Ushauri: Namna ya kufanikiwa maishani

Joined
Oct 24, 2019
Posts
13
Reaction score
9
Kwema humu ndani?

Ningependa kupata ushauri/ namna ya kufanikiwa maishani kama kijana. Kwa ufupi mimi nina miaka 21, ni mwajiriwa sehemu fulani. Pia, nina mpango wa kuanzisha miradi yangu kufikia February 2020. Nina uwezo wa kutengeneza mpaka laki moja na elfu hamsini (150,000) kwa mwezi tofauti na mshahara wangu ila ninajikuta nashawishika kufanya starehe kama kwenda club every weekend. Natumia Mpaka laki moja kwa Ijumaa na Jumamosi na baada ya hapo Najuta why nisinge-save nifanye mambo mengine.

Kama mdogo wenu, naombeni mnisaidie. Pia, agemates mnisaidie kwa ushauri.

NB: Nina elimu ya kilimo na mifugo pia.
 
Cyphers Richardson

Kufanikiwa ni timing na bahati. Kuna watu tangia wanazaliwa ni bahati tuu mpaka kifo kinapokuja. Wengine tabu tu, hata wawe na kazi gani wanaishia pombe na magonjwa ila at the end of the day, 95 percent ya maisha yako yatategemea choice ya mke wako au mume wako. Life is about choices.
 
Sijawabagua mkuu....

Kama mdogo wenu naombeni mnisaidie Kwa Ushauri....... pia agemates mnisaidie Kwa Ushauri.........

Nidhamu kujituma ndio chanzo cha kufanikiwa ..jitahidi kuangalia opportunity mpya za kupata kipato.

Kingine acha starehe kama huna kipato,huwezi niambia unashindwa kujizuia wakati unaweza bana mkojo ukakojoa muda ujao, kwa nini ushindwe kupunguza na kuacha starehe.
 
Vitu unavyoona sio vya muhimu ndio unatakiwa uviache ikibidi uchague moja usave mshahara au hicho chajuu.

Ukifaulu zoezi la kusave hapo ni rahisi kutekeleza vipaumbele vyako kimoja baada ya kingine.
 
Ushauri wangu ni huu

Kwa ndoto ulizo nazo (ndoto za kufanikiwa), huwezi kuzitimiza kama hutabadili tabia

Badili tabia ya kupenda anasa. Kila binadamu duniani anapenda starehe, lakini ili ufanikiwe unatakiwa ujinyime. Kama upo bachela, kwa umri wako hiyo 150,000/= inakutosha kabisa. Hiyo 150,000 ya dili save kama mtaji. Kumbuka, hela za dili huwa zina mwisho wake. Chukulia kila senti unayopokea kama hela yako ya mwisho maishani mwako

Pia, angalia marafiki ulionao. Inawezekana marafiki (akiwepo/wakiwemo mademu zako) ndio chanzo kikubwa cha matumizi makubwa uliyonayo ikiwemo kufanya starehe. Tafuta marafiki wenye kiu ya mafanikio, sio marafiki ambao mwanzo mwisho story zao, ni za mademu, story za kulewa na za kwenda klabu.

Jinsi ya ku save. Mfano pato lako kwa mwezi ni Tsh 300,000. Kila unapopata fedha, tenga kwanza kiasi ulichopanga kutunza, halafu kinachobaki ndio fanya matumizi mengine.

Tambua kwamba, mafanikio (kiuchumi) ni mentality na si kiasi cha fedha unachoingiza, ndio maana, washinda bahati nasibu wengi wanarudi kwenye umasikini. Hata uwe na uwezo wa kuingiza kipato kiasi gani, huwezi kukuza uchumi wako ukiwa na poor mentality
 
Mbona maisha tayari unayo,cha kufanya hapo ni kuachana na sitarehe zinazokufanya utumie pesa unazopata bila mpangilio, kiasi utakachokuwa umekusanya ndicho kitakachokuongoza mradi wa kufanya kutokana na kiwango cha pesa ambacho utakuwa umekusanya.
 
Acha Wiz officer ... Kwahiyo company yenu hamtoagi receipt ?
whole sale sitoagi receipt 😂😂😂Coz I'm just like a street vendor when I'm doing my work.... Mzigo Upo ghetto Natoka nao asubuhi Napita madukani jioni au after some days napitia cash yangu kaka
 
nashukuru kaka ninafanyia kazi huu Ushauri kuanzia sasa na kuendelea
 
Mbona maisha tayari unayo,cha kufanya hapo ni kuachana na sitarehe zinazokufanya utumie pesa unazopata bila mpangilio, kiasi utakachokuwa umekusanya ndicho kitakachokuongoza mradi wa kufanya kutokana na kiwango cha pesa ambacho utakuwa umekusanya.
Nashukuru kaka
 
We njooo huku tuwe wote shoe shine

mi nakula vichwa na brash viatu vya madon wanasahau hela haooo

Hadi kwenye viatu so cha msingi njoo nikupe idea jinsi ya kuwa shoe shine
 
- pendelea kuongeza maarifa zaidi ya maisha kwa kusoma vitabu, kuongea na watu mbalimbali hasa waliofanikiwa zaidi yako na kuuudhuria semina na makongamano mbalimbali.
- weka malengo ya kuyafanikisha kila mwaka, kila mwezi hata kama hutaweza kuyafanikisha. Yatakusaidia kukuongoza na kukukumbusha cha kufanya mara kwa mara.
- Rahisisha mahitaji yako ya kila siku
- Jiunge na Saccos yoyote iliyokaribu nawe uwe unaweka akiba na kuzungusha hela zako huko na baadae uje upate msaada wa mkopo katika miradi yako
- Ongeza kipato chako kwa kuongeza vyanzo mbalimbali vya mapato kutokana na akiba ya fedha unazoweka na kupata. Mfano hiyo 150,000 inatosha kutengeneza kitoroli cha chuma chenye miguu ya pikipiki ambapo unaweza ukawa unakikodisha na kujipatia hata 3,500 kwa siku (fikiria viwe 10).
- Pendelea kuonana na marafiki zako uliosoma nao shule ya msingi, sekondari na vyuo. Watasaidia kukupa hasira kimaisha na kukukumbusha ulipotoka na ulipo na kukupa boosting ya kutafuta zaidi ili walau uwe sawa nao au uwe zaidi yao.
- Jifunze nidhamu ya pesa na uishi katika uelewa wa hicho ulichojifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…