Ushauri: Nahitaji dawa ya kuondoa upara (uwalaza)

Delacruzito

Senior Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
123
Reaction score
141
Habari zenu wana JF

Poleni sana na Swaumu naimani tunaendelea na Mfungo Mtukufu wa Ramadhani

Ndugu zangu nina miaka 25 Mzee wangu ana Uwaraza kwa Mbele hapa ule wanauita Upara wa Pesa. Sasa naona kama nimerithi kwake na maana nywele zangu za hapa Mbele zinakatika zinakua fupi kuliko nyingine halafu nikijiamgalia kwenye kioo naanza kuona ile Ngozi za kichwa kwa mbali.

So, wanadugu jamani kwa yeyete mwenye anajua dawa ya kutibu upara au uwaraza kwa njia yeyote ile iwe ni kwa kutumia dawa za asili ama kama kuna mafuta ya kununua ya kupaka please naombeni mnisaidie[emoji1488][emoji1488]

1619891930151.png

Kama ni Genetics huwezi kuuzuia, japo unaweza kupunguza kasi yaa nywele kukatika. Njia sahihi ni kwamba tafuta vitunguu maji uvisage, vichuje na paka yale maji yake sehemu ambayo nywele zinakatika. AU utafute tui la nazi likiwa la vuguvugu unapaka sehemu iliyoharibika. AU chukua mayai mabichi changanya na mafuta ya mizeituni kisha paka kichwani. Fanya hili zoezi usiku muda wa wiki mbili hadi tatu.

Angalizo: Uwe na Shampoo ya kuoshea kichwa ili kutoa harufu za mayai, vitunguu na nazi. Lakini kubwa zaidi punguza mawazo na hakikisha unapata muda mwingi wa kulala....
 
Sawa mkuu And inawezekana Depression inachangia pia maana
 
Upara wa pesa hio siku hizi labda, zamani tunaita Airport hio.

Turudi kwenye mada, dawa ya asili ya kiuwaraza ni kunyoa kipara.

Dawa za kisasa zipo nyingi tu unaweza kuvaa wig au tafuta dawa inaitwa Minoxidil.

Kila la kheri

Pamoja mkuu
 
Ndugu kwa ushauri wangu usijiangaishe kutafuta madawa hutoweza. Hiko kipata ni cha kurithi nikama ulivyorithi baadhi ya vitu mfano rangi, urefu, ndevu etc

Kuna jamaa ninamfahami anapesa ameshakomaa kukiondoa kipara lakini amesanda. Njia nzuri Anza kunyoa nywele zibaki ndogo,.Jinsi kipara kinavyo ongezeka nawewe nae unazidi kunyoa kuendana na hiko kipara.

Unaona kina Idris sultan, Mr blue walikuwa wananywele kibao walikuwa wakibadili mitindo ya nywele karibia kila siku kama anavyofanya jux,,Lakini upara ulivyoingia nawenyewe wameanza kunyoa kipara, sio kwamba wanapenda hapana hiyo ndio best option iliyobakia na still wanapendeza.
 
Inategemeana na umbo la kichwa cha mtu. Kama ana kichwa kama kiazi au kile cha madenge,akinyoa kipara atakuwa kituko.
 
Habari zenu wana JF

Poleni sana na Swaumu naimani tunaendelea na Mfungo Mtukufu wa Ramadhani

Ndugu zangu nina miaka 25 Mzee wangu ana Uwaraza kwa Mbele hapa ule wanauita Upara wa Pesa. Sasa naona kama nimerithi kwake na maana nywele zangu za hapa Mbele zinakatika zinakua fupi kuliko nyingine halafu nikijiamgalia kwenye kioo naanza kuona ile Ngozi za kichwa kwa mbali.

So, wanadugu jamani kwa yeyete mwenye anajua dawa ya kutibu upara au uwaraza kwa njia yeyote ile iwe ni kwa kutumia dawa za asili ama kama kuna mafuta ya kununua ya kupaka please naombeni mnisaidie[emoji1488][emoji1488]

Wasiliana na Rooney.
 
Upara wa pesa hio siku hizi labda, zamani tunaita Airport hio.

Turudi kwenye mada, dawa ya asili ya kiuwaraza ni kunyoa kipara.

Dawa za kisasa zipo nyingi tu unaweza kuvaa wig au tafuta dawa inaitwa Minoxidil.

Kila la kheri
Bongo ipo? Na ni kiasi gan?
 
Back
Top Bottom