USHAURI: Nafikiria kufungua duka la Vitasa tu Arusha mjini

USHAURI: Nafikiria kufungua duka la Vitasa tu Arusha mjini

Trust me, utatengeneza pesa sana, hakikisha tu una deal na mlango wote, accessories za mlango zote.
√ Vitasa vya milango ya mbao na mageti, kuanzia low quality to the highest quality.
√ Makomeo yote ya sizes zote
√ Bawaba sizes zote, Bawaba za milango ya mbao na zile za mageti...uwe na za kichina na hizi za Sido/Tanzania.
√Tairi za mageti sizes zote na rollers zake.
√ Kufuli sizes zote na ubora wote.
√ Uza pia discs za kukatia chuma na kunolea chuma.
Boss ushawahi Fanya biashara ya kufuli ,samahani
 
Boss ushawahi Fanya biashara ya kufuli ,samahani
Kuna kipindi nilifanya, ila sio kufuli kama kufuli mkuu(ilikuwa mini hardware). Ukiwa na mtaji mdogo ni risk kuwekeza kwa kitu kimoja tu.
 
We angalia biashara kubwa zilizofika mbali Wana bidhaa ngapi madukani kwao
Siku hata mabucha hawauzi nyama ya ng'ombe tu bali utakuta mbuzi, samaki, kuku na hata pweza
Bidhaa moja tu labda mahindi ya kuchoma
 
Kuna kipindi nilifanya, ila sio kufuli kama kufuli mkuu(ilikuwa mini hardware). Ukiwa na mtaji mdogo ni risk kuwekeza kwa kitu kimoja tu.
Mimi nafanyaga ,sema sijui machimbo yakupata mzigo kwa bei nzuri sana ,na mtaji nao unanisumbua sana....ni mdogo.
 
Back
Top Bottom