganyikiwa maana nina waza mawazo nisiyo endana nayo, nikapiga kimya nikaamua nifanye kimya kimya, nikamua nitakayoomba iwe ni visa ya kwenda masomoni baada ya kupata ushauri wa jamaa mmoja humu jukwaani, nikiwa huko kila kitu kitafunguka.
Nikaanza kuomba vyuo kwa fujo, kuanzia, course zote nilizoona nina vigezo, NOTE; lengo sio kusoma TU ila nikiwa nasoma niwe nafanya KAZI na baada ya masomo nitengeneze mazingira mazuri ya kubaki.
Mwezi wa 3 mwishoni, nikaomba vyuo sita, nikalipa application fees, ina range from 50 - 65 USD per university, nikaishiwa pesa nikakaa sasa kusubiri majibu.
Majibu yakaanza kutoka, chuo cha kwanza nimekoswa, cha pili nimekoswa, cha tatu vivyo hivyo, cha nne nimekoswa pia . Nikahisi kuchanganyikiwa, nikawa nimepoteza kila kitu, nikasema hapa nachanganyikiwa sio muda mrefu, nikawa mtu wa kujitenga tu na kulala tu, nawaza kufa kufa tu. Kumwambia rafiki yangu siwezi, maana sikumshirikisha, nikabaki kulia na Mungu wangu.
Sababu kuu iliyosababisha nikoswe nilikuwa naomba, nikilipa pesa mwisho kabisa kwenye application checklist, wananiambia nitume jaribio la ujuzi wa lugha (English Language Proficiency Test - mojawapo kati ya IELTS, DUOLINGO na TOEFL) tafrani ikawa hapa, maana pesa ya kufanya IELTS pekee inaanzia 700K (laki saba) na pia wakataka niwatumie matokeo yangu ya undergraduate kwa kupita wakala ( WES - course by course evaluation ) ambao gharama zake ni 300K.
Nikaendelea hivyo hivyo, mwisho kabisa, namshukuru Mungu vyuo viwili vilivyobaki vimenikubalia, tayari vimenitumia ADMISSION LETTER na I - 20 FORM kwa ajili ya kwenda kuombea Visa - US EMBASSY.
Vyuo vyote nimepata partial Scholarship, moja ya Masters ya masomo ya DINI na nyingine ni masuala ya ELIMU, sasa nipo kwenye kuhangaika pesa kwa ajili ya visa, nauli na mambo mengine ya safari. Natakiwa kuwa MAREKANI kabla ya 16 August.
Napenda kutumia fursa hii kuwauliza wajuzi wa mambo, kunisaidia yafuatayo.
JE,
1. F 1 visa itaniruhusuruhu kufanya kazi halali?
2. Naweza kwenda USA na kufanikiwa kwa kutumia Partial Scholarship? wakati nikipambana kujilipia sehemu inayobakia kwa kufanya kazi?.(maana uchumi wangu umeyumba mno).
3. Ni vitu gani natakiwa kuzingatia wakati wa kwenda kuomba visa, ili niwe na uhakika wa kupata?
4. Nichague kusoma Masters ipi ya DINI au ELIMU? itakayonifanya nifanikiwe?
Karibuni kwa ushauri na msaada wowote tafadhali.
Dahh..we jamaa hongera Sana,nawaza ndugu walokutenga na washakji walokukimbia plus mchumba wakiskia umefika US watakua na Hali gani?pole sanaNavumiliaje hapa, nikiwa na insufficiency fund Mkuu, ngoja niende mbele sijui safari yangu itanipa nini lakini naamini Mungu atakuwa nami.
Ahsante sana MkuuDahh..we jamaa hongera Sana,nawaza ndugu walokutenga na washakji walokukimbia plus mchumba wakiskia umefika US watakua na Hali gani?pole sana
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mkuu Maisha yapoje hapo USAAhsante sana Mkuu
Namshukuru Mungu mkuu,kijumla maisha sio mabaya japo yana ughali kutofatisha na kwetu.Mkuu Maisha yapoje hapo USA
Mimi leo Kesho nataka nije kuishi huko
Mkuu kama umekwama bado weka bank details tukuchangie japo hela ya majiAhsante sana Mkuu, nashukuru sana kwa ushauri wako, sitarudi nyuma abadan, ikiwa nimevumilia suluba za mashariki ya kati, Marekani sitashindwa,Mungu atakuwa nami.
Mkuu Mungu akubariki sana, niko hapa nasoma huu ushauri wako leo nikiwa USA, nina amani kabisa na furaha, yote uliyoniombea naona yanatokea, Mungu akubariki nawe sana.Acha nitie neno hapa. Mkuu kwanza nikupe shout out sana kwa hatua uliyofikia, nimeusoma uzi wako umenigusa sana!
Me nataka nikutie moyo keep moving! Usirudi nyuma wala kukata tamaa, nenda mbele mwanangu huwezijua labda huko ndipo yalipo mafanikio yako. Hiyo scholarship ndio link ya kupata kazi.
NB: watu wema bado wapo kwenye hii Dunia yetu na ndio hao wanaishikiria Dunia kwa Imani zao na maombi yao kwa Mungu ili asije kuiangamiza tena kwa dhambi zetu tunazokufuru kila siku, otherwise ingeshatokea kama gharika au sodoma & gomora
Wakuu salaam,
Awali ya yote namshukuru sana M. Mungu kwa nafasi hii adhmu niliyobahatika kupata. Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikihangaika kuboresha maisha yangu ndani na nje ya nchi.
Mara tu baada ya kuhitimu tu masomo ya elimu ya juu, niliamua kusafiri kwenda bara la Asia nchi za Gulf kutafuta maisha, nikakaa huko kwa kipindi cha miaka miwili nikifanya vibarua vya hapa na pale hadi COVID-19 ilipoanza nikaamua kurejea nchini.
Nikafika na nikaanza maisha, maambukizi yalipopungua na mipaka kuanza kufunguliwa tena, nilijaribu mara nyingi sana kurudi kwenye kibarua changu bila mafanikio, sababu kuu ilikuwa ni kutokuwepo kwa chanjo ya COVID-19 nchi - utakumbuka wakati huo uongozi ulikuwa tofauti na huu tulionao leo (utofauti wa sera kuhusu COVID). Mwisho nikapoteza kibarua changu.
Nikakutana na changamoto kubwa ya maisha baada ya miezi kadhaa tu kupita, nikaanza kuishiwa pesa,maana sehemu ya kipato changu nilikuwa nikitumia kuhudumia wazazi na wadogo zangu wawili waliokuwa masomoni (Elimu ya juu). Kwa sasa wamehitimu wote, wapo nyumbani hawana ajira pia.
Baada ya kusota, nikaamua kiasi kile nilichobakiza (nilichokuwa napanga kutumia kwa ajili ya safari) nikiweke katika biashara, nikachukua pesa nikaweka kwenye biashara, biashara ikafa kabisa bila kupata faida yoyote.
Baada ya hapo, kuanzia mwaka jana mwezi wa tano, nikawa sina chochote kabisa hata hela ya kununua bundle.
Kidogo kidogo nikaanza kupoteza marafiki na jamaa zangu, hata wale niliokuwa nawasaidia wakanidharau kabisa, sikuwa chochote kabisa mbele yao.
Nikakataa tamaa kabisa, maana hata mpenzi wangu,niliempenda sana, niliyepanga kumuoa akaniacha akaolewa na mtu mwingine, sikuwa tena na uwezo wa kumtimizia mahitaji,na wakati alipohitaji ndoa,ndio kabisa mimi hata pesa ya kujihudumia mwenyewe sina, nikabaki mwenyewe.
Nikatoka mjini, nikaamua kurudi nyumbani wazazi wakanipa moyo sana, lakini baadae mambo yakabadilika, kwa ndugu zangu sikuwa na ile heshima niliyokuwa nayo mwanzoni,kila mtu nikaona anajitenga na mimi,nikadharaulika wakawa wananiita mchizi wa Bongo ( In Alikiba's voice).
Mwanzoni mwa mwaka huu, nikifanya maamuzi magumu, nikaamua nitoke nyumbani, baada ya kukaa huko miezi kadhaa, nikaenda mjini kwa mshikaji, bila kuwa na sent mfukoni, jamaa akanipokea maisha yakaanza, tukipata tunakula tukikoswa tunalala.(Mungu ambariki sana huyu jamaa).
Baadae nikapata wazo, nikasema kwa namna yoyote lazima nitoke hii nchi, nikaamua niende Canada au USA, mwisho wa siku baada ya kutafiti sana nakaamua USA will be the best option baada ya kuangalia baadhi ya facts.
Nikaamua kuwa niuze eneo langu, ambalo nilinunua wakati nikiwa nje, nikauza japo kwa bei ya kutupa, nikampatia mshikaji aliyenipokea Tsh 500K (nilimpatia maana maisha yake ni magumu sana na kwa kipindi nikiwa pale alinipambana sana kuhakikisha mkono unaenda kinywani, so nilimpatia kama shukran).
Nikabaki na 1.5 M, nikasafiri kuelekea Dar, huko nina mshikaji mwingine, kufika Dar mradi nina pesa nikatafuta wakala (Agent) wa kazi za Arabia (Qatar), nikaenda ofisini kwake Kariakoo, tukaandikishana, nika submit documents alizohitaji pamoja na agency fee 500K. Akaanza kunizungusha sana mwisho wa siku nikajua tu nimepigwa[emoji4], nikamshukuru Mungu, nika move on, mfukoni ikabaki 900K.
Nikasema ngoja nipambane niende USA kama wazo langu la kwanza lilivyokuwa, nikamshirikisha mshikaji akaanza niambia kuwa naanza kuchanganyikiwa maana nina waza mawazo nisiyo endana nayo, nikapiga kimya nikaamua nifanye kimya kimya, nikamua aina ya visa nitakayoomba iwe ni visa ya kwenda masomoni baada ya kupata ushauri wa jamaa mmoja humu jukwaani, nikiwa huko kila kitu kitafunguka.
Nikaanza kuomba vyuo kwa fujo, course zote nilizoona nina vigezo, NOTE; lengo sio kusoma TU ila nikiwa nasoma niwe nafanya KAZI na baada ya masomo nitengeneze mazingira mazuri ya kubaki.
Mwezi wa 3 mwishoni, nikaomba vyuo sita, nikalipa application fees, ina range from 50 - 65 USD per university, nikaishiwa pesa nikakaa sasa kusubiri majibu.
Majibu yakaanza kutoka, chuo cha kwanza nimekosa, cha pili nimekosa, cha tatu vivyo hivyo, cha nne nimekosa pia . Nikahisi kuchanganyikiwa, nikawa nimepoteza kila kitu, nikasema hapa nachanganyikiwa sio muda mrefu, nikawa mtu wa kujitenga tu na kulala tu, nawaza kufa kufa tu. Kumwambia rafiki yangu siwezi, maana sikumshirikisha, nikabaki kulia na Mungu wangu.
Sababu kuu iliyosababisha nikose nilikuwa naomba, nikilipa pesa mwisho kabisa kwenye application checklist, wananiambia nitume jaribio la ujuzi wa lugha (English Language Proficiency Test - mojawapo kati ya IELTS, DUOLINGO na TOEFL) tafrani ikawa hapa, maana pesa ya kufanya IELTS pekee inaanzia 700K (laki saba) na pia wakataka niwatumie matokeo yangu ya undergraduate kwa kupita wakala ( WES - course by course evaluation ) ambao gharama zake ni 300K.
Nikaendelea hivyo hivyo, mwisho kabisa, namshukuru Mungu vyuo viwili vilivyobaki vimenikubalia, tayari vimenitumia ADMISSION LETTER na I - 20 FORM kwa ajili ya kwenda kuombea Visa - US EMBASSY.
Vyuo vyote nimepata partial Scholarship, moja ya Masters ya masomo ya DINI na nyingine ni masuala ya ELIMU, sasa nipo kwenye kuhangaika pesa kwa ajili ya visa, nauli na mambo mengine ya safari. Natakiwa kuwa MAREKANI kabla ya 16 August.
Napenda kutumia fursa hii kuwauliza wajuzi wa mambo, kunisaidia yafuatayo.
JE,
1. F 1 visa itaniruhusuruhu kufanya kazi halali?
2. Naweza kwenda USA na kufanikiwa kwa kutumia Partial Scholarship? wakati nikipambana kujilipia sehemu inayobakia kwa kufanya kazi?.(maana uchumi wangu umeyumba mno).
3. Ni vitu gani natakiwa kuzingatia wakati wa kwenda kuomba visa, ili niwe na uhakika wa kupata?
4. Nichague kusoma Masters ipi ya DINI au ELIMU? itakayonifanya nifanikiwe?
Karibuni kwa ushauri na msaada wowote tafadhali.
Upo outdated, mshkaji viza alishatusuwa na yupo Marekani tangu mwaka Jana.I have been to USA many times, kama hauna ties zozote za mke na ndugu na marafiki nenda USA.
Ukifika USA jimbo lolote hata kama huna lolote utasogea tu, cha maana usiwe na aibu. Hata kama huna pa kulala.
Cha maana.
- Ukifika tafuta wa Tanzania, wapo wengi na hukutana mara nyingi, elezea hali yako.
- Jitahidi sana kuwa active member Kanisan kwa Imani kabisa au kwa dini yako yeyote.
- Usiwe omba omba kabisa, yani kaa kiume, ukishibana na mtu sana ndo umweleze shida zako.
Kwa maelezo yako, changamoto kubwa nayoiona kwako ni kupata visa kwa mazingira yako ya kudunduliza.
Na visa sio fee tu, ni uwezo wako wa kueleze na uhalisia wa financials zako, mfano: Your Bank statement.
Shukuru Mungu unayapitia haya una mle wala mtoto, ungekuwa nao ni story ingine kabisa.
Mungu ni mwema hajawahi kumtupa yeyote mwenye bidii na Imani.
Ahsante sana Mkuu, kwa sasa namshukuru Mungu, ahsante kwa concern yako.Mkuu kama umekwama bado weka bank details tukuchangie japo hela ya maji
Mkuu nilifuata hii njia ulivyonishauri, hawa watu wamekuwa wema mno kwangu, Mungu yupo aisee, Mungu yupo, in short leo nimeona nifanye Personal Reflection kupitia hii thread ili kuniongezea hamasa zaidi ya kupambana, kujua na kukumbuka ulipotoka (siku mbaya ulizopitia) ni hatua bora ya kukumbuka ni nini unapaswa ufanye.Wewe hauko well informed, dini hasa makanisa ndio biashara inayolipa sana kwa sasa na haina hasara, weww wajaze hofu kondoo tu kuhusu mbinguni ingawa hujawahi kufika utasambaziwa upendo.
Yule muhindi wa Agape Fernandes pesa za sadaka amefanikiwa kumsomesha mtoto wake chuo bora kabisa Marekani na sasa anamiliki App ya Nala.
So sad, mnaishi vipi mjini mpaka mnakwama kwa kitu kama hiki?
Ahsante Mkuu, nashukuru sana kwa huu ushauri bado naweza kuufanyia kazi hata huku niliko, nimefika US nina almost nusu mwaka sasa, naendelea vizuri kabisa Mungu amekuwa mwema kwangu, namshukuru.I have been to USA many times, kama hauna ties zozote za mke na ndugu na marafiki nenda USA.
Ukifika USA jimbo lolote hata kama huna lolote utasogea tu, cha maana usiwe na aibu. Hata kama huna pa kulala.
Cha maana.
- Ukifika tafuta wa Tanzania, wapo wengi na hukutana mara nyingi, elezea hali yako.
- Jitahidi sana kuwa active member Kanisan kwa Imani kabisa au kwa dini yako yeyote.
- Usiwe omba omba kabisa, yani kaa kiume, ukishibana na mtu sana ndo umweleze shida zako.
Kwa maelezo yako, changamoto kubwa nayoiona kwako ni kupata visa kwa mazingira yako ya kudunduliza.
Na visa sio fee tu, ni uwezo wako wa kueleze na uhalisia wa financials zako, mfano: Your Bank statement.
Shukuru Mungu unayapitia haya una mle wala mtoto, ungekuwa nao ni story ingine kabisa.
Mungu ni mwema hajawahi kumtupa yeyote mwenye bidii na Imani.
Mpaka December kibubu chako cha part time job kitakuwa kimejaa, usinisahau kunitumia ya ugolo ili Nile matunda ya free consultation, au siku hizi wanaita sadaka.Mkuu nilifuata hii njia ulivyonishauri, hawa watu wamekuwa wema mno kwangu, Mungu yupo aisee, Mungu yupo, in short leo nimeona nifanye Personal Reflection kupitia hii thread ili kuniongezea hamasa zaidi ya kupambana, kujua na kukumbuka ulipotoka (siku mbaya ulizopitia) ni hatua bora ya kukumbuka ni nini unapaswa ufanye.
Sawa MkuuMpaka December kibubu chako cha part time job kitakuwa kimejaa, usinisahau kunitumia ya ugolo ili Nile matunda ya free consultation, au siku hizi wanaita sadaka.